DARASA LA VIJANA NA WATOTO

DARASA LA VIJANA NA WATOTO

SOMO: KIJANA THAMANI YAKE AKIOKOKA NDANI YA KANISA HATA KATIKA JAMII.

Karibu Tunaongelea Leo Thamani Ya Kijana mkristo Nafasi Yake kibiblia na mbele za Mungu. Kijana huandamwa na Tamaa mbalimbali na Changamoto za utafutaji Zinazomfanya Aishi mbali na Mungu Kutokana na Kuwa na muda mchache wa Kupumzika Mungu anatambua Kijana husumbuliwa na Tamaa za Pesa Mali Ujana Ukisoma 2Timotheo:2:22

Karibu Katika Darasa Hili Naitwa Bishop Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa


MAMBO SABA YA MSINGI YA KUKUSAIDIA KUTAMBUA THAMANI NA NAFASI YAKO KAMA KIJANA MKRISTO

1.  Ni vizuri ufahamu kwamba KABLA HAUJAZALIWA Mungu alishakujua na aliweka tayari KUSUDI,  NYAKATI, na UWEZO ndani yako maalum kwa ajili ya KANISA.{Yeremia 1:5; Zaburi 139:13,15,16;}

Kijana unatakiwa ujue Kusundi ambalo Mungu amekuitia Kama Ni kuimba imba Kama Ni uchungaji uinjilist Tumika Kwa Kujitoa Kweli Kweli Usiishi maisha ya Kikristo bila kujua Kusundi lako

2. Tambua kuwa hakuna Rika lililopewa upendeleo na nafasi ya pekee kama UJANA katika Ufalme wa Mungu.{Mithali 20:29; 1Yohana 2:14; Maombolezo 3:27}

Kijana Ni wazi Utambue Mungu amekupendelea Kuwekeza ndani Yako ukakamavu Ushawishi Kujitambua na Kujenga hoja zenye mashiko kwa Jamii na Kwa Kanisa Simama uelewe ujana wako Ni wa thamani

3. Licha ya uzuri mwingi ulioko kwenye UJANA, UJANA ni kipindi cha MPITO i.e. UMEPIMWA KWENYE MUDA na kwa hiyo basi UJANA HUPITA UPESI.{Mhubiri 12:1; Yohana 21:18;Matendo 17:26;Mhubiri 3:1,11}

KIJANA Utambue Rika la ujana utapita Sasa unaandaaje maisha Yako kiroho na Kimwili ukipita muda uliokuwa na nguvu ya Kumtumikia Mungu nakufanya kazi Yake wewe nakuacha ujihoji nguvu zako za ujana wako zinatumika kwa Mungu au dunia

4. Kijana ni KIUNGO MUHIMU SANA katika mwili wa Kristo yaani KANISA hivyo ni vema utambue thamani na nafasi yako katika kujenga na kuimarisha KANISA i.e. Mwili wa Kristo.{Waefeso 5:23; 1Korintho 12:27;Waefeso 4:12,16}

Kijana utawaleta na kuwavuna wengi utakapotambua nakuelewa Kuwa wewe Ni kiungo Kikubwa katika Kazi ya Bwana Nafasi Yako Ni ya mhimu ndani ya kanisa

5. Udhaifu na Ulemavu wa KANISA LA LEO ni matokeo ya VIUNGO vingi kulala na kutofanya kazi ipasavyo, na hasa VIJANA. {Mithali 25:14;}

Kijana Usilale au Kujiweka nyuma katika majukumu ya Kanisa Hebu amka Ufanye kazi Kama Mimi Baba Yako wakiroho Pastor Richard

6. Kijana anayeweza kuleta MABADILIKO kwenye KANISA ni Yule ambaye tayari ametambua thamani na nafasi yake kama kiungo katika MWILI wa KRISTO yaani KANISA, na anatumika katika kiwango na muda husika /sahihi {Yohana 4:34}

Kanisa ili Liendelee nakukua huhitaji Vijana wengi waamke wafanye Kazi ya Bwana wapewe kipa umbele ndani ya Kanisa

7. Ili Kijana Mkristo atumike vizuri kwenye KANISA ni lazima ajifunze kutoka kwa Yesu. Yesu ni mfano bora wa kuigwa na kielelezo sahihi cha maisha kwa Kijana yeyote.{1Yohana 2:6; Yohana 13:15;Mathayo 12:30;Mathayo 11:29}

Kijana chukua Siku moja TU ujifunze kwa Yeremia Daudi Samweli KWANINI wao waliweza Kumtumikia Mungu nakutembea ndani ya Kusundi la Mungu Kisha chukua hatua maisha Yako kuyajenga Kiroho na Kimwili. Mimi Ni Kijana mwezio rafiki Yako Mpendwa Naitwa  Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa

Simu piga Jioni saa 12 00 kwa Namba +255759861768 nieleze Ni Nini Tatizo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.