SOMO; KUOKOKA NA MWILI

SOMO: KUOKOKA MWILI NA ROHO 

Karibu Tujifunze Pamoja  Somo hili Watu wengi wamekuwa wakiokoka rohoni Miili yao inakuwa bado ni Dhaifu inayoishi kwenye dhambi na Kutenda Dhambi Kwa Kuwa Mwili siku zote ni Adui namba moja Anayemfanya mwanadamu Akosane na Mungu wake.

Wapo watu rohoni wapo vizuri wanaomba na mpaka wanawafungua watu wegine lakini miili yao bado inawatumikisha kuwa watumwa wa dhambi na hawana ujasiri wa kusimama kujizuia kutenda dhambi. Hebu fatana na ujumbe huu utakuponya


 Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro veta Dakawa


MAMBO HAYA HUTOKEA MTU ANAPOOKOKA MWILI (FAIDA ZA KUOKOKA MWILI)

1: MAGONJWA HAYATAKUTE$A KWA KUWA MWILI UMEOKOKA


Mithali 3:8
[8]Itakuwa afya mwilini pako,
Na mafuta mifupani mwako

Utaufanya Mwili Wako Uzidi Kupendeza nakunawili kwakuwa umeuepusha. Na Dhambi


2;MWILI WAKO UTAUFANYA USITENDE MABAYA NA HUTAKUWA NA MAJONZI AU KUFANYA YACHUKIZAYO.


Mhubiri 11:10
[10]Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.

Kwakuwa Mwili Umeokoka Hautafanya Tena yachukizayo kwakuwa kila ukitaka KUTENDA mwili unaogopa Dhambi na utakufanya Uishi kwa ushindi lakini mwili ukiwa hujaokoka utafata njia mbaya.


3;MOYO WAKO UTAKUONGOZA KUWAZA NA KUAMUA YALIYO MANZURI TU


Mithali 14:30
[30]Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili;
Bali husuda ni ubovu wa mifupa.

Moyo utaufanya uwe unakuogoza katika hofu ya Mungu katika njia ya Bwana
Hutamkuta mtu ALIYEOKOKA mwili anakata Tamaa au Anatenda DHAMBI



4; MUNGU ATATENDA MIUJIZA MIKUBWA ILIYO$HIDIKANA KWA AKILI YAKO



Yeremia 32:27
[27]Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?

Hii itamfanya Mungu ajishughulishe na Maisha Yako Lakini Mwili wako Usipookoka Bado utateseka.


5;HAUTAZIDIWA NA CHOCHOTE KWA KUWA BWANA ATAWASHA MOTO WAKUMTUMIKIA KWA NGUVU ZOTE.



Ezekieli 20:48
[48]Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, BWANA, nimeuwasha; hautazimika.

Watakujua vizuri watu kuwa wewe unatembea na Mungu kwa kumanisha katika Kiwango Kikubwa.
Utamfanya Mungu ajidhihirishe kwa kukutumia

6; MUNGU ATAKUPA KILA KITU KIPYA UTAKUWA WATOFAUTI NA WEGINE



Ezekieli 36:26
[26]Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Kwakuwa Mwili Umeokoka utapewa Kila kitu kitende Kama kimeokoka mwili usiokoka hufanya Dhambi.


7;ROHO WA MUNGU HUKAA NA WATU WALIOKOKA MWILI



Yoeli 2:28
[28]Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

Ndipo Utaona Mungu anaachilia maono macho yakuona kwakuwa Mwili Umeokoka


8;HUTAOGOPA KIFO AU MTU YEYOTE ANAEKUTISHA.


Mathayo 10:28
[28]Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Mwili ukiokoka hutaongopa kifo au Chochote kinachoua mwili.


9;MWILI WAKO ULIOKOKA TOKA ZAMANI PAMOJA NA YESU
KUPITIA MATESO YAKE UNAPOUTENDESHA DHAMBI UNARUDIA KULEKULE.



Warumi 6:6
[6]mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️
Warumi 7:16-19
[16]Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
[17]Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
[18]Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
[19]Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.


10;ONGEZA POINT YAKO


HITIMISHO
Je wewe Umeokoka mwili au bado unatabia zilezile za kale hujabadilika  mwili ni wako lakini unakutumikisha uishi maisha ya dhambi ni heri ng oa macho kuliko mwili ukupeleke Jehanamu unajiona.


Unasubiri Nini kuokoka na mwili wako


WITO


Fika Kanisani Morogoro Veta Dakawa
Uponywe matatizo yako
Tuma ujumbe Whatsap upewe maelekezo ya Kufika+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.