SOMO;MAADILI YA UVAAJI KWA MKRISTO
SOMO: MAADILI YA UVAAJI WA MKRISTO KATIKA MAANDIKO.
UTANGULIZI
Tuache Kujifariji na Kudaganyana Kwa kuwafundisha watu kuwa Mavazi Kwa mkrito ni moyo wake na siyo muonekano wa nje hali ambayo inapelekea wakristo wengi kuuguka kiroho na kupoteza ushuhuda mzuri ndani ya kanisa mimi Leo nataka nikufundishe mavazi ya kimwili na wewe kiroho yanaenda sababa nitafundisha kwa ushahidi wa maandiko Biblia inasemaje
Nayekuandalia Somo hili na kuliwasilisha kwako
Naitwa Bishop Richard Ninaishi Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Moto Wa Yesu.
1:(a)KWA MKRISTO MWANAMKE HAPASWI KUVAA MAVAZI YA MWANAUME
Kama.
Suruali,Pesi, nk
Mwanamke anayevaa haya mbele za Mungu anakuwa mwenye dhambi kwa kuwa kashindwa kutii angizo au alivyoamriwa na NENO.
(b)MWANAUME HATAKIWI AVAE NGUO ZA MWANAMKE
Kama Gauni,nk
Mwanaume Yeyote mwenye kuvaa mavazi yampasayo avae mwanamke Yeye akavaa Tayari utakuwa mwenye dhambi mbele za Mungu umeshindwa kutii Neno lake
✍✍✍✍TUSOME
Kumbukumbu la Torati 22:5
[5]Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
MADHARA YA VAZI HILI.
Ni kumchukiza Mungu na Kukuona Kama mtoto mkaidi usiyemtii Baba Yako.
Kuwa makini unaweza ukakosana na Mungu kwa kitu kidogo sana kusimamia uvaaji wako.
2;MKRISTO USIVAE MAVAZI YA KIKAHABA YATAKAYOACHA WAZI MAUMBO YAKO.
Soma kitabu hiki
Mithali 7:10
[10]Na tazama, mwanamke akamkuta,
Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
Kumbukumbu la Torati 23:17
[17]Pasiwe na kahaba katika binti za Israel.
Mavazi yanayobana sana nakuonesha mwili wako kwa ndani na mavazi yasiyo na staha kwa Mwanaume na Mwanamke Hata kama akiwa mtu wa heshima yatamtambulisha Kama kahaba.
Kahaba ni mtu anayetumia mwili kujipatia kipato kwa kuuza mwili wake na kushawishi watu kwa uvaaji wake.
MADHARA YA UVAAJI WA KIKAHABA.
Utasababisha watu wengi waanguke katika dhambi ya uzinifu wa mawazo na utasababisha Yesu wako atukanwe na watu wa mataifa hata kama ukiwa hutendi ukahaba lakini ile nguo tu itakutambulisha tabia yako kwa watu waliokuzunguka..
Soma mithali;23:27
NGUO UNAZOTAKIWA UVAE KAMA MKRISTO
🍉🍉🍍🍍🍍🍍🍍🍍🍉🍉🍉🍉🍉🍉
3:MKRISTO UNAPASWA UVAE NGUO NZURI
ZITAKAZO KUFANYA UONEKANE VIZURI.
Kama nguo zisizobana, Nguo zinazoachanisha umbo zishike umbo lako
Sawasawa na andiko hili.
Unahamasishwa ni wewe ujitambue kama Mtakatifu vaa nguo zako nzuri zenye heshima
Isaya 52:1
[1]Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;
Jivike mavazi yako mazuri,
Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;
4:MKRISTO VAA NGUO ZA HADHI YAKO KULINGANA NA NAFASI YAKO KANISANI.
✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍
Kama Mchungaji unatakiwa uvae mashati mazuri au suti zuri suruali nzuri kutokana wewe unaigwa ni mfano kwa wale unaowaogoza katika roho.
Ukivaa nguo za hadhi zinakufanya uheshimike hata unaposimama kuongea kitu na kumshuhudia Yesu wako wanakusikiliza ujumbe unafika kwa unaowahubiria.
Tusome huu mstari.
Mithali 31:25
[25]Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
Utaheshimika kutokana na uvaaji wa nguo zenye hadhi popote unapoenda ofisi yoyote utapata kibali.
Yakobo 2:3
[3]Nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,
5:MKRISTO UNAPOVAA VIZURI VAZI LA HESHIMA.
Unatangaza nuru na kuwafanya watu wavutiwe na ucha Mungu wako kutokana huvai mavazi ya ovyo ovyo .
Wewe ni nuru usisahau hilo
Zaburi 104:2
[2]Umejivika nuru kama vazi;
Umezitandika mbingu kama pazia;
HITIMISHO
Tengeneza Uvaaji wako uendane Sawaswa na unayemhubiri au kumshuhudia kwa mataifa yasiyo mjua Mungu jiweke maridadi nyosa nguo zako na jiweke kuwa safi uendapo nyumbani kwa Bwana.
Mungu anataka uje nyumbani kwake umavaa mavazi yanayoendana na heshima yake Kama Mungu Baba.
WITO
Je unatamani uache Tabia fulani kupitia somo hili umejifunza kitu au unataka kuokoka
Piga jioni saa 12:00 mpaka 2:00Usiku
+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni