SOMO; MAOMBI YA UKOMBOZI WA ARIDHI
SOMO: MAOMBI YA UKOMBOZI WA ARIDHI.
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Jifunze kitu kupitia haya maombi.
Aridhi Usipokuwa na nguvu ya kuitawala Adui na roho zitakutesa Sana. KILA Jambo liwe la Baraka au Laana Hushirikishwa Aridhi Adui anayetaka aharibu maisha yako hawezi kukudhuru endapo Aridhi na Anga ukiwa umevimiliki Ndiyo maana maandiko yanasema Ibarahimu Mungu alipotaka kumbariki alimwambia ondoka katika aridhi ya Baba Yako na mama yako na Jamaa uende mpaka nitakapokupa. Kwanini Asigembariki pale kutokana aridhi ya hapo alipokuwa Ibrahimu haikuwa aridhi iliyoandaliwa kwa ajili ya Baraka zake ilikuwa imebemba laana tu. SOMAπMwanzo:12
MUNGU Akasema
Mwanzo 1:28
[28]Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Nataka nikuambie ukitaka kumiliki Mfano.
Kazi
Biashara
Pesa
Kilimo
Majumba.
HUDUMA NK
LAZIMA UWE NA NGUVU YA KUTAWALA NA KUMILIKI ARIDHI.
Yoshua 1:3
[3]Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
SIFA KUBWA YA MTOTO WA MUNGU NI KUMILIKI BARAKA.
Tazama nyayo zako kisha ujue haya
1.Umekanyaga kata ipi kijiji gani wilaya gani na nchi ipi na Bara gani..?
2.Utataja Anga kwa kufata mtiririko juu wa kijiji kata wilaya mkoa na nchi.
3.Aridhi Utaishika chini
UTAOMBA HIVI.
1;Aridhi ninakuamuru uachie Kazi Yangu Ndoa Yangu Uchumi wangu Kila unachoona kimeshikwa mwambie Aridhi aachie.
Taja eneo ulipo unapoomba
Mfano.Aridhi wa kijiji cha mateteni nasema achia kazi yangu wilaya ya kilosa achia kazi yangu mkoa wa Morogoro achia kazi yangu unaenda kwa kuamuru hivyo mpaka Bara unalifikia kulitaja.
2.Kila uendapo kutafuta maisha au umepangwa kazi au umeenda Ugenini.
Isemeshe aridhi hivi Wewe aridhi wa eneo hili la Buza kanisani nimefika hapa kibiashara nimebemba Mchicha Ndizi,na vinywaji nakushika ukawalete wateja unasikia nakuamuru ulete wateja ifikapo saa nane mchana nimalize biashara yote.
Kama umeenda kikazi ombea upate kibali kwa eneo hilo lote. Kama umeenda likizo au Ugenini. ombea afya yako
3.SHUGHULIKA KWENDA KUISHi MAISHA KAMA YA WENYEJI
Nimefika hapa mimi nitakuwa watofauti na wakazi wa hapa aridhi nakuamuru nakujitenga na kila madhabahu za wenyeji aridhi nakuamuru ukalete Baraka Kwangu Katika Jina la Yesu.Amen
ππππππ
Kutoka 34:13
[13]Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.
Kama hujui hujawahi kuona mtu anaenda sehemu Maisha yake yanafanikiwa au maisha yake yanaharibika
Aridhi imebemba Vitu vingi kwako hata maneno yako ambayo ulitamkiwa laana Au ubaya wowote uliwahi kufanya yenyewe inakushuhudia kila dhambi ifanyayo ndiyo maana rahisi kwa Wachawi kutumia aridhi ikaharibu mafanikio yako.
OMBA KADIRI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUONGOZA JITENGEE MUDA UOMBE.
Maoni
Chapisha Maoni