SOMO: USHUHUDA

SOMO: USHUHUDA WA MUNGU

Zaburi 19:7
[7]Sheria ya BWANA ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa BWANA ni amini,
Humtia mjinga hekima.
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️
Marko 14:55
[55]Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione.
✔️✔️✔️✔️🙏🙏🙏🙏🙏✔️✔️✔️
1 Wakorintho 1:6
[6]kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu;

Karibu Katika Nakala Hii Jumapili ya Tar;30/5/2021
Lengo Ujifunze Ushuhuda Ndani Yako Na Umhimu wa Wewe KUSHUHUDIA ulazima Wakumshuhudia Bwana Kwenye Maisha Yako.
Naitwa Pastor Richard
Kutoka Morogoro Veta Dakawa
Madhabahu Ya Moto wa Yesu

MAANA YA USHUHUDA;Matendo Makuu Au Ni Jambo Ambalo Mungu Amekufanyia kwenye Maisha Yako

USHUHUDA WA MUNGU NINI? Ni mabadiliko Unayoyapata nakupokea Baada yakuomba au Kuombewa Ambayo Hufanya Ujione umekuwa Tofauti na Hali ya Mara ya Kwanza ulivyokuwa Kabla hujaomba au Kuombewa.

Pia Tunaweza kusema Ni mabadiliko yakiroho yanayoonekana Kimwili.

USHUHUDA NI BARAU NZURI ILIYOANDIKWA NDANI YA MAISHA YAKO KWA KARAMU YA IMANI NA DAFTARI LA MAFUNDISHO Ya Neno la Mungu

USHUHUDA HUUNDWA NA VITU VINNE(4)

IMANI YENYE NGUVU 👉🏿Hii Ni Imani Ni uwezo wa mtu uliomo ndani Yake wakuona Ngumu Ni Jepesi Kwake.

MADHABAHU 👉🏿Hii Huwa Ni mahusiano Yako na Mungu

SADAKA 👉🏿Hii Ni Chochote Kile Cha thamani chenye kufaa Kwa Mungu inaweza kuwa Pesa Kiwanja Gari Nyumba Nguo Kutumika Kujenga hekalu la Mungu.

BABA WA KIROHO 👉🏿Huyu Husimamia Kukufanya ufikie Ushuhuda Wako kwa Kukuelekeza na Kukuonya unapoenda Tofauti.

MAJARIBU AU PITO👉🏿Jaribu ndilo litakufanya umtafute Mungu.

UMHIMU WA KUSHUHUDIA KILA MABADILIKO UNAYAONA.
1:Utejenga Ushuhuda mkubwa Upokee
2:Utamfanya Mungu Atende Zaidi ya Alivyotenda
3:Utawavuna na Kuwakomboa Watu walioelemewa na Mapito
4:Utazaa matunda yanayodumu kwenye wokovu
5: Ushuhuda Wako utawaponya wengine.

KINYUME NI HASARA ZINAZOMPATA ASIYESHUHUDIA.

USHUHUDA GANI USHUHUDIE.
Ushuhuda unaopaswa USHUHUDIE Ni ule Ambao Mungu Amekufanyia Yaani mabadiliko uliyaona toka umjue Mungu au Uaze kusali au Uaze Kufundishwa Mafundisho ya Neno la Mungu.

Hutakiwa USHUHUDIE Jambo au mabadiliko Ambayo hujayaona ndani yako.

FAIDA ZA KUSHUHUDIA
1:Utamuaibisha Shetani na Pito
2:Shetani atakuogopa na ulimwengu wa roho utakuongopa
3:Utabadilisha Maisha ya Wengi nakuokoa wengi.
4: Utafunguliwa Shuhuda zinamiminika Kama Mvua.
5;Mungu atatenda Zaidi na Zaidi.

HASARA Ni KINYUME Cha Hizi.

SEHEMU GANI UNAPASWA USHUHUDIE.
1;SHUHUDIA Watu wa Nyumbani Kwako na Kazini Kwako waliokuzunguka waeleze Mungu Alivyotenda
2: SHUHUDIA Kanisani Shuhudia kwenye mtandao Shuhudia Sehemu mbalimbali.

HITIMISHO YA SOMO LETU.
JIFUNZE KUSHUHUDIA Chochote Kile unachokiona Mungu anakibadilisha ndani Yako Ili ufungulie majibu megine.

WITO
Toa Ushuhuda Kupitia WhatsApp Number Pastor Richard+255759861768 ILI USHUHUDA WAKO USOMWE NA DUNIA
Tuma na Picha Yako Na Ukiwa nayo na picha inayonyesha Kabla Mungu hajakubadilisha Tuma .

AGALIZO; Usitume Ushuhuda usio na Picha Ya Udhihirisho.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO