SOMO:MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA UNAPOOMBA

SOMO: MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA UNAPOOMBA. 

Kuna vitu ni vya muhimu Sana Kufanya Maombi Yako Yafike mbele za Mungu na ujibiwe.


1:MUDA WA KUOMBA.
Jifunze unapotaka uingie maombi yoyote mfano unaombea kitu au unaombea familia yako 
Hakikisha unaweka muda wa kuomba Huo muda utapatana na Roho Mtakatifu na Mungu mwenyewe nawewe simamia huo muda maana katika ya huo muda ndio Mungu atashuka akuhudumie.

Mfano umesema kila siku nitaamka saa sita usiku nianze kuomba mpaka saa nane simamia huo muda ulioutamka usipishane nao.

Kwa Kufanya hivyo utayafanya maombi yako yawe yanajibiwa haraka.


2:TUBU.
Hakikisha kama unajiona uliwaza vibaya au ulimunug,unikia Mungu au ulikata tamaa, au ulifanya dhambi Yoyote unaitubia hiyo dhambi. 

Upotubu Hakikisha unapiga magoti na unaijutia dhambi yako kwa maombi ya kuugua na kuijutia dhambi hiyo.


3:UWASILISHAJI WA MANENO.
Hakikisha unatamka maneno yanayoeleweka Yenye hekima na utaratibu maalumu usiende kuomba mbele za Mungu ukitumia lugha za mitaani 
Mfano. BABA WA HEAVEN NINAKUOMBA UJE UFANYE UNIPE KAZI NA NILIKUOMBA UNIPE NDOA HUJANIPA

UTAONA MTU HUYU HAJAPANGA VYEMA MANENO YAKE.

SAHIHI; Baba wa mbiguni nikakuomba uje ufanye mapenzi yako kwangu ukanipe kazi na ndoa sahihi ninakuomba katika Jina la Yesu.Amen 

KUWA MAKINI KWENYE UTAMKAJI WAKO WA MANENO.



4:SADAKA 
Hakikisha Maombi yako unapokuwa unafunga au umejiwekea utafunga siku 7 au 30 hakikisha siku ukija kufungua kumaliza unadaa Sadaka yako unaitoa kwenye madhabahu yako wewe

Pia usifunge kuanzia asubuhi mpaka jioni hujaomba mpaka unaenda kufungulia hujaomba

Hakikisha Unaomba Kabla hujafungua na Unaomba baada ya kufunga


Nashukuru kwa nakala hii
Mwaandaaji Roho Mtakatifu na Kuwasilishwa kwenu na Pastor Richard Kutoka Kanisa la Holy Spirit Tanzania 
Yupo Morogoro Veta Dakawa 

Mfate WhatsApp mwambie akuuge kwenye Group la Maombi +255759861768

Rejea Mathayo;17;21
Isaya:61:1-10

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.