SOMO;Misingi 3 Ya Kabla ujaingia ndoa
✍️✍️SOMO; MISINGI MITATU (3) YAKUBORESHA NDOA YAKO IWE YENYEFURAHA NA YAKUDUMU KATIKA AMANI✍️✍️✍️Chukua hii Ufurahie ndoa yako🙏🙏
Karibu Mtoto wa Mungu Tuelimishane nakujifunza Katika nguzo tatu za kuandaa ndoa iliyobora ndoa Yenye Amani na furaha ya kudumu
Tufunue Biblia Zetu 1Timotheo;2;11-14, 1wakoritho:7;2-39 ,11:1-13 Mwanzo;34;12 Mithali;30;10
✍️✍️Lengo La Kuwepo Darasa la Wanandoa ✍️🙏Ni kufufua mahusiano yasiyodumu nakufikia Malengo kuwajengea Elimu ya KuZijenga na kuimarisha ndoa Zetu Kama Kristo Alivyolijenga kanisa lake.
✍️✍️DHIMA YETU Kama Moto wa Yesu Kufanya ndoa ziwe na Amani na upendo uliojazwa hofu ya Mungu.
✍️✍️Misingi Nini ? Ni chochote kinachosimamisha Jambo liwe imara
✍️✍️✍️Darasa la Wanando
✍️✍️Mwalimu Wa Wanandoa.
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu +255759861768
KILA kitu ukikiona kimesimama imara ujue Msingi wake ulijengwa imara lakini ukikuta chochote watu wanagombana hawaelewani Ugomvi kila wakiwasiliana majibishano Yao Ni Ugomvi hakuna maelewano mazuri ndani MWANAUME hatulii ndani Ujue ulikosea mwenyewe muoaji au muolewaji kwa Kukosa kuandaa na kupanga Msingi uliobora ukaanza kushusha tofali tu usichimbe Msingi wako.
Karibu darasani ujifunze
Hatua Hizi Tatu huwa Misingi ya ndoa iliyo na nguvu na upendo.
1️⃣✍️🍉🌱MWANZO WA MAHUSIANO YENU.
Katika kipengele hiki wewe unayeanza Kuingia kwenye mahusiano au uchumba kuanzisha unatakiwa uzingatie hatua Hizi ili Kumfanya mchumba wako kufurahia na kukupenda Zaidi. Baadae msije mkaanza kuchokana mkiwa kwenye uchumba tu.
1:Uwazi Usiwe Msiri kwa Mwezako.
Chukua Nafasi hii ya Kumwambia ukweli Katika maisha yako pamoja nakumpa historia yako Kumwambia Kama unamtoto ulishaoa au Kuolewa Unachopenda na Usichokipenda ufanyiwe
Usiagalie Atapokeaje Kama Atakuacha kwa Sababu ya kumuweka wazi Ni Bora Zaidi kuliko uingie ndoa isiyo na Amani
Mshirikishe Mwezako ili Akupe Mawazo na Ushauri
2;MASILIANO YA KARIBU NA MBALI.
Hatua hii huwa inawaweka Karibu na kuwafanya nyie wachumba muwe na upendo msichokane nakuyafanya mahusiano Yenu yawe hai.
Tenga muda wa kukaa na mkeo/Mmeo mtarajiwa pia Tenga muda kuongea nakuwasiliana nae Kama utamtumia sms EPUKA kutuma sms zinazo mkwanza au zinazoenda kuua uchumba wenu.
Mfano: Hi, Mambo vip, niaje, Pw, Hbr. Krb ul chkl mtindo huu haufai umtumie mchumba wako itakavyoendelea itamfanya Awe Kimya Mawasiliano Yenu yawe yakulazimisha na MWANAUME aliyemakini anayetaka MKE mwema wa Kuoa Huwa Anaitaji Asome sms ieleweke isiwe kwa ufupi mkato.
Mfano; Umeamkaje Mme wangu/MKE wangu Karibu chakula mme wangu Tumia maneno yaliyo hai pia katika mahusiano Yenu
Maneno hayo
a-Nakupenda
b-Samahani
c-Ansate
d-Pole
e-Karibu
Maneno haya huweka hai mahusiano Yenu na kustawisha yatumie Mara kwa Mara kwa mwenzi wako wa uchumba.
3: BADILIKA NA ACHANA NA MAKUNDI.
Hatua hii inatakiwa ifanyike Mwanzo tu wa mahusiano Na Usiingie na Tabia zako zilizokuwa mchumba wako hazipendi. Anza kuacha Tabia zile Ambazo Mwezako hazipendi Taratibu usiendelee ukaanza Kujipa moyo atabadilika ndani ya ndoa ujue Utaharibu Msingi wa ndoa Ni Bora ukavunja mahusiano hayo kuliko uje kwenye ndoa unalia kila siku.
🚻🚫Huu Ni Msingi Wa Mwanzo Kabisa mkiwa Bado Tu Marafiki Wachumba Kabla hamjaoana Tahadhali kubwa Usifanye makosa.
2️⃣🌱🍉✍️KATIKATI MWA MAHUSIANO YENU.
Hii hatua Huitwa KATIKATI kwa kuwa watu Hawa huwa wameshafikia hatua ya ndoa hatua wameshaenda kwa wazazi wamepata Baraka Zote za Wazazi.
Mambo Ambayo unatakiwa uyapitie uyazingatie katika hatua hii.
1;AGANO LA UCHUMBA
Hakikisha uchumba wako toka Mwanzo Unapoanzisha weka Angano la Uchumba Msizini mpaka mfike kwa wazazi. Uoneshe msimamo huo ukiona mchumba wako anakuongoza kuzini au Anataka uzae nae Kwanza ndio akuoe ujue huyo SI mme mwema au MKE mwema
Usifanywe singo mother kabla ya Kufika kwa wazazi usikubali ukalea UZINIFU kwa Sababu ya umri unaona unaenda. Tulia na Uendelee kuomba Mungu atakupa Aliyesahihi.
Kuna Hatua Tatu za Kuweka Agano.
a.Kuwa Marafiki
Hii huwataka muwe Karibu na kufahamiana kitabia mienendo kuchunguzana
Hatua hii huwa hamjaenda kwa mchungaji au kwa wazazi
Tunaposema uende kwa wazazi uende ukayatambulishe mahusiano yako yawe na uhalili sio mzini kabla hujayarasmisha.
Katika hatua hii hampasi kuzini au kuanza kudaganyana hapa muaze kuwekana wazi kila kitu unachopenda na usiyopenda ufanyiwe.
b.Kwenda kwa viongozi wa dini
Hii hatua unatakiwa mweleze Mlezi wako wa kiroho Kisha atakupa muongozo wa nyie kwenda kufata hatua Zote.
c.Kufika Kwa Wazazi
Hi huwa ndio hatua ya mwisho inayokupa uhalali ambayo hatua hii Usifanye Kama bado Hujajilizisha na kuwa na utayari wa Kuolewa na mwanaume/mwanamke usithubutu kuolewa au kuoa kwa kukizi haja zako za kigono.
Hatua hii humpa uhalali mtu Kuingia kanisani na ndoa ikafungwa hapa haparukwi ukataka uchukue Ndugu wa kabila Ni makosa
Hakikisha hauzini na mwanaume na mwanamke mpaka Umefika kwa wazazi ukienda kinyume utajikuta Mahusiano Yako yanakuwa hayadumu
Mungu Akupe hatua Ufikie Hapa kwa wazazi Basi mtakuwa mmejenga Msingi mzuri usiaze kuitwa singo mother kabla ndoa haijakufanya kuwa MKE halali.
3️⃣🌱🍉🚫 MWISHO WA MAHUSIANO YENU.
Hii Huitwa mwisho maana Hukupa Msingi wa maisha ndani ya ndoa na familia utakayoipata
Hapa Tayari unakuwa ndoa yako inaamani Na furaha
Mambo ambayo hapa Utajenga Mwisho Mzuri wa ndoa yako.
1:UMHIMU WA MWENZI WAKO
Hakikisha mwenzi wako unampa nafasi ya Kwanza unathamini na kuepuka kufanya moyo wake uwe na huzuni mjali na kumrekebisha anapota arudie Tabia zake na atabadilika sababu Msingi uliujenga vizuri toka Mwanzo.
2;MTOSHELEZE
Hapa hakikisha mwenzi wako unamtimizia Mambo yafatayo bila kusuasua.
a:Tendo la ndoa
Hakikisha Tendo la ndoa Unamtosheleza Mmeo/mkeo Usimpe nafasi Shetani Akaanza kuwavurunga Kupitia Tendo la ndoa maana moja ya wajibu wako Mkubwa wa ndoa Ni Kumtimizia Mwenzi wako Tendo la ndoa.
b:Muongozo Mwema.
Mfundishe Na kumwelekeza mwenzi wako Amjue Mungu awe na Hofu na kumjengea kuwa mwenye msimamo wa upendo wenu nakuwa Hondari mwenye kujiamini katika Utafutaji mfundishe yote yanayomjengea ujasiri wa kufanya kazi na Kumpenda Mungu.
c:MTHAMINI NA KUMPA KIPAUMBELE
Ndoa njema huhitaji msimamo wa watu wawili Kati ya MKE na mme hutakiwa wasimame nakupeana kipaumbele usiruhusu mtu mwingine Akaanza kuingilia ndoa yako au upendo wenu usikubali kuyumbishwa kwa ndoa yako na ndugu wazazi marafiki no
Simamia na Linda ndoa yako kwa maombi TU
Hakikisha unajenga pembe tatu kwenye ndoa Yako
-Mungu mmoja
-Mme mmoja
-Mke mmoja
Mungu Awabariki Kupitia Mafundisho haya ya Wanandoa Yataenda Kujenga ndoa Bora
Hii ndio Misingi ya wewe Kujenga ndoa ya Amani na Furaha
Naitwa Pastor Richard
HITIMISHO
Anza Kujenga nakuandaa ndoa Bora sio ndoa itakayokufanya Usifanye kazi yako kwa Umakini uwe unalia unaumizwa kila siku.
Comment na share
WhatsApp +255759861768 Pastor Richard
Maoni
Chapisha Maoni