SOMO: NGUVU YA UMOJA

🎙️🎙️DARASA LA NENO🎙️🎙️

🔥🔥SOMO: NGUVU YA UMOJA

Tufunue Yohana:17:21-24 Zaburi:133:1 Waefeso;4;3

MWALIMU: Pastor Richard
NIPO Morogoro veta Dakawa
Simu+255759861768

Mambo mengi hayaendi vizuri na yanaishia njiani Iwe ndani ya ndoa Zetu familia Zetu mahusiano yetu katika Huduma Zetu makanisa yetu
Kwa sababu yamekosa nguvu ya umoja Lakini yatakaponjegwa kwa umoja Kama kristo Yohana;10;30

Karibu Leo Nataka nifundishe Nguvu ya umoja.

Naitwa Pastor Richard NIPO Morogoro veta Dakawa

🔥🔥 NGUVU YA UMOJA NI NINi?? Ni Ushirikiano na SAUTI moja Kama watoto wa Mungu.

Lengo la SoMo;Tujenge kanisa na jamii Yenye umoja.

Dhima ya Moto wa Yesu;Watu wafundishwe Neno la Mungu wakombolewe

Faida Ya Umoja

1;Kujengana katika Misingi Yenye mafanikio.

2:Kusaidiana na Kubebana kwenye matatizo na matukio mbalimbali

3:Kuwa na SAUTI moja inayopaza kunena utetezi kwa mwingine.

4:Kufika juu kimaendeleo na kimawazo pia.

5;Kanisa na familia Zetu zitastawi katika mafanikio

6:Kuongelea changamoto na kuzitatua pia

7;Mwana umoja anapopatwa na kitu wezake watamsaidia.

Hasara ya Kukosa Umoja.

1:Haitakuwa na Misingi iliyo hai katika kanisa au familia

2:Hamtasaidiana katika Mambo yoyote

3;Familia au kanisa huwa linakuwa dhaifu Sana

4;Ndoa huvunjika,Familia kutokujaliana,Ukoo kanisa linakuwa halishirikiani,Washirika watahama hama Kutokana na nyie wachungaji hamuona umoja mtachafuliwa Na Waumini wenu kwa kuwa nyie wenyewe wachungaji hamna umoja.

5:Wachawi na roho ya kanisa kutoendelea hulivaa kanisa kukosa mwitikio wa umoja.

6:Familia huwa zinakosa mfuko wa kusaidizana kwenye matukio mfano ya msimba nk

7:KILA mmoja huwa Peke yake peke yake Anaenda tu MKE Anawaza hili na MWANAUME Anawaza hili mipango Yao inakuwa ipo chini chini KILA mmoja anamficha mwezake.

Tunafanya Nini Sasa.

1:Itisha kanisa lako,Familia Kisha Wekeni mikakati ya kukutana pamoja Kuongelea familia Yenu au kanisa lenu.

2:Changueni Kiongozi atakayewasimamia ndani Yenu humohumo.
Kiongozi awe na UWEZO huo

3:Kama wewe Ni Mzazi unawatoto wajengee Misingi watoto wako wanakutana Kuongelea Mambo ya familia UFANYE hivyo Mzazi kabla ujafa utawajengea Msingi mzuri endelevu.

4;Kama Ni Mchungaji weka utaratibu KILA mwisho mwenzi kaa na viongozi wako muangalie kanisa Nini bado unakwama.

5:Onesha Ushirikiano na muweke Katiba au utaratibu utakao kuwa Kama Amri ya mwanaumoja afanye.

HiTIMISHO

Kwa kuwa na umoja tutafanya Mambo mengi makubwa na kushirikiana.

Wito
KILA aliyenguswa na SoMo hili alifanyie kazi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.