SOMO: MOYO WA IBADA

            SOMO; MOYO WA IBADA
Tufungue Biblia
ISAYA:1:13👉🏿AYUBU:15;4👉🏿Sefania;3;18
Matendo;13:2👉🏿Warumi:12:2👉🏿Waebrania;12:28
Mwalimu Pastor Richard
NIPO Morogoro veta Dakawa
WhatsApp+255759861768
🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦
Ushuhuda wa mtoto Aliyekuwa Amechukuliwa Msukule.

Mtoto mmoja Aliyeitwa Saidi aliletwa Jumanne Usiku Akiwa hajiwezi na wazazi wake hapa Kanisa katika Ibada ya Maombi ya mkesha wakanikuta wazazi wakilia kwa kumpoteza mtoto wao nikawaambia muwekeni hapo chini Baada ya Kumuweka chini Niliaza kusifu nakumchezea Bwana mpaka mtoto Akafunguliwa Wazazi na waliongozana nao Waliokuwa waislamu Baada ya kuona hayo kwa macho Yao walisema Huyu Yesu wako Tunataka nasisi Nikawaongoza ukiri wakaokoka Watu Sita Huu Ni Ushuhuda wa Mtu mwenye Moyo wa ibada.

Moyo wa ibada👉🏿Ni moyo uliojitoa katika masuala ya ibada

MAANA YA MOYO WA IBADA 👉🏿Unyenyekevu wenye nguvu ndani Yake.

KUNA TABIA TATU ZA MOYO WA IBADA NDANI YA MTU
1:Tabia Ya Moyo Uliojitoa kwa ibada
2:Tabia ya Moyo Uliojeruhiwa kwa Ibada
3:Tabia ya Moyo Uliofikia Mwisho kwa ibada.

TABIA YA MOYO ULIOJITOA KWA IBADA
Hawa Ni Watu waliosimama na kujitoa kwa kumanisha masuala ya ibada

Sifa Zao
1:Watu Wenye nguvu ya ibada
2:Watu Wasiokata Tamaa
3:Watu walioamua Kutembea na Mungu
4;Watu wasioenda kanisani kwa Sababu ya Mtu
5;Watu Wenye Imani na Yesu sio Dini au dhehebu.

TABIA YA MOYO ULIOJERUHIWA KWA IBADA
Hawa Ni Watu Walioacha ibada kwa Kukata Tamaa na Mambo ya ibada wanaamua kukaa nyumbani bila Kwenda Kanisani

SIFA ZAO
1:Watu waliorudi nyuma Kiroho
2:Watu wasioenda Kanisani lakini wanamjua Mungu
3:Watu Waliochukia ibada
4:Watu waliokosa imani na Wachungaji wao
5:Watu Wasiofanya maamuzi ya kurudi kanisani.

TABIA YA MOYO ULIOFIKIA MWISHO.
Hawa Ni Watu wasiomjua Kabisa Mungu hata ibada

SIFA ZAO
1:Watu Wasio  Kwenda Kanisani
2;Watu Wasiotenda maovu au Wanatenda maovu lakini wanakuwa hawafanyi ibada
3;Watu Waliojikatia Tamaa nakusali
4;Watu Wasiohubiriwa Wabishi

MOYO WA IBADA FAIDA ZAKE
1:Utakufanya uwe na mahusiano mazuri Kati yako na Mungu
2:Utakufanya uutawale ulimwengu wa roho na shida zake
3;Utakufanya ukubalike na uaminike na watu
4;Utapokea uzima wa milele ukifa
5:Utakukuza imani yako

KINYUME Cha haya Ni HASARA zakukosa moyo wa ibada

HITIMISHO
Tunapaswa tuwe na ibada na Mungu yenyekujitoa

WITO
Wewe Upo Tabia ipi Mpigie Jioni Saa 12 00 Pastor Richard+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.