MAMBO 20 YA KUFANYA UKITAKA UMFURAHISHE MUMEO

MAMBO 2O YA KUZINGATIA UNAPOTAKA MUME WAKO AFURAHIE NDOA YENU

Mithali:12;1_5 
Karibuni katika Darasa la Wanandoa +18 Tuongeee na Kupeana elimu katika Njia yenye kujenga ndoa zetu katika kipengele cha kuwapokea Wanaume wapotoka Kazini na mambo yanayomfurahisha mumeo
Mwalimu anayekuletea Darasa
NAITWA PASTOR RICHARD 
WHATSAPP NUMBA +255759861768

1:Unapomkaribisha mume wako hakikisha unaanza kwa kupokea mzingo wake kisha msalimu kwa heshima (piga magoti) nakumkaribisha.

2:Unapoanza Kuongea naye anzia kumweleza Habari nzuri na kumpa Pole kwa mihagaiko kisha muulize anaenda kuoga au Anakula kwanza.

3;Hakikisha Unakuwa msafi na unaoga vizuri mumeo anaporudi akukute upo msafi.

4;Safisha nyumba yako na Kutandika kitanda chenu vizuri mumeo asirudi akute chumba hakijatandikwa.

5.Badilisha mitindo ya nywele Na Kuvaa nguo anazozipenda mume wako.

6.Mshukuru Mumeo Kwa Kile kindogo anachokupa mwambie Ansate mfalme wangu. Fanya mara kwa mara.

7.Usimuite mumeo majina haya mume/Jeremia/rafiki yangu/nk
Baadala yake muite mume wangu,Baby,sweetheart, Baba fulani,nk 

8;Mtii mume wako nakumsikiliza.

9.Ukiona mumeo hayuko vizuri subiri kwanza awe sawa ndiyo uanze kuogea naye mambo ya mipago yenu.

10;Mwadalie mumeo chakula mwenyewe  na kaa kula nae kama akiwepo.

11;Kuwa faraja kwake anapopitia mambo magumu epuka nawewe kumchaganya.

12;Badilika na Kuacha Yale Anayokuambia yanamuuzi isipokuwa Habari za Mungu.

13:Mfundishe na Kumusahihisha kwa lugha ya upole na utii.

14: Muombe Musamaha ukimkosea

15;Akikasirika na kuanza kufoka nyamaza usimjibu kitu.

16;Usiongee Habari ya kumpenda Sana shemeji yako wa kiume kumpenda mtu yeyote wa kiume usizungumze hayo mbele zake

17;Usitumie ovyo Pesa anazo kupa simamia mali vizuri mnayojaliwa.

18;Jilinde na Kujitunza Usimsaliti.

19;Mushauri kwa uaminifu wa fungu la kumi muwe waaminifu.

20;Wapende Wanae na Wazazi wake

Mshajiishe na umhamasishe mumeo kupunguza matumizi na kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya sadaka na kuwasaidia maskini na wale wenye dhiki.
21. Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo.
22. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.

23. Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: “Kwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?” Epuka hali hiyo.

24. Daima kuwa mtiifu kwake.

25. Shikamana na mumeo, hususan katika nyakati za shida, dhiki, maradhi au mumeo anapofilisika au anapokuwa hana pesa.

26. Muunge mkono kupitia kazi yako, fedha yako au mali yako pindi inapohitajika.
27. Fuata maagizo yake, isipokuwa katika mambo ya haramu. Katika Uislamu, mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

28. Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha.
29. Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.
30. Ukimkosea muombe msamaha.

31. Akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye. Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.

32. Akiwa na hasira kutokana na mambo ya nje ya nyumba basi subiri mpaka atakapoondokana na hasira hiyo.

33. Mpe faraja na kumuonea huruma, yumkini akawa amechoka, ana matatizo ya kikazi au kuna mtu kamtusi, n.k.

34. Usimuulize maswali mengi au kung’ang’ania kutaka kujua yaliyotokea. Mathalan, kuna wanawake wengine wakiona mume ana hali tofauti huanza kusema: Niambie kumetokea nini? Lazima utaniambia kilichokufanya mpaka ukawa na hasira hivyo… unaficha nini? Nina haki ya kujua au kuna mwanamke kakuvuruga?

35. Jilinde dhidi ya mahusiano yaliyoharamishwa.

36. Tunza siri za familia, hususan mambo ya chumbani na mambo mengine ambayo mumeo hapendi watu wayajue.

37. Usisahau kushughulikia vizuri malezi ya watoto na huduma za nyumbani. Mumeo atafurahia kula chakula ulichompikia na chenye virutubisho.

38. Zilinde mali na fedha zake.
39. Usiende matembezini au nje ya maeneo ya nyumbani bila idhini yake; unapotoka vaa mavazi sahihi.

40. Usiwakaribishe au kukutana na watu ambao hapendi ukutane nao.
41. Usikae faragha na mwanaume yeyote ambaye sio mahram wako.
42. Kuwa mwema kwa wazazi na ndugu zake. Wakaribishe wageni wake.
43. Jitahidi sana kuepuka migogoro na ndugu zake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.