MAREKEBISHO YA KATIBA

IBARA YA 8; MUUNDO  WA KANISA LA HOLY SPIRIT MINISTRY TANZANIA

Katika Huduma hii ya Holy Spirit Ministry Tanzania Kutakuwa na Uongozi wa ngazi ya Juu Taifa na Uongozi wa ngazi za chini.

Itaundwa Kama ifatavyo;-

a)Uongozi wa Juu Taifa Makao Makuu zitakapokuwepo
Utaundwa na-:
I) MWENYEKITI TAIFA
II)KATIBU TAIFA
III) MHAZINI TAIFA
IV) Bondi Ya Wadhamini

b)Uongozi ngazi ya chini Ngazi ya Kata ,Wilaya ,na Mkoa
Itaundwa na ;-
I) MWENYEKITI
II) KATIBU
III) MHAZINI

IBARA YA;9; WAJIBU NA VYEO VYA UONGOZI

1:AINA YA UONGOZI

a)Bondi Ya Wadhamini
b) MWENYEKITI TAIFA
c)KATIBU TAIFA
d) MHAZINI TAIFA
e)MWENYEKITI MKOA
d) KATIBU MKOA
e) MHAZINI MKOA
f) MWENYEKITI WILAYA
g) KATIBU WILAYA
h)MHAZINI WILAYA
I)MWENYEKI KATA
j)KATIBU KATA
k) MHAZINI KATA

2:SIFA ZA KIONGOZI.

Kiongozi atapatikana kwa kuangalia Sifa zifatazo ;-
1:Awe Ameokoka Yaani Mwanafunzi wa Yesu( 1Timotheo;3;6)
2:Awe na Tabia Njema Kwenye Jamii (Yakobo;3;1-12)
3;Awe mtu mwenye kujitoa,Kujali, Kuhudumia na Kuhurumia(You;3;16)
4:Awe mtu wa Kumtengemea Mungu(Waebrania;10;38)
5;Aishi Maisha Yenye Ushuhuda Mzuri Kwa Jamii(Hesabu;14;11 Yer;17;5)
6;Awe mume wa mke mmoja au mke mmoja(1Timotheo;3;2,12)
7;Awe mtu asiye na upendeleo(Yakobo;2;1-9)
8;Awe mtu wa Kusema Kweli na Anayechukia mapato ya udhalimu(Kutoka;18;21)
9:Awe mtu Ambaye Asiyezini na Anachukia Uzinzi kwake(Waefeso:5;3 Mithali;6;32)
10;Asiwe mtu mlevi au kilevi Chochote.(Luka;21;34 Warumi;13;13)

           3;KAZI ZA VIONGOZI

            a)BODI YA WADHAMINI.
Bodi ya Wadhamini wa Kanisa itakuwa na Majukumu yafatayo:-

I)Watakuwa Ndiyo Wasimamizi Wakuu Wa Shughuli Zote za Huduma

II)Kuwa muongozaji mkuu wa mikutano na vikao vyote vya Huduma

III)Kutoa Uamuzi wa mwisho kwa Jambo lisilohitaji Kupigiwa kura

IV)Kutoa Taarifa Za Maendeleo ya Umoja Kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama Wote.

V)Itawakilisha Umoja katika Majukumu na Mikutano Mbalimbali itakayofanyika nje ya Umoja(Kitaifa na Kimataifa)

VI)Itahidhinisha Fedha Za Matumizi Mbalimbali ya Huduma Baada ya Kuruhusiwa na Kamati Tendaji

VII)Msuluhishaji ,mtatuzi,na mshauri mkuu wa njia bora za kutatua migogoro inayojitokeza ndani ya Huduma.

VIII)Itakuwa na kura ya Uamuzi,Iwapo kura za Waumini wanaoafiki na Wasioafiki zitalingana/fungana.

4;Viongozi wa Kanisa la Holy Spirit Ngazi ya Kata,Wilaya,Mkoa,na Taifa(Makao Makuu)

          b)MWENYEKITI TAIFA
Huyu ndiye Atakuwa amiri jeshi mkuu wa Huduma msemaji na msimamizi mkuu wa Huduma ya Holy Spirit Tanzania.

Wajibu wake Utakuwa Kama ifatavyo;-

1.Kustawisha Huduma ya Holy Spirit Ndani na Nje ya Tanzania.

2.Ndiye msemaji mkuu wa Huduma ya Holy Spirit Ndani na Nje ya Tanzania

3.Kusuhulisha migogoro au migongano iliyoshindikana ngazi za chini kadri ya Busara na Hekima zake.

4.Ndiye atakayeidhinisha na Kudhibitisha Majina ya Viongozi wote na Mali zinazosimamiwa na Huduma.

5;Atasimamia Misingi ya Katiba na Maadili Ya Viongozi ngazi zote.

6.Ataruhusiwa kutunga sheria na miongozo Mbalimbali kwa kushirikiana na Katibu na Mhazini na Wanachama.

7;Ataisimamia na kulinda Imani ya Kristo.

        c)KATIBU TAIFA
Huyu Ni mtendaji mkuu wa Huduma ya Holy Spirit Of Ministry Tanzania Ngazi ya Taifa.

WAJIBU WAKE UTAKUWA KAMA IFATAVYO;-

1.Kuijua na Kuielezea Katiba Ya Huduma ya Holy Spirit Tanzania na Kuitumia Kwa Busara Bila Kupoteza Lango Lake Katika Kuwasilisha kwa Wanachama.

2;Kumshauri Mwenyekiti Taifa na Kumsaindia masuala Yote ya Kiutendaji

3;Kutayarisha dondo za Mikutano.

4;Kuitisha Vikao  Kwa Kushirikiana na Mwenyekiti Taifa ngazi ya Taifa.

5;Iwapo Kuna Semina,Kongamano, Mikutano atandaa Mambo yote yatakiwayo kwa Kushirikiana na Viongozi Wezake.

6;Kuandaa mahali Pa Mikutano na Mambo muhimu yatakiwayo.

7;Kuwakaribisha Wageni Kutoka Taasisi Mbalimbali.

8;Kuandaa muhstasari wa Mikutano ngazi ya Taifa na Kuisoma Katika Kikao.

9;Kupokea na Kuhifadhi Kumbukumbuka na Nyaraka Zote za Huduma.

10.Kujibu barua Zote na Kushughulikia barua zilizofika ofisi kuu.

11;Kuandaa Taarifa Mbalimbali nakuziwakilisha kwa Mwenyekiti Taifa.

         d.MHAZINI TAIFA

Huyu atahusika kusimamia Mambo yahusuyo fedha na miradi Yote ya Huduma.

WAJIBU WAKE UTAKUWA KAMA IFATAVYO;-
1.Kutunza Mali za Holy Spirit na Kumbukumbu zake zote.

2:Kuweka Vizuri hesabu na mapato na Matumizi ya Huduma na Kudhibiti Matumizi mabaya

3.Kufatilia Utekelezaji Wa Maazimio Ya Husuyo Fedha  na Miradi Yote Ya Huduma Pamoja na Kutembelea na Kufanya ukanguzi na uhakiki wa hesabu ngazi za chini.

4;Kutoa Taarifa ya mapato na Matumizi katika Vikao vya Huduma Taifa.

5;Kuandaa Bajeti ya Huduma Taifa.

            e.MWENYEKITI MKOA
Huyu ndiye Atakuwa mtendaji mkuu na muhimili wa utendaji ngazi ya Mkoa.

WAJIBU WAKE UTAKUWA KAMA IFATAVYO;-
1.Kustawisha Huduma ya Holy Spirit Katika ngazi ya Mkoa,Wilaya,na Kata

2.Ndiye msemaji mkuu wa Huduma ngazi ya mkoa,Wilaya, na kata

3.Kusuhulisha migogoro au migongano katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata.

4;Kuwahamasisha Shughuli za Maendeleo kijamii na kisiasa ngazi ya Mkoa

5.Kutoa Taarifa Za Mara Kwa Mara za Maendeleo ya Huduma na Utekelezaji ngazi ya Taifa

6:Kuwa na ushirikiano wa Karibu/ kiungo Kati ya Viongozi ngazi ya chini.

7.Kuwasilisha Mambo yaliyo juu ya uwezo wake kwenye ngazi ya Taifa.

8.Katika utendaji wake wa kazi ataajibika kushauriana na Mwenyekiti ngazi ya Wilaya na Kata.

          f.KATIBU MKOA
Huyu Ni mtendaji mkuu wa Huduma ngazi ya Mkoa.

WAJIBU WAKE UTAKUWA KAMA IFATAVYO;-

1.Kuijua na Kuielezea Katiba Ya Huduma ya Holy Spirit Tanzania na Kuitumia Kwa Busara Bila Kupoteza Lango Lake Katika Kuwasilisha kwa Wanachama.

2;Kumshauri Mwenyekiti mkoa na Kumsaindia masuala Yote ya Kiutendaji.

3;Kutayarisha dondo za Mikutano.

4;Kuitisha Vikao  Kwa Kushirikiana na Mwenyekiti mkoa ngazi ya mkoa

5;Iwapo Kuna Semina,Kongamano, Mikutano atandaa Mambo yote yatakiwayo kwa Kushirikiana na Viongozi Wezake.

6;Kuandaa mahali Pa Mikutano na Mambo muhimu yatakiwayo.

7;Kuwakaribisha Wageni Kutoka Taasisi Mbalimbali.

8;Kuandaa muhstasari wa Mikutano ngazi ya mkoa na Kuisoma Katika Kikao.

9;Kupokea na Kuhifadhi Kumbukumbuka na Nyaraka Zote za Huduma.

10.Kujibu barua Zote na Kushughulikia barua zilizofika ofisi kuu.

11;Kuandaa Taarifa Mbalimbali nakuziwakilisha kwa Mwenyekiti mkoa

        g.MHAZINI MKOA.

Huyu Atasimamia Fedha na Miradi katika ngazi ya mkoa

WAJIBU WAKE UTAKUWA KAMA IFATAVYO;-

1.Kutunza Mali Za Holy Spirit Tanzania Ngazi ya Mkoa

2.Kuweka Vizuri Hesabu Za Mapato na Matumizi ya Huduma na Kudhibiti Matumizi mabaya.

3.Kufatilia Utekelezaji Wa Maazimio Yahusuyo Fedha na Miradi ihusuyo mkoa

4.Kutoa Taarifa Ya Mapato na Matumizi katika Vikao vya Huduma Vya mkoa

5.Kuandaa Bajeti  ya Huduma Mkoa.

  h.MWENYEKI WILAYA
Huyu ndiye Atakuwa mtendaji mkuu na muhimili wa utendaji ngazi ya Wilaya.
Majukumu na Utendaji wake wa Kazi Utafafana na Mwenyekiti  ngazi ya mkoa.

    i.KATIBU WILAYA
Huyu Ni mtendaji mkuu wa Huduma ngazi ya Wilaya
Majukumu na Utendaji wake Wa Kazi Utafafana na Katibu ngazi ya mkoa .

j.MHAZINI WILAYA
Huyu Atasimamia Fedha na Miradi katika ngazi ya Wilaya
Majukumu na Utendaji wake Wa kazi Utafafana na Mhazini ngazi ya mkoa.

k.MWENYEKITI  KATA.
Huyu ndiye Atakuwa mtendaji mkuu na muhimili wa utendaji ngazi ya Kata
Majukumu na Utendaji wake wa Kazi Utafafana na Mwenyekiti  ngazi ya mkoa na Wilaya.

l.KATIBU KATA
Huyu Ni mtendaji mkuu wa Huduma ngazi ya kata
Majukumu na Utendaji wake Wa Kazi Utafafana na Katibu ngazi ya mkoa na wilaya

m.MHAZINI KATA
Huyu Atasimamia Fedha na Miradi katika ngazi ya kata
Majukumu na Utendaji wake Wa kazi Utafafana na Mhazini ngazi ya mkoa na wilaya

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.