SOMO WANANDOA MPATANE

              DARASA LA WANANDOA

SOMO👉🏿 WANANDOA MNATAKIWA KUPATANA.
Mathayo:20:13 Marko:14;56 Mithali:9;9

KUPATANA Ni Kuelewana kwa Wanandoa Ili muweze kuishi vizuri ndani ya ndoa huwa MNATAKIWA mpatane Kwa haya Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa Somo Hili linahusu miaka 18-60

1:KUPATANA KWA MIPANGO YENU
Mipango Ni mikakati yenye Kuleta Maendeleo na kuifanya ndoa Yenu Iwe na Msingi mzuri wa Maendeleo nakuinuka Kiuchumi.

2: KUPATANA KWA MATUMIZI YA PESA
Wanandoa MNATAKIWA mpatane katika matumizi ya Pesa nakudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kuweka bajeti Yenu  Na Kupangilia Nini mfanye Nini msifanye kwa muda huo.

3: KUPATANA KWA UZAZI.
Mnatakiwa Wanandoa mzae Watoto mtakaoweza Kuwalea nakuwatuza Vizuri msizae tu Watoto bila mpagilio au kuangalia Uwezo wa kuwasomesha na kuwatunza

4:KUPATANA KWA IMANI.
Wanandoa MNATAKIWA mpatane maswala ya imani kila mmoja awe huru kuweka wazi kadiri Imani Yake anavyoamini na atasali wapi mtasali pamoja iwe hivyo msipishane Kwenye Imani.

5; KUPATANA KWA KAZI
Mnatakiwa Kama mtaoana wafanya Kazi mpatane na muelewane ili Baadae isije Kuleta shida Kwa mmoja wenu.

Nawatakia Ujezi Mwema na Tafakari njema ya Ndoa waweza kutufatilia 👉🏿👉🏿www.mchungajirichardi.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.