Somo;Tabia 7 za Malaika

      SOMO: TABIA 7 ZA MALAIKA.


  KARIBU KATIKA SOMO HILI UJIFUNZE KITU   KUHUSU Somo hili la Tabia Za Malaika.

Naenda Kuongelea Tabia Walizonazo malaika kule mbinguni

1;Ni Watiifu.


Malaika wanatabia ya utiifu hwana Neno hapana kwa Mungu au Viongozi wao kila kitu husema ndio wanachoamriwa kufanya.
Tusome;Mathayo:6;10 Zaburi;103;20

2;Ni Wacha Mungu Sana.


Yaani Malaika Kazi Yao Kubwa Kumcha Mungu Usiku na mchana muda wote hufanya hivyo mbinguni.
Tusome;Nehemia;9;6 Filip;2;9-11

3;Ni Wenye Busara Sana.


Malaika hufanya kila jambo kwa hekima busara na maarifa ya juu.

1Petro;1;12, 1wafalme;8;39


4.Ni Wanyenyekevu.


Malaika Wanatabia Ya Kunyenyekea
Hawachukii wala kununa wala kupigana
2Petro:2;11,Yuda.9

5.Ni Wenye Nguvu Sana.


Malaika mmoja anauwezo wa kuua majeshi au malaika wa shetani 1000
Anauwezo wa kuua Taifa au nchi nzima  malaika mmoja Tu. Wananguvu kuliko kawaida.
Tusome 2wafalme;19;35,Ufunuo.18:1,21

6;Ni Watakatifu Hawana Dhambi

 
Malaika hana dhambi Yeye ni mtakatifu.
Ufunuo:14;10 Marko;8;38

7;Wanapenda Kusifu na Kuabudu.;


Kazi Kubwa Ya Malaika Kumwabudu Mungu na kumchezea Bwana Mbinguni huwa wanafilimbi zao na Wanafurahi muda wote wanapomchezea Bwana.
Luka;2;13 Ufunuo:4:8 Waebrania;1:6.

  HITIMISHO


Tunapaswa Tuinge Tabia hizi za malaika kufanya maisha yetu yawe matakatifu Yenye utukufu kwa Mungu.
Tabia ipi unafanya uifanyie kazi kati ya hizi.


   WITO


Kama Somo hili umelipenda share kwa magroup yako ndugu zako

 
Kama Unaswali Uliza inbox


NAITWA PASTOR RICHARD
Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.