SOMO;KAZI ZA MZEE WA KANISA
SOMO; MAJUKUMU YA MZEE WA KANISA NDANI YA KANISA.
1:Walio na uwezo
Wenye kumcha Mungu
2:Watu wa kweli / si wenye ndimi mbili
3:Wenye kuchukia mapato ya udhalimu
4;Wenye kujawa Roho wa Mungu
5;Wenye kujali na kutunza familia zao /mahusiano mema katika familia
6;Wenye kushuhudiwa mema na watu walio njeWatu wasiolaumika
7;Wenye kiasi na busara/hekima Wenye kujali/kufuata utaratibu
8;Si watu wa kujadiliana(:: si watu wa kubishana)
9;Wasiwe wepesi wa hasira
10;Wasiwe watu wa kujipendekeza nafsi zao
11;Walio kielelezo kwa maneno mema na matendo mema, usafi, imani, na upendo. {Kut.18:21; Mdo.6:3; 1Tim.3:1-13; 4:12-16; Tito 1:5-11; 2:1, 7,8}
MZEE WA KANISA (::: Mwangalizi wa Kanisa)
Ni daraja lenye madaraka makubwa.
👉👉Mzee wa Kanisa Apaswa awe
:1.Aliyejitoa kikamilifu kwa Kristo. 👉🏿“Huwezi kuwa na mvuto utakaowabadilisha wengine mpaka moyo wako mwenyewe umenyenyekezwa na kusafishwa na kulainishwa na neema ya Kristo” (Evangelism, 458).
2.Kielelezo kwa washiriki👉🏿: Wazee wa kanisa hawana budi kuwa kile wanachotaka wengine kuwa, kuamini kile wanachotarajia washiriki wao kukiamini, na kumpenda Kristo kama wanavyowataka kupenda
.Wazee wanachaguliwa na kuwekewa mikono katika kanisa si kwa ajili ya kufanya kazi ya kanisa tu, bali kudhihirisha tabia ya Kristo.
Kuwa kielelezo sahihi kwa hakika kutajumuisha yafuatayo:
a.Unga mkono mafundisho ya kanisa (Tito 2:1)
b.Dumisha mahusiano imara ya familia (1Tim.3:4, 5).
Kama mzee wa kanisa, wewe ni sehemu ya familia mbili; familia yako mwenyewe na familia ya kanisa.
c.Uwe msafi kingono (Ebr.13:4). Epuka kuvunja miiko ya ngono kwa:1)Kumpenda mwenzi wako kama nafsi yako
2)Kuelewa udhaifu wako
3)Kuwa na tahadhari unapomshauri mtu wa jinsia tofauti
4)Kuwa imara kiroho
5)Mit.6:32, 33; Thes.4:3-7 iwe kinga yako.
d.Epuka ubaguzi wa aina yo yote (Gal.3:28).
e.Uwe mrudishaji zaka na mtoaji sadaka kielelezo.
Ukiwa kielelezo katikahili, unaweza kufanya vingi kuwatia moyo washiriki wa kanisa kuwa mawakili waaminifu.33.
Kiongozi wa washiriki: Rum.12:8. “
Karama ya uongozi ni uwezo wa kutoa mwelekeo na mwongozo kwa watu wa Mungu ili watende kazi pamoja kutimiza kile Mungu wanachotaka watimize”(MwM,49).
1;Wapende washiriki wako. Kama ukiwapenda wale unaowaongoza,wengi pia watakupenda. Na kama wanakupenda watafuata uongozi wako.
2;Unganisha washiriki wako. Kuwasaidia washiriki kuvuta pamoja kwa umoja ni moja ya sehemu muhimu sana za uongozi wa mzee. Soma Zab.133:1.
3Shauriana na washiriki wako. Lisaidie kanisa lako kupanga malengo yake lenyewe. Panga na wale unaowaongoza na si kwa ajili yao tu.4.Mwezeshaji wa washiriki: Kama mzee, unapaswa uwe mratibu na mwezeshaji ukitumia mvuto wako kumsaidia kila mshiriki wa kanisa lako kukuza uwezo kamili wa karama zao binafsi za kiroho kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.
>wasaidie washiriki kuzijua karama zao za kiroho, kisha wape mafunzo.
Baadhi ya Majukumu ya Mzee wa Kanisa:
1.Kulilisha kanisa kupitia mafundisho na mahubiri kanisani na nyumbani mwa washiriki (Mdo.20:28; 1Pet.5:2; Yn.21:15-17).
2.Kulilinda kanisa kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kanisani.
3.Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote, kupitia idara zote na vyama vyote kanisani.
4.Kuhimiza uwakili katika nyanja zote::: mwili, wakati,talanta, mali, mvuto
,5.Kusimamia ibada za kanisa. kuhakikisha kuwa ibada za kanisa (Jumatano, Ijumaa, Sabato); zinaendesha inavyostahili, na wahudumu wanaostahili.
6.Kuwaandaa wanaotajiwa kubatizwa. Wale wanaohitaji kujiunga na kanisa wanapaswa kujua kanuni zinazoongoza kanisa hilo; wanapaswa kujua maana ya kutoa maisha yao kwa Kristo.
7.Kuwashikiria washiriki wapya. Yapo mambo manne uwezayo kufanya:a.Wafanye rafiki. Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa wapya. (wajibu wa walezi-MwM, 143)
Maoni
Chapisha Maoni