SOMO;KAZI ZA SHEMASI


🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

*SOMO: KAZI YA SHEMASI
KANISA LA MOTO WA YESU
Morogoro Wilaya Ya Kilosa Dumila (Mbingiri)
KWA PASTOR RICHARD

*KAZI ZA MASHEMASI*

*1) Kusimamia taratibu zote za kikanisa, kama vile.*

a) Usafi na upambaji wa kanisa

b) Kupanga ukaaji wa watu kanisani

c) Ulinzi wa kanisani wakati wa ibada

d) Kusimamia upishi na uugawaji wa vyakula

e) Kuwakarimu wageni - kuwapokea, kuwakaribisha, kupata taarifa zao na kuwapa maelekezo.

f) Kuwahudumia wagonjwa na wasiojiweza

g) Kuwasaidia wanao dondoka na wenye mapepo wakati wa maombezi

h) Kusimamia ratiba za kikanisa.

*2) Kusimamia waamini wa mtaani kwako.*

a) Kusimamia ibada za nyumba kwa nyumba

b) Kuwahudumiawashirika walio wajane, yatima, wagonjwa na wasiojiweza.

c) Kusaidia mawasiliano ya kikanisa wakati wa ibada na hata wakati mwingine.

d) Kufuatilia taarifa za washirika.

*3) Kufundisha, kuonya, na kuelekeza na kuwatia moyo washirika.*

*4) Kushirikiana na kufanya kazi kwa upendo pamoja na mchungaji na wazee wa kanisa.*

a) Kusaidiana pamoja na wazee wa kanisa katika kusimamia kazi za kanisa.

b) Kutunza pesa na mali za kanisa pamoja na kumbukumbu za kanisa.

c) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo ya kanisa la mahali;

d) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo toka ngazi za juu.

e) Kujitoa kwa hali na mali, ili kuifanya kazi ya Mungu.

*5) Kuwa mshauri wa mchungaji na wazee wa kanisa.*

*6) Kuliombea kanisa.*

*7) Kuiombea, kuihudumia, na kuitunza nyumba na familia ya mchungaji.*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.