Darasa la ndoa

DARASA LA WANANDOA✍️✍️MAMBO YA KUZUNGUMZA KAMA WANANDOA.

Naekuletea Darasa Hili Ni Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richar

Wanandoa Wanapishana Kauli na Kukosana ndani Kwakuwa Kila mmoja Anakuwa hazingatii Maisha ya ndoa ndani ya NYUMBA Karibu Tufunzane nakujengana Ndoa Zetu.

NDOA HUJENGWA KATIKA MISINGI YA MUNGU NA HUTAKIWI UOLEWE AU UOE KWA KUBAHATISHA AU KWA TAMAA YA KIGONO

Mambo haya Wanandoa Hutakiwa Kuyazingatia Mambo matatu la nne utaongeza hapo mwanandoa.

1;Kusikilizana Nakuwa Makini mwezako anapoongea Siyo Anaongea Upo na Mambo Yako

Wanandoa Wengi waliopo Kwenye ndoa hasa Kundi la Wababa hupenda Kusikilizwa Tu wao lakini wao Kusikiliza maoni ya wake Zao huwa ni kazi na hii husababisha ndoa nyigi Uchumi wake ushuke Wasipinge hatua nakuvunjika kwa ndoa👉🏿👉🏿Wewe Ukioa Usioe Kwa Kuwa unataka uonekane kwa Watu owa ukiwa umejipanga Kuingia Maisha mapya utakayotakiwa ndani Kama Wanandoa msikilizane
Yakobo;1;19

2:MSIDANGANYANE NA MHESHIMIANE NINYI WOTE WAWILI.

Ndoa nyigi zinakuwa na Upendo wa Kuingiza yaani Kama tamthilia au Bongo movie wanavyoingiza na Wanandoa Wengi wamekopi Maisha hayo nakuishi ndani huku wakidanganyana nakupeana Taarifa za Uogo ooh Leo nitaenda kusuka kumbe Safari ilikuwa ya kwenda kwa shangazi ooh Mimi huyu rafiki yangu kakosea namba kumbe mchumba wa Pembeni. KWANINI unakuwa muongo muongo wakati unaemdanganya mtu mzima mwezako Umetolewa MAHALI Tulia na ndoa Yako wewe mwanaume Hukuoa mtoto wa wawatu umtese au unamfanyia vituko nikwanini uowe ukiwa unajua hutaki Kubadilika sababu ndoa huhitaji mambadiliko kiakili kifikira na MTAZAMO wako
Walawi;25:17

3:MKATAZANE NA KUKEMEANA MIENENDO ISIYOMPA USHUHUDA MUNGU.

Wewe mwanandoa mwezako Kama anakuambia Acha Tabia Fulani au mwenendo Fulani Acha Mara moja usiwe Mtu ambaye Hutaki kuacha Tabia Zako njia inayomkwanza mwezako wewe Ndio unafanya Tena unamwambia utanifanya Nini SI Kama umechoka ondoka huo huwa Tunauita Uchanga wa Kiroho uliopitiliza Tengeneza ndoa Yako mpaka wengine wakikuona Upo na mkeo wanakutamani sio mtu aliye nje unamfanya aongope ndoa
Marko;1;43

HITIMISHO

Kubali Kuijenga ndoa Yako Katika Msingi Wa Mungu mfurahie maisha mazuri ya ndoa

Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro veta Dakawa
WhatsApp+255759861768
14/1/2021

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.