SOMO;Kijana na Ujana

SOMO:KIjana na Ujana

KIJANA NI Nani?


Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo:


Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa.


Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.


Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi.


Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimakuzi. Kuna tofauti kati yao na miongoni yake ni hizi:-


MTOTO

KIJANA

Umri miaka 0-10 hapa wengi wao ni watoto wasiopevuka,

11-17 ni walio katika upevukaji (balehe).

18-35 ni umri wa vijana ambao wamepevuka na wanakuwa na tofauti kubwa katika maumbile yao.

Kisheria miaka 0-17 ni mtoto.

Kisheria miaka 18-35 ni kijana.

Akili yao haijapevuka na huwa na utoto mwingi.

Akili imepevuka na anaweza kuwa na mambo ya kiutu uzima.

Hana haki ya kufanya maamuzi yake bila kushirikisha wazazi au walezi.

Anahaki ya kufanya maamuzi yake bila wazazi au walezikushiriki.

Hawezi kushiriki masuala mbalimbali kama vile siasa, ajira na yasiyohusika kisheria.

Anauhuru wa kushiriki masuala mbalimbali kama vile siasa, ajira na masuala yote yanayohusu jamii kwa ujumla.

MAMBO MUHIMU YA KUANGALIA UNAPOELEZEA MAANA YA KIJANA.


Utambuzi:
Kijana ni lazima awe na utambuzi binafsi, utambuzi wa jamii yake na mazingira


yanayomzunguka. Kujitambua kunamfanya kijana kufanya mambo sahihi na kuenenda sawa na


maadili ya jamii na Taifa kwa ujumla. Hapa kijana anakuwa na uelewa wa kipi nifanye na


kipi nisifanye.


Ukomavu wa akili: 
Katika umri wa miaka 18 vijana wengi wanakuwa na akili ya kufanya


Mambo ambayo yanaendana na umri huo,kijana pia ataweza kuwa mshauri kwa wenzake,familia


na jamii aliyomo. Hapa ndipo kijana anapanga malengo yake na kuanza ufuatiliaji ili


yatimie,kamavile kubuni wazo fulani lenye manufaa kwake au jamii, biashara au  kufikiria kazi


nzuri anayoweza kufanya.

Uelewa wa changamoto:
 kijana ni lazima aelewe changamoto mbalimbali na kujua jinsi ya


kukabiliana nazo. Changamoto hizo ni kama tatizo la ajira kwa vijana mtu utawaza kujiajiri au


kutafuta kazi halali itakayokuingizia kipato.


Kujenga hoja
: umri mzuri wa kuwa na hoja zenye nguvu katika masuala mbalimbali.


Unapokuwa kijana ni lazima uwe mwepesi katika kushiriki masuala mbalimbali na kujenga hoja


ambazo zinanguvu na kufanya usikilizwe na jamii hata Taifa.


Ushawishi
Kijana ni lazima uwe na ushawishi kuhusu jambo fulani,katika kushawishi ndipo


tunaona nguvu ya kijana na kuanza kutengeneza Taifa imara. Vijana wengi wa sasa tunajitahidi


sana kuwa na nguvu ya ushawishi katika masuala tofautitofauti. Pia tunaona asasi nyingi


zikiongozwa na vijana wenyewe ili kuweza kushawishiana mambo yenye tija kwa maisha ya


kijana. Hivisasa vijana kushawishi wenzao kushiriki uongozi, kupiga kura, kushiriki huduma za


kijamii na kitaifa.

KIJANA ANAPASWA AFAHAMU MAMBO HAYA KUMHUSU


AJITAMBUE
Kijana ni lazima ajitambue na kutambua fursa mbalimbali zinazowahusu vijana.


Siku hizi kuna masuala mengi ambayo vijana wanashiriki hivyo kijana anaweza kushiriki


uongozi, ajira, ujasiriamali na mengine mengi. Unapojitambua ni lazima ujue thamani yako na


kusudi la uwepo wako ili uweze kufanya mambo mazuri sana kwa jamii na taifa kwa ujumla.

AJIKUBALI:
    kujikubali ni hali ya kuyapokea mambo yote yanayokuhusu, kijana anapaswa


kujikubali vile alivyo hii itasaidia kusonga mbele zaidi.Hapa mfano mtu unatatizo fulani ambalo


linakufanya  tofauti na wengine unapaswa kujikubali ili ujione kuwa ni wa thamani kama


walivyo wengine. Unapojikubali unaweza kujiona kawaida na kufanya mambo makubwa kwa


familia,jamii na Taifa na kufanya utambulike na uweze kuwa mfano wa kuigwa.

AWE NA SHAUKU , NIA AU KIU:

   kijana ni lazima uwe na shauku nia au kiu ya kufanya vitu


vya tofauti vyenye lengo la kuelimisha kuonya au kuasa jamii na pia kuishi maisha ya kusaidia


wenginekatika kujenga au kutikmiza kusudi, maono au matarajio yao.

AWE MZALENDO:
 Kijana anapaswa kuwa mzalendo sana. Hapa kama kijana inabidi ujiulize


na ujue kusudi la kuzaliwa na kukwepo Tanzania. Ni lazima ujue kuwa unapaswa kufanya


uzalendo kwa nchi yako,ufanye yaliyo mazuri kwa jamii ya Kitanzania. Hivyobasi, kijana na


vijana tunapaswa kuelewa na kutambua nafasi yetu binafsi kwa familia zetu, jamii, wilaya, mkoa


na Taifa kwa ujumla ili tuweze kufanya mambo ya busara katika kuchochea maendeleo ya nchi


yetu.

UJANA NI NINI?


·         Ujana ni hatua ambayo mtu anapitia baada ya utoto.


·         Ujana ni hali ya kuwa na tabia za umri wa ujana ambao ni miaka 18-35.


·         Ujana ni kipindi cha makuzi ya mtu kabla ya utu uzima na hatimaye uzee.


·         Ujana ni kipindi kati ya miaka 18-35 hivi ambapo mtu anakuwa amepevuka na ukomavu wa kiakili na kimwili.

Hali ya ujana huanza baada ya maumbile ya mtu kubadilika na kuanza kuwa na hisia za kimwili na kutamani kuwa na uhuru wake katika maamuzi.  Hiki ni kipindi chenye changamoto nyingi sana kwa kijana, sababu anakuwa amekumbana na hali mpya ya mabadiliko ya mwili na anajiona yupo tofauti na aliyokuwa mwanzo.


Katika ujana kuna vichocheo, hisia na mabadilio mbalimbali ya kimwili na tabia kwa ujumla.


Mabadiliko ya kimwili ni yale yanayoambatana na ukuaji wa mtu toka utoto kuelekea ujanani.


Mabadiliko hayo huambatana na vichocheo vya mwili pamoja na hisia kali sana za kimaumbile,katika kipindi cha ujana ndipo hutokea mihemko na matamanio mengi hasa ya kukaa au kuwa na urafiki na mtu wa jinsia nyingine. 


Mahusiano baina ya kijana wa kike na wa kiume ndipo huanza, utovu wa nidhamu,ujeuri,kiburi,na kujisikia au kujiona bora kwa kijana.


                    MAISHA YA UJANA YANAAMBATANA NA TABIA HIZI;


·         Kuwa mbichi,mwenye nguvu, na kuchangamka.


·         Kutokuwa na  ukomavu wa kutosha sababu bado upo kwenye ukuaji.


·         Kuwa na nguvu nyingi kimwili na kiakili.


·         Kuwa na majukumu machache na uhuru mwingi.


·         Kuwa na muda wa kutosha kufanya mambo mengi.


·         Kuwa na shauku ya kufanya mambo mazuri katika maisha yako.


·         Kuwa na muda wa kushirikiana na vijana wengine katika masuala ya maendeleo.


             MAMBO YA KUFANYA KATIKA MAISHA YA UJANA


·         Nidhamu: Ujana ni lazima uambatane na nidhamu ya hali ya juu ili uweze kuvuka vikwazo mbalimbali.


·         Heshima: Heshima utakayoionesha wakati wa ujana ndiyo itakayokusaidia uzeeni,utaheshimika kama ulivyoheshimu wengine.


·         Uwajibikaji: Jifunze kuwajibika katika majukumu mbalimblai ili ufanikiwe.


·         Msingi wa maisha yako: Ni lazima kufahamu namna ya kujiandalia maisha ya baadaye.


·         Chagua marafiki wema na sahihi: Jua kuchagua marafiki wanaofaa katika shida na raha


·         Uhusiano: Tengeneza uhusiano wenye matokeo chanya,fahamu uhusiano wenye mafanikio na kuchagua watu wema kwenye mahusiano.

                    MATOKEO YA KUUTUMIA UJANA VIBAYA


Majuto na malalamiko
Ukitumia vibaya ujana wako ni lazima ujute na kulalamika uzeeni.


Kulaani watu au kulaaniwa:
 Kuwalaani watu ambao unahisi walifanya ushindwe  au watu kukulaani kutokana na mwenendo wako.


Kushindwa au kutofaulu katika maisha:
 Usipojifunza na kuwajibika basi kuna hatari ya kushindwa au kutofaulu malengo ya maisha yako.


Kuchanganyikiwa:
 Ukiutumia vibaya ujana kwa mambo yasiyofaa kama vile bangi, madawa ya kulevya, sigara na pombe yanaweza kukufanya uchanganyikiwe.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.