SOMO;ACHA KUSIKILIZA MAPEPO
SOMO; ACHA KUYASIKILIZA MAPEPO《 ACHA KUSIKILIZA MAGONJWA, ACHA KUSIKILIZA MATATIZO MSIKILIZE YESU TAYARI AMESHAKUFUNGUA.》》
●●●●●●□□□□□●●●
Vitabu Rejea:1samweli:28:7-10, 1wafalme:22;22-23 Ayubu;4;15, Mathayo;8;30-34
°°°•••••°°°°••••••••▪︎▪︎▪︎°°°°•••°°°°°°°
Naitwa Pastor Richard
Ninayekuandalia Somo hili na kuliwasilisha Kwako Leo 30/04/2022
Karibuni Katika Somo hili linalosema[ "ACHA KUSIKILIZA MAPEPO"]
Linalenga kukufungua wewe usiyesikia watumishi wanaposema Umefunguliwa Umeponywa ukirudi nyumbani yanaanza mawazo ya kukurudisha kwenye magonjwa tena hizo huwa sauti za MAPEPO zinakufanya Umepona Leo Kesho unaumwa tena Umetoa zaka Leo Kesho unaacha. Ujue unateswa na MAPEPO Soma kwa umakini rudiarudia uelewe vyema.
MAANA YA PEPO
PEPO Ni Nini?
Ni roho chafu zenye umbo la mtu visivyoshikika vipo kama moshi au Upepo.
Ni moja ya Jeshi la Shetani linalomshambulia mwanadamu kuzuia malengo afya na maono yake.
DALILI ZINAZOKUJULISHA UNASIKILIZA MAPEPO.
__________________________________________
1:Kusikia Sauti ikikuamuru ukate Tamaa au Urudi nyuma Umuache Mungu.
Hapa utaanza kujiona unakata tamaa na kuanza kulaumu watu ooh mimi nilimsomesha lakini hanijali Natoa Zaka Mungu hanijibu Nimechangia Ujenzi wa kanisa Mungu hajatenda nk.
2;Kusikia Sauti Au Mawazo Usitoe zaka katika madhabahu yako au Usimtolee Mungu chochote.
Hapa Utajiona Taratibu Unaacha Kutoa zaka unaanza visababu mara siuzi siku hizi mara mshahara wote unakatwa mara nasomesha.
Ukijiona hali hii ujue Unayasikiliza Mapepo.
3;Kusikia Sauti Ukiwa Unaombewa Inasema nawe wakati mwingine huwaambia usidodoke au empire Mtumishi au mtukane mtumishi.
Utaona nguvu ya Mungu inaingia wewe unaizuia unajiona kama unatapika unaanza kujizuia au Unahisi Kudodoka unajikaza
Ukiwa unaona dalili hii unasikiliza MAPEPO ambayo hayataki upone.
4;Kusikia au kuja mawazo mabaya akilini mwako unaanza kuiwaza dhambi uliyokuwa umeiacha.
Utaanza kuwawazia mabaya watu au Watumishi au ndugu zako
5;Kuombewa Unafunguliwa lakini mawazo yako unakuwa unajiona kama bado hujafunguliwa.
Utaanza kujiona bado mbona hali hii kama inanirudia Pastor Richard alisema Tumbo nimepona mbona linaniuma Bado sijapona
Mtumishi akikwambia Kitu Ujue imeshakuwa ukianza kujiuliza utayapa nafasi mapepo yakuongoze.
6;Kusikia Mawazo ukazini Usiende ibadani Usiombe nk.
Utaenda kudanga au kutafuta mtu uzini nae
7;Kuahirisha kwa malengo mara kwa mara au Kuwa ni Visababu vingi kipindi unapoambiwa habari za Mungu.
Hapa utaanza kuwa muogeaji lakini sio mtekelezaji
8;Kuuacha Wokovu na Kujiuga na Dunia kuyatenda Yote Yachukizayo Kwa Mungu.
Utarudia Matendo machafu yaleyale uliyoambiwa yaache
9;Kuwa mtu usiyesikia maelekezo Ya Mungu ukielezwa yote yanafutika.
Utapuuza Mtumishi anachokuelekeza
10:Kuteswa na dhambi unaiacha lakini Baada ya miezi unairudia kuifanya.
Utakuwa unarudia rudia dhambi uliyoiacha.
MADHARA MATATU MAKUBWA YA MTU KUSIKILIZA MAPEPO
1;Tatizo Lake Kutokuisha.
2;Mungu hatamsikiliza atayatiii mapepo na Kumtumikisha
3;Kuwa mtu wa MATESO yasiyoisha.
NINI UFANYE SASA.
Amini Neno ulilotamkiwa na mtumishi lilonjema kuwa imekuwa hivyo usione mashaka ndani yako fata maelekezo aliyopewa na Mungu Kwako na Kama humwamini hugo Mtumishi omba Mungu akueleze ni kweli. Usiache Kutii Bila kuuliza kwa Mungu.
HITIMISHO
Matatizo mengi ndani ya watu yanasababishwa na watu KUSIKILIZA MAPEPO yanayokuwa yanawaongelesha kwenye mawazo yao.
Wito
MTAFUTE Pastor Richard kwa WhatsApp Pastor Richard +255759861768
Maoni
Chapisha Maoni