SOMO: CHANZO CHA IMANI KUULETA MATOKEO

SOMO: CHANZO CHA IMANI KULETA MAJIBU.
Kitabu  Warumi;10 9-25

IMANI; Ni uhakika Wa Unachokiongea Kitakuwa Kama ulivyosema.

IMANI huwa ili ikupe matokeo au ifanye kitu lazima usikie
Mfano; Huna Tatizo unaenda Kupima KWA Daktari Anakuambia wewe hutazaa Kizazi chako kina shinda kwa Kuwa Umesikia Neno Kizazi Kinashinda Kweli Utakuwa na Shinda. ILi Upone Unatakiwa usikie Kizazi chako hakina shida

MAMBO YANAYOIFANYA IMANI YAKO ILETE MATOKEO.

1:KUSIKIA NA KUELEWA NENO
Tusome;Yohana 5:24
[24]Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ
Warumi 10:17
[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Kuna maneno mengi utakayoyasikia Kuna
a)Maneno Ya Mungu
b)Maneno Ya Watu
c)Maneno Ya Moyo katika Kuwaza au Kufikiri

Katika Maneno Haya Lolote litakalokuwa Nzuri litafanyika na utaliishi

Mfano; Ukawa unawaza Mimi siwezi hiki kwa kuwa moyo wako umeuruhusu ufikirie hivyo Imani itadhibitisha.hutoweza Kweli.

Mfano; Mimi Sitoolewa au Kuoa Kweli utakaa muda huolewi kumbe Ni Kwasababu ya maneno yaliyojaza moyo wako.

2: KUOMBEWA NA KUFUNGULIWA
Kuombewa na Kufunguliwa Ni kitendo Cha wewe kwenda kwa Mtumishi na Kuombewa Kisha Kufunguliwa Ni kuona Hali ya Utofauti
Hapa Utafanya Mambo mawili
a)Kwenda Kuombewa
b) Kuomba Mwenyewe

Luka 17:12-19
[12]Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
[13]wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
[14]Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
[15]Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
[16]akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
[17]Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
[18]Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
[19]Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ
1 Wathesalonike 3:10
[10]usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu?

3; NGUVU YA MAAMUZI KUAMUA MWENYEWE.

UNAPOFANYA MAAMUZI :-Unaichochea Imani Yako Ilete Matokeo Ukiwa Mtu mgumu wa Kufanya MAAMUZI Imani Yako Utaifanya Isikupe matokeoa Nguvu ya Maamuzi huhusisha
a)Fanyia Maamuzi Kila Unachosikia
UFANYE au Usiifanye
b)Fanyia Maamuzi Kila Unachokiona
Kipo Sawa au Sio Sawa rekebisha
Mfano huu chini.πŸ₯¦
πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ
Luka 8:43-47
[43]Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
[44]alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
[45]Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.
[46]Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.
[47]Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.

4:JITOE NA KUTOA SADAKA KWA IMANI.
Chukua Elimu Ya Utoaji Ikae moyoni Mwako Kwakuwa
Huifanya Imani Yako Ikupe Matokeo ya Ulichokiomba

JITOE KWA...
a)Mwili wako kumtumikia Bwana
b)Mali zako Viwanja majumba Magari nk.
c)Jitoe Elimu Yako Kuitumia Kwa Faida Ya Bwana.
πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘†πŸ‘†
Waebrania 11:4-7
[4]Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
[5]Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
[7]Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

5:UPENDO KWA WENGINE
Upendo huwa unamfanya mtu ajisikie Yupo wa Thamani na Imani Yake ikue Kutokana Anapendwa

Fanya Mambo haya
1;MPE MATUMAINI
2:MPE IMANI ATAVUKA USIMVUNJE MOYO.
3;MPE UPENDO

1 Wakorintho 13:13
[13]Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

6:JIEPUSHE NA DHAMBI NA DHAMBI YA UZINIFU.
Wagalatia 3:22
[22]Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

Dhambi Ya Uzinifu huua Imani Yako kwa haraka na kuishusha chini Nakuwa mtumwa wa Dhambi ya Uzinifu.
JIEPUSHE ili Imani Yako inakupa matokeo ya unachoomba.

7;JARIBU AU CHANGAMOTO HUIFANYA IMANI YAKO IKUE.

Majaribu hukupa nafasi Ya wewe kumtafuta Mungu Tena Kwa Juhudi Nyigi nakuikuza Imani Yako Kupitia Kipindi Unachopitia huwa Darasa kuikomaza Imani Yako

1 Petro 1:7
[7]ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.

8;IMANI HUPEWA NGUVU NA MATENDO.

Hakikisha Unafatilia Na Kutembea Katika Mafundisho Ya Neno la Mungu au Kuenenda Sawasawa na Mtu aliye na Mamlaka
Hakikisha Unakuwa na haya
a)Baba Wa Kiroho
b) Madhabahu Yako
c)Sadaka Yako
Fanyia MATENDO unachofundishwa Sio uwe msikiaji TU huna kitendo Chochote huwezi kuifanya Imani Yako Ikupe majibu.

9; UTAISHI NA KUYAENDESHA MAMBO KWA IMANI.

Waebrania 10:38
[38]Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Mtu mwenye Imani huishi nakuyaongoza maisha Yake Kupitia imani na Mungu humfurahia mtu mwenye imani.

10;TAJA YAKO

HITIMISHO
Imani ndio kila kitu huwezi fanya kitu bila imani  Kupitia Imani ndio Huleta majawabu ya maswali yako.

Haya Tulioyataja Ni Mambo yanayomfanya Mtu ajibiwe Maombi yake.

WITO
Fika Kanisani Morogoro Veta Dakawa Mfate WhatsApp Pastor Richard Akupe maelekezo ya Kufika +255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.