SOMO;MAMBO YANAYOLINDA UCHUMBA
🗨️.SOMO; MAMBO YAKUFANYA ili KULINDA UCHUMBA WENU USIVUNJIKE.
✍️✍️DARASA LA WANANDOA
✍️✍️MWAL WA WANANDOA
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Mithali:30;9-10 Mithali;12;4
KARIBU KATIKA DARASA LA WANANDOA Tuongelee Mambo unayotakiwa uyashike mahusiano Yenu ili kuyalinda yasivunjike Unapaswa chukua Elimu hii
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:✍️✍️ Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa Awana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
2. Upekee wa mambo ya mwezi wako:✍️✍️ Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
3. Mwenye maamuzi unayoyachukua:✍️✍️ Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.
4. Kuwa na subira:✍️✍️ Usichukue maamuzi ya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yanayohusu uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.
5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: ✍️✍️Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine.
6. kuwa mbunifu’ : ✍️✍️ Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu. Vile vile kuwa mbunifu wa mambo mbalimbali kwa mwezi wako kama vile kuhakikisha unajua vitu gani anapenda ukimfanyia au vitu gani hapendi ukivifanya.
7. Kuweni peke yenu: ✍️✍️Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi. Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi
Maoni
Chapisha Maoni