SOMO:UDHIBITISHO WA YESU KUFUFUKA

SOMO:UDHIBITISHO WA YESU KUFUFUKA.


UTANGULIZI. 

Kwanza Jiwe lilowekwa Kwenye Kaburi Lilikuwa Kubwa Sana Kiasi Kwamba Mtu asingelisogeza Lakini limesongezwa Walizi nao walikuwa na silaha kali za moto hawakuweza kuona Tukio hilo Kitu cha Kushangaza Sada inaonekana mtu aoenekani Hili ndiyo liloshutua wengi mpaka kuingia kaburini watazame kweli hayumo

Kama Tunavyoshuhudia kaburi mtu aliyekufa akizikwa huwa ni ngumu Sana mtu kutoka Lakini Bwana Yesu Yupo huru Amefufuka.

Naitwa Pastor Richard 

Nipo Veta Dakawa Morogoro Nchini Tanzania

 🇹🇿 Yohana 20:5

[5]Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. 


Nakuletea udhibitisho huu wa Yesu yupo hai Tena



1:KWANZA KABURI LIPO TUPU

🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉

Thibitisho la kwanza la kufufuka kwa Yesu ni kaburi tupu. Ukweli kwamba kaburi la Yesu lilikuwa tupu siku tatu baada ya kufa kwake ni thibitisho kuu la kufufuka kwake. Waandishi wote wane wa Injili wanakubaliana kwamba kaburi la Kristo lilikuwa tupu siku tatu baada ya kufa kwake. Washuhuda wengine wengi pia walithibitisha ukweli kwamba kaburi lilikuwa tupu.

Shambulizi la zamani kabisa la kufufuka kwa Kristo ni kule kusema kwamba mtu aliiba mwili wake. Makuhani wakuu

“…wakawapa askari fedha nyingi, wakisema, semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala…Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo” (Mathayo 28:12-15).

Lakini maneno haya hayakuwashawishi watu wengi. Akili ya kawaida itakwambia ya kwamba Wanafunzi hawakuiba mwili wake halafu wanjifanye kwamba amefufuka. Siku tatu zilizotangulia Wanafunzi walikimbilia maisha yao wakati Yesu alikamatwa na kusulibiwa. Haionekani ni ukweli kwamba watu hawa waliojawa na woga wangepata ushujaa wa kuiba mwili wa Yesu – halafu waanze kuhubiri kwa ujasiri ya kwamba alifufuka kutoka kwa wafu – jambo ambalo lilihatarisha maisha yao! Hapana, hilo ni jambo ambalo halingewezekana kabisa! Madai hayo hayaambatani. Wanafunzi walijificha katika chumba na mlango ulikuwa umefungwa, “kwa hofu ya Wayahudi” (Yohana 20:19). Walikuwa katika mshtuko. Hawakuamini kwamba angefufuka tena. Hakuna yeyote katika wafuasi wa Kristo ambaye alikuwa na imani au ushujaa wa kubishana na serikali ya Warumi iliyokuwa na nguvu na kuiba mwili wa Yesu. Huo ni ukweli wa kisaikolojia ambao hauwezi kupuuzwa.

Wachukiwa wengine, ambao wangeuiba mwili wa Kristo, ni maadui wake. Tatizo la dhana hiyo ni kwamba maadui wa Kristo hawakuwa na nia ya kupora kaburi lake. Makuhani wakuu na viongozi wengine wa dini walimuua Kristo kwa sababu alitishia desturi ya dini yao na jinsi walivyoishi. Jambo ambalo hawa watu hawangelipenda ni kwamba watu wafikirie Kristo yu hai tena! Hiyo ndiyo sababu hawa viongozi wa dini walifanya juhudi kuondoa jambo lolote kuhusu kufufuka kwake. Injili ya Mathayo inatwambia ya kwamba walienda kwa liwali wa Warumi, Pontia Pilato,

“Wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjaja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza” (Mathayo 27:63-64).

Pilato aliwaambia wachukue askari na walilinde kaburi “salama kadiri mjuavyo” – muwaweke askari kwa kaburi na mlilinde kadiri mwezavyo (Mathayo 27:65). Hivyo walilitia lile jiwe la kaburi muhuri na wakawaweka walinzi pale kulilinda (Mathayo 27:66). Ajabu, ilionekana kwamba hawa makuhani wakuu na viongozi wa dini walikuwa na matumaini ya kufufuka kwa Kristo kuliko walivyoamini Wanafunzi wake!

Ukweli ni kwamba wakuu wa dini walitumia taratibu za upeo kuzuia mwili wa Kristo usiibiwe. Walitaka kuthibitisha kwamba ahadi ya Kristo ya kufufuka kutoka kwa wafu ni uongo. Wakuu wa dini walifanya chochote walichoweza kuondoa uwezekano wowote wa habari kuenea kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Kuiba mwili lingekuwa jambo la mwisho la maadui wake kulifanya. Lakini kama wangekuwa waliuiba mwili, bila shaka wangeutoa wakati ambapo Wanafunzi wake walianza kuhubiri kuhusu kufufuka kwake. Lakini maadui wa Kristo hawakuutoa mwili wake. Kwanini? Kwa sababu hawakuwa na mwili wa kutoa! Kaburi lilikuwa tupu! Kristo alikuwa amefufuka kutoka kwa wafu!

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

Kaburi tupu ndilo thibitisho la kwanza la kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu, lakini kuna mengi!

2: WALIOSHUHUDIA WAMESEMA KABURI. 

🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇

Yesu aliposulibiwa, Wanafunzi wake walikosa tumaini. Imani yao iliharibiwa. Hawakuwa na tumaini kwamba watapata kumwona tena akiwa hai. Halafu Yesu akaja,

“akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu” (Yohana 20:19)


3;MATESO WALIYOYAPATA WANAFUNZI WAKE.

🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉

Watu hawa walikufa kwa sababu walisema ya kwamba walishuhudia kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu:

Petro – alipigwa mijeledi halafu akasulibiwa kichwa kikielekea chini.

  Andrea – Alisulibiwa kwa msalaba uliokuwa na umbo la X.

    Yakobo, mwana wa Zebedayo – alikatwa kichwa.

      Yohana – alitiwa birikani ya mafuta yanayochemka, halafu

      wakamhamishia kisiwani cha Patmo.

        Filipo – alipigwa mijeledi halafu akasulibiwa.

          Bartholomayo – alichunwa ngozi na kusulibiwa.

            Mathayo – alikatwa kichwa.

              Yakobo, nduguye Bwana – alitupwa kutoka juu ya hekalu,

              na halafu akapigwa hadi akafa.

                Thadayo – alichomwa na mishale hadi akafa.

                  Marko – alikokotwa chini hadi akafa.

                    Paulo – alikatwa kichwa.

                      Luka – alisulibiwa kwa mti wa mzeituni.

                        Tomaso – alichomwa na mikuki,

                          na akatupwa katika miali ya tanuru.


Rejea vitabu Hivi Kavitafute.

(Kitabu cha wafia dini cha New Foxe, Bridge-Logos Publishers, 1997, uk. 5-10;

Greg Laurie, Kwa nini ufufuo? Tyndale House Publishers, 2004, uk. 19-20).


Watu hawa walipitia mateso makali, na wakafa vifo vibaya, kwa sababu walisema kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Watu hawafi kwa jambo ambalo hawajaliona! Watu hawa walimuona Kristo baada ya kufufuka kutoka kaburini! Hiyo ndiyo sababu mateso na kifo chenyewe havingeweza kuwasimamisha wasitangaze, “Kristo amefufuka kutoka kwa wafu!”



HITIMISHO 

Tunaudhibitisho wa Kutosha Juu Ya Tukio la Yesu Kufufuka kutokana na vitabu mbalimbali na Biblia vilivyoandikwa nakuweka udhibitisho Sasa Nasi Kuna Kitu cha Kujifunza Kama wezetu waliokubali kufa kwa ajili ya kushuhudia ukweli.



Wito

Karibu ujiuge nasisi WhatsApp Pastor Richard +255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.