SOMO:MWANAMKE TAMBUA NAFASI YAKO.

SOMO:MWANAMKE TAMBUA UTHAMANI WAKO

Vitabu;Mithali;21;9-19 Matendo;9;15-17 Esta:Sura ya 5 mpaka 9 Mwanzo;5;2 Mithali:12;4 1wakoritho;7;16-20

Biblia inamtambulishaje mwanamke mcha Mungu anayetembea katika kusundi la Mungu👉👉

Zaburi : Mlango 68

11 Bwana analitoa neno lake;Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa

Mwanamke Akisimama Vyema Katika Nafasi yake huwa Neno hili hutimia ndani yake. Lakini Mwanamke Asiyesimama Nafasi yake Na Kutumia Vyema Neema aliyonayo Atakuwa Kama Delila Nakatika Kundi au Jeshi Tutapata Dorcas na Tutampata Delila

Wanawake wanaomuwakilisha Delila Ni wale hawajasimama Nafasi Yao kwa Usahihi(Waamuzi:16;10-16

Wanawake wanaosimama Nafasi ya Doricas Ni wale waliosimama katika Nafasi zao katika Kanisa na kwenye Jamii kwenye ndoa zao;(Matendo;9;10-19


Mwanamke Katika Kanisa na Jamii Ananafasi Kubwa Kama Biblia Inavyomtambulisha Karibu Naitwa Pastor Richard Somo hili Linalenga wanawake Kujitambua Ndani ya Kanisa wao Ni Nani pia inaenda kuwajengea Kusimama nakufata nyayo za kina Eva Esta Dorcas na mariamu mama ye Yesu.

Mifano hiyo kwenye Biblia inayowaimarisha Kujiona ndani Kunakusudi Kubwa Mungu Ameliweka lituzwe.


1;MWANAMKE NI MWANAHARAKATI WA UKOMBOZI.

Mwanzo;3;15 Esta:5

Mwanamke Ni Mtu aliyeandaliwa toka Zama za Kale kuwa Chanzo Cha UKOMBOZI na Mabadiliko la Eneo lolote mahari popote atakapoenda kukaa Mungu humtumia Kupabadilisha nakupaweka Pakae Katika mpangilio sawa wakuonekana kimwili na kiroho

Mwanamke akikaa nafasi take Ananguvu ya Kuleta mafanikio na Kuongeza pato la uchumi wa familia yake.


2: MWANAMKE ANATAKIWA AJISHUGHULISHE NA SHUGHULI ZAKE.

Matendo;9;16

Mwanamke Asiyesimama Nafasi yake Anajua Anatakiwa Awe mchango wa Kuleta UKOMBOZI wa kiuchumi ndani ya familia na kwenye ndoa take.

Mwanamke hapaswi Akae nyumbani bila kishughuli Cha kumuingizia Uchumi Tunaona kwenye Biblia wanawake walikuwa wanafanya kazi hautakiwi ufungwe na ufahamu wa Kumtengemea MWANAUME KILA kitu na Kumfanya mmeo Baba Yako hapana mmeo Ni mmeo na Mzazi Ni Mzazi.


3:MWANAMKE MLEZI WA MMEWE/

Mwanzo;2;21-23

Mwanamke unatakiwa usimame nafasi unaporudi nyumbani Kuvua cheo Chako Elimu yako na Kutimiza majukumu ya ndani ya Nyumba Kama MKE mwema 

Mlee mmeo mnyoshee nguo mfulie mpendezeshe nakumuongoza mmeo katika mwelekeo mzuri.


Kama ikatokea umeolewa na mtu AMBAYE hajaokoka Biblia inasema usimuache huyo mwanamme au ukawa unaishi nae usimuache(1wakoritho;7;13)

Ndio unapaswa mwanamke utumie nguvu ya ushawishi Aokoke sio umuache mme Kama huyo.

Pia mama Mlezi na mwangalizi wa watoto hata familia Mungu Alimpa nguvu ya uongozi ndani Yake Kumbe Anatakiwa pia Ajitoe kwenye Jamii kanisani katika maswala ya kuongoza.


4; MWANAMKE NDIO WAKUOMBEA KANISA NA KIZAZI CHAKE.

Yeremia:9;17

Wanawake ndani ya Kanisa huwa ndio wanapaswa kuliombea kanisa KUSIMAMA kufunga na Kuombea Uzao na KIZAZI Chao Biblia inawatambua Kama wanawake waombolezaji wanaomulilia Mungu kumuomba Mungu Kuombea kanisa.

5;MWANAMKE NI MZAZI Mwanzo;1;28

Mwanamke Biblia inamtambulisha Kama Mzazi pia Ambaye Mungu Alimpendelea Kumpa Utashi na hekima Yenye mapenzi ya dhati kwa mwanae 

Unatakiwa mwanamke Ujue we unehekima Upendo Mkubwa Kama Mzazi kwa mwanao.

6:MWANAMKE NI USTAWI WA KANISA NA FAMILIA

1samweli:2 Mwanzo:4

Mwanamke Ananguvu ndani Yake yakusitawisha Mambo yaliyolala nakumfanya Mwanaume afike mbali kiuchumi Kimalengo Kutokana na nguvu ya mvuto wenye kushawishi na Kubomoa ngome Sungu au Akili isiyobadilika ndani ya Mwanaume Anapoingia Kama Mwanamke Anaejuathamani Yake humbadilisha kijana au Mwanaume kitabia na mienendo 


Mwanamke hushawishi Mwanaume aweze kufanya hata Kile ndani ya Akili Yake hakikuwemo au hajawahi kukiwaza.


UNAJUA

Kuna wanaume Maisha Yao yalikuwa yanaenda kuwa mabaya Sana lakini toka walipooa au Kuwa familia maisha Yao yamependeza wamebadilika kabisa Wapo tofouti na walivyokuomba kabla ya Kuoa. Wanawake ndio wamewatengenezea maisha mazuri.


Kila Kitu ukikiangalia Mungu Anamtumia mwanamke Asilimia Kubwa kumuongoza mwanamme nakumfanya Aonekane wa wathamani katika jamiii pia Mungu Anamtumia mwanamke kukomboa Vijana wakike na WAKIUME.

Ndio maana mwanamke Anaemjua Mungu nijeshi Kubwa

Zaburi;68;11.


Hitimisho

Wanawake Wanaosimama Sasa wasimame katika zamu Yao ili kuleta mabadiliko ya Kiroho na kimwili.


Mungu Anachukizwa na mwanamke asiyejitambua nakusimamia majukumu Yake Kama mama Mzazi msaidizi mpambanaji.


Inuka mwanamke Jitambue nafasi yako.


@Pastor Richard 2020

Simu+255759861768


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.