SOMO: YAFANYE HAYA KWENYE MAHUSIANO NAYATADUMU

SOMO; YAFANYE MAHUSIANO YAKO YADUMU KWA KUFANYA HAYA KABLA HAMJAOANA.

Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa

Kuna Watu Wengi Wameshindwa KUIMARISHA mahusiano Yao Nakuyafanya Yasifikie kwenye ndoa Kwa Sababu Yakukosa Ufahamu wakujua haya mapema

Mithali 8:10

[10]Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, 

Na maarifa kuliko dhahabu safi.

✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️

Yeremia 7:28

[28]Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya BWANA, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali na vinywa vyao.

✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏπŸŒ΄πŸŒ΄πŸŒ΄πŸŒ΄πŸŒ΄

Mwanzo  wa Mahusiano

Msidanganyane(a)Mwambie mwenzi wako ukweli.

(b)Mwambie yale unayopenda na usiyopenda.

(c)Kuwa muwazi kwa mwenzi wako.

(d)Onyesha upo tayari kuachana na mambo yote uliyokuwa umeyazoea ambayo kwa sasa yanaweza bomoa uhusiano wenu.

Mfanye Mwenzako Ajisikie ni wa Muhimu

(a)Tenga muda maalumu wa kuwa naye.

(b)Onyesha unafurahia uwepo wake.

(c)Mnapozungumza jambo onyesha umakini kwa kumsikiliza na kuacha kila kitu.

(d)Usijifanye unajua kila kitu na kwamba yeye hajui.

(e)Hata anapokosea mwonye tu na kumuelekeza kwa upendo.

Usifanye Mambo Kwa Mazoea

(a)Kila siku ona ni fursa mpya ya kufanya jambo kwa ajili ya koboresha uhusiano wenu.

(b)Mfanyie jambo jipya ambalo hategemei kwamba utamfanyia.

(c)Usifanye jambo litakalomfanya ajione hana thamani tena kwako.

Usipende Kushikilia Mambo Kwa Mda Mrefu Bila Kusamehe

Anapokosea mweleze kwa upendo na umwambie umemsamehe.

Usiwe mtu wa kurudiarudia mambo kila anapokosea unakusanya makosa anapokosea tena unamkumbusha.

Kumbuka Aliwaacha Wengi Akaamua Kuwa na Wewe

Sasa usijifanye wewe ni mjanja kuliko wote.

Mwonyeshe yeye ni wa kipekee.

Usipende kila wakati kuelezea mambo ya mpenzi wako wa zamani.

Onyesha Hisia Za Kweli Kwake

Kumkumbatia mnapokuwa faragha.

Kumbusu na kumwambia maneno matamu,wengine husema maneno yanayovunja mifupa.

Mfano:Nakupenda wewe tu mpenzi wangu,hakika siwezi kukuacha mpenzi wangu, Unaniweza wewe tu mahabuba.

Mtosheleze

Husika na mahitaji yake ya kimwili na kihisia.

Hakikisha anajisikia vizuri anapokuwa kwa kumtimizia mahitaji yake ambayo una uwezo nayo yale usiyoweza shaurianeni.

Jambo analolipenda lipe kipaumbele.

Tendo la ndoa au mapenzi yafanyike kwa usahihi na kwa kutoshelezana.

“Watu wengi  wakishazoeana tu wakazaa watoto basi wanaona  tendo la ndoa siyo jambo la muhimu ni swala la dharura,na ndio utapata malalamiko mengi kwa wanandoa ama wapenzi wakisema zamani tulikuwa vizuri ila sasa amebadilika


Naitwa Pastor Richard

WhatsApp Number+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.