SOMO;MAADUI WA 5 KATIKA MAISHA YAKO
SOMO: WAJAUE MAADUI WA 5 KATIKA MAISHA YAKO.
JUMAPILI KANISANI LEO
▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎▪︎
Karibu Kuna Maadui Wanne Hatari Kwenye Maisha Yetu Ambao Ni Vyema Uwajue.
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
WhatsApp +255710889892
Karibu
1:ADUI KAINI. TUNASOMA (MWANZO;4;2-25
Hawa ni Maadui Ambao Wanaojifanya wanakupenda ndani ya moyo yao wana mikakati mibaya Juu Yako.
SIFA ZA WATU HAWA
1:Ni watu wanaojifanya wanakupenda kumbe wauaji.
2;Ni Watu Wanaofanya Uadui nawewe Kwa Siri ni ngumu kuwajua hivihivi.
3:Ni watu Wasiopenda wewe Ufanikiwe wanapenda wao tu wafanikiwe.
4:Wanaushauri Na Nia Ya Kukuzunguka Kipindi Ukifanikiwa ukawazidi.
5;Ni watu wanaona wivu kila uwapitapo hatua moja ya maendeleo.
6;Ni watu wanaweza kukuwekea hata sumu wakue.
TUFANYE NINI KUWAEPUKA ADUI HAWA
1:Tusiwape nafasi kubwa ya kujua malengo Yetu
2;Tumuombe Mungu atuepushe nao.
2:ADUI DELILA Tusome WAAMUZI;16;1-20
Hawa ni Kundi la Watu Wanaotumwa na watu au wafatiliaji wa maisha yako kisha huzitoa nje kwa adui zako siri za maisha yako au kukwendea kwa mganga.
SIFA ZAO HUWA HIVI.
1:Ni watu wanataka kujua siri za maisha yako au mafanikio.
2:Ni watu waliotumwa Kuyachunguza .maisha yako kisha kuyatangaza nje ulivyo.
3;Ni watu Wanaotumia Udhaifu Wako Kukutesa
4;Ni Watu Wanaoweza Kujifanya wapo nawewe kumbe kuna kitu wanakitaka kwako.
5:Ni Watu Wanaotumiwa na wapagani kukuharibia maisha yako
6;Hutumia Siraha ya ukaribu nawewe.
TUFANYE HAYA KUEPUKANA NAO
1;Kutowapa nafasi ya kutuzoea
2:Ni watu wakukaa nap mbali
3:ADUI PENINA Tusome 《1SAMWELI;1;1-7》
Hawa ni watu wanaokukatisha tamaa na kukucheka kuwa huwezi.
SIFA ZAO WATU HAWA.
1:Chochote utakachowaambia watakutangaza kwa wegine.
2:Ni watu waogo na Wazushi waoeneza habari zako zisizo za kweli.
3:Watakuvunja Moyo na Kukudharau huwezi.
4:Wataishi na Wewe Kwa Vita Ya Maneno ni wepesi kukutengenezea mazingira ya kesi.
5;Kina Penina Huwa kazi yao kusema wengine.
TUFANYE HAYA KUEPUKA.
1:Kuwaonya nakuwakemea
2:Kutokuwaambia maisha Yetu
3;Kuwa bize nakanisa.
4:ADUI HARMAN Tusome( Esta Sura 3,4,na 5
Hawa ni Watu Wanaotengeneza kuyaharibu maisha yako au kukugeuka nakwenda kinyume nawewe.
SIFA ZAO ZIPO HIVI
1:Ni watu wanaojipendekeza kwa boss waonekana wanapiga kazi.
2:Ni watu wanaopenda kazi yako ife au uondoke wasikuone.
3:Ni watu wanaoishi kazini kwa ukabila.
4;Ni watu Wanaowaua wegine kwa sababu ya cheo au masilahi furani
5;Sio watu wazuri hao maana ni hatari
TUFANYE NINI SASA
1:Epukana nao kabisa
2:Ukiwagundua Kaa nao mbali.
5:ADUI YUDA Tusome 《MATHAYO:26;10-50
Hawa ni watu wasaliti wasioaminika muda wowote wanaweza Kukusaliti
SIFA ZAO WATU HAWA
1:Ni watu waliokaribu nawewe lakini .mipango yao kukuumiza
2;Wapo Tayari Kubadilika Wanapoona Pesa hauna au upo na Tatizo.
3;Wanatamaa ya mali Sana.
4:Yuda alimsaliti Yesu.
Tufanye Haya kuepuka
1:Sio watu wa kuwaamini sana
2;Uombe Mungu Sana.
HITIMISHO
Maadui hawa wapo katika maisha Yetu Tuombe haya Maombi Wote
Baba Naomba Uniepushe na maadui wote mkono wako uwe ngao yangu katika jina la Yesu. AMEN
WITO
Shiriki somo hili kwa wako
Maoni
Chapisha Maoni