Maombi ya kuvunja agano la kitovu
1;Yesu Kristo Mnazareti ninakuja mbele zako siku ya leo ninavunja kila agano lililosimama kinyume na wewe katika Maisha yangu,liniachie Leo kwa Jina la Yesu.Amen
2.Kila agano la ndoa lililofanyika kwenye ndoto nilipovishwa pete nalivunja,pete hiyo naichoma kwa moto wa Roho Mtakatifu.Agano hilo la ndoa limekosesha ndoa yangu amani,limefanya nisipate mwenzi sahihi,Kwa uhalali wa Damu ya Yesu nalivunja Leo .Amen
3.Kila agano lililosimama katika Maisha yangu Kupitia viungo vyangu vya mwili au chochote changu kilicho pelekwa kwenye nyumba za waganga.Iwe ni kitovu changu,unywele wangu wa kwanza ulionyolewa nilipokuwa mchanga,iwe Ni kucha zangu,nguo zangu,kalamu yangu,mchanga wangu,jasho langu,Leo Hii KWA Mamlaka ya Jina la Yesu napangua nabatilisha Navunja KWA jina la Yesu.Achia Maisha yangu,Mimi si wa kwako Tena KWA jina la Yesu.Amen
4.Baba Tazama Mimi mwanao nilienda kwa waganga wa kienyeji nikatoa sadaka,KWA mikono Yangu nikapokea hirizi ,nikachanjwa.Leo hii chale hizo zimesimamisha maagano katika Maisha yangu .Navunja maagano hayo,Kila chale nafuta KWA Damu ya Yesu, nazimaliza nguvu hazitakuwa na madhara Tena .KWA jina la Yesu Kristo Mnazareti.Amen
5.Bwana Yesu Kristo nilipoenda kwa waganga,niliagizwa kutoa kafara ya ndege na wanyama, Damu zao zikamwagwa kwenye ardhi,ardhi inanidai ,nikajiunga katika maagano ya kuzimu.Baba Tazama ,Leo Hii Najiondoa kwenye hayo maagano,nayavunja najitenga nayo kwenye ulimwengu wa Roho,kwa Jina la Yesu Kristo.Amen
6.Baba Tazama,nilitamka maneno fulani,nikatamkiwa na mengine pia,kumbe maneno hayo yaliniungisha kwenye maagano ya mateso .Leo Hii natumia Damu ya Yesu,nafuta hayo maneno,nafuta kila Habari chafu kunihusu,kwa Jina la Yesu.Amen
7.Kuna madhehebu niliyoenda Baba,kumbe niliabudu Miungu na sanamu pasipo kujua,sadaka nikatoa Baba,Miungu hiyo ikaniungisha kwenye maagano.Leo hii nahangaika,hakuna kinachosonga mbele,Hata kiroho nimepoa Sana,siombi Kama zamani ,sisomi neno Baba,macho yangu na masikio yangu ya kiroho yamefungwa.Kwa Damu ya Yesu,naangusha hayo maagano,nafuta kila hukumu ya Miungu kwenye Maisha yangu,kwa Jina la Yesu.Amen
8.Baba,nilitoa mimba,nilishawishi na wengine kutoa mimba,nilisimamia mchakato wa utoaji mimba.Nikajiungisha kwenye maagano na kuzimu.Niliwapa Damu na nyama,Ardhi inanidai,sauti zinanidai.Kwa Damu ya Yesu nafuta hayo maagano na kuzimu.Nanyamazisha kila sauti kwa Damu ya Yesu,kwenye hiyo ardhi nanyunyiza Damu ya pasaka.Wewe kuzimu sikia neno la Mungu,futa hayo maagano KWA Jina la Yesu,achia Maisha yangu Sasa na KILA ulichoshikilia.Natakasa tumbo langu la uzazi KWA Damu ya Yesu.Amen
9.Baba kuna wakati niliota ndoto fulani,kwamba nazini,sikujua ninaingia kwenye maagano na jini Mahaba,Leo Hii KWA uhalali wa Damu ya Yesu,Navunja KILA Kazi ya jini Mahaba,beba virago vyako na uondoke,sikia,sikutaki Tena Mimi Ni wa Yesu.Natakasa malango ya ndoto zangu kwa Damu ya Yesu.Navunja maagano na jini Mahaba KWA Damu ya Yesu,kwa Jina la Yesu Kristo.Amen
10.Kuna vyakula na vinywaji nilikula Baba,kwenye ndoto na kihalisia.Nikajiungisha kwenye maagano Baba,maagano yanayonitatiza,yananihangaisha mno.Baba agano lililofanyika Kupitia vyakula Hivyo Navunja,nafuta kazi ya vyakula Hivyo kwenye Maisha yangu KWA Damu ya Yesu,kwa Jina la Yesu Kristo.Amen
Maoni
Chapisha Maoni