SOMO:NATAKA MUNGU ANIJIBU

SOMO; MIMI NATAKA MUNGU  ANIJIBU NIFANYAJE 2021.?

Je ulishawahi Kujiuliza Swali Kama Hili Kuwa Nimekuwa nikiona Shuhuda mbalimbali Watu wakitendewa na Mungu Akijibu nikisoma maandiko Naona Mungu alijidhihirisha Kwa viwango vikubwa kwa kina Elia Musa Yesu Na Kina shadrack Na wezake Unafikiri kwanini kwako humuoni
Karibu Somo Hili au muongozo wa Kumgusa Bwana Naitwa Bishop Richard
Tusome👉🏿👇Luka:8:45-47 👉🏿Yakobo;2;21👉🏿Mwanzo;12👉🏿1Wafalme;18;25-40

MUNGU huwa ananjia au Fomula Yake Ukitaka umguse mpaka nguvu zake azielekeze Kwako huhitaji muda wako na Kujitambua wewe Ni mwanae kwake Mpango na Kusundi lake Ndani Yako Ni Kukubariki nakukuinua Sasa utafikiaje hatua hii ya Kumgusa Bwana nakuinuliwa huwa TUNAITAJI TUMGUSE BWANA NA KUMFANYA TUMFANYE USO WAKE ATAZAME.

MAMBO MAWILI TU HUWA CONNECTION YA KUMFANYA MUNGU AJIBU Mfumo huu ulivyo hata Watu Wa Shetani Wanayoconnet mbili tu.

A: MADHABAHU
       1 wafalme;18;25-37
Madhabahu:- huwa Ni Mahusiano Kati ya wewe na Mungu ndani Yako

Mahusiano hayo hujengwa hivi
1:Wewe Kuipenda Nyumba ya Bwana na Kutoa Mali Yako Kujenga na kuchangia Kazi ya Mungu Au Kununua Chochote na Kupeleka kanisani au kuijali nyumba nafamilia ya mchungaji wako.
Agalizo;Ukifanya ufanye kwa ajili ya Bwana na Hupaswi uaze mdomo kumuongolee mchungaji wako utafuta kila Kitu.

2;Kufanya Kazi ya Kumtumikia Mungu na Kusimamisha Huduma Yake Kama Ni uimbaji hakikisha unasimama Kama uchungaji simama .

3:Kuhakikisha UNAKUWA na mlezi wa kiroho hapo utatambulika kwa Fungu la KUMI na UTOAJI wa Ushiriki Kujenga nyumba ya Mungu 👉🏿👉🏿Usiposhiriki Chochote Fungu la KUMI ukalipeleka pengine hata MAJIBU Yako ile Madhabahu haitakuletea na ukisema Madhabahuni pako usitoe yaani Baba Yako wa Kiroho Ujue ile Madhabahu itawahudumia TU wale wanaoijali na kuituza.👉🏿👉🏿Tunaona ibrahimu alibarikiwa Baada ya Kuijenga Madhabahu ya Bwana Hata Elia Moto aliushusha Baada ya Kujenga Madhabahu.

HIVI NDIVYO UNATAKIWA UJENGE MADHABAHU NDANI YAKO UTAONA MGUSO WA BWANA USHUHUDA HUTEKWA NA MTU ANAEITUNZA MADHABAHU YAKE KAMA ULIKUWA HUJAWAHI FANYA CHOCHOTE KANISANI KWA BABA YAKO NA MADHABAHU YAKO UJUE umejifunga usione Mkono wa Bwana

B: SADAKA YAKO

Waebrania:13;16

Mathayo : Mlango 23

19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka

Tafsiri Ya Sadaka Ni Kujitoa kufanya Jambo Kwa Ajili ya Bwana Sadaka unaweza Kutoa Pesa Elimu Yako Kipaji Chako Mali zako mashamba Viwanja Ukifanya Jambo Hili au linaloendana nakitendo Cha Kutoa Unamfanya Mungu Ajibu Maombi Yako.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri Sadaka ni Pesa TU hapana hata elimu Yako mfano Kama Mimi nikiwa ninahubiri injili mtandaoni  na Kushiriki Kuwafanya Watu waokoke waache DHAMBI lazima Mungu aniinue kwa Kuwa Mtandao nautumia muda wangu kwa Ajili ya kuwaleta Watu kwa Yesu Je wewe Simu Yako au Ukurasa wako group lako umewaleta wagapi kwa Yesu hakuna umefanya Jambo ngani Kanisani hakuna Ikiwa Wewe Huna muda wa Kujitoa kwa Ajili ya Mungu Ni ngumu KUMFANYA Mungu AJIBU

MTUMIKIE MUNGU KWA ULICHONACHO NENDA KWA BWANA NA PESA ZAKO


Naitwa Bishop Richard


Je unatamani Kuniuliza nipigie au tuma sms nitakupa muda wa Kupiga


Simu+255759861768



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.