SOMO:BINU (7) ZA KUBORESHA MAHUSIANO MNAPOANZA MAHUSIANO

✍️✍️✍️SOMO; BINU SABA(7) ZA KUBORESHA MAHUSIANO MNAPOANZA MAHUSIANO.

Mithali;31;7-12 Mithali;12;4

✍️✍️ MASOMO ya WANANDOA
✍️✍️MWAL.PASTOR RICHARD
✍️✍️SIMU+255759861768
Nipo Morogoro Veta Dakawa

Karibu Katika DARASA la Wanandoa Leo naongelea Mambo mhimu unatotakiwa uyafanye ukiwa ndio unaanza mahusiano Yako au ulishaanza mahusiano lakini umeyafanya mzoeane mpaka vitu vigine ulivyokuwa unavifanya saivi huvifanyi Basi Karibu ujifunze

Cha Kwanza Msingi wa mahusiano Yako au ndoa huaza kutengenezwa mkiwa ndio mnaanza ukifanya makosa hapo unaweza kuadaa kitu kitakachokunyima Amani.

1.✍️✍️Mwanzo  wa Mahusiano.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
Msidanganyane(a)Mwambie mwenzi wako ukweli.
(b)Mwambie yale unayopenda na usiyopenda.
(c)Kuwa muwazi kwa mwenzi wako.
(d)Onyesha upo tayari kuachana na mambo yote uliyokuwa umeyazoea ambayo kwa sasa yanaweza bomoa uhusiano wenu.

2.✍️✍️Mfanye Mwenzako Ajisikie ni wa Muhimu.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈😮😮
(a)Tenga muda maalumu wa kuwa naye.
(b)Onyesha unafurahia uwepo wake.
(c)Mnapozungumza jambo onyesha umakini kwa kumsikiliza na kuacha kila kitu.
(d)Usijifanye unajua kila kitu na kwamba yeye hajui.
(e)Hata anapokosea mwonye tu na kumuelekeza kwa upendo.

3✍️.✍️Usifanye Mambo Kwa Mazoea.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
(a)Kila siku ona ni fursa mpya ya kufanya jambo kwa ajili ya koboresha uhusiano wenu.
(b)Mfanyie jambo jipya ambalo hategemei kwamba utamfanyia.
(c)Usifanye jambo litakalomfanya ajione hana thamani tena kwako.

4✍️✍️Usipende Kushikilia Mambo Kwa Mda Mrefu Bila Kusamehe.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
Anapokosea mweleze kwa upendo na umwambie umemsamehe.
Usiwe mtu wa kurudiarudia mambo kila anapokosea unakusanya makosa anapokosea tena unamkumbusha.

5✍️✍️Kumbuka Aliwaacha Wengi Akaamua Kuwa na Wewe.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
Sasa usijifanye wewe ni mjanja kuliko wote.
Mwonyeshe yeye ni wa kipekee.
Usipende kila wakati kuelezea mambo ya mpenzi wako wa zamani.

6✍️✍️Onyesha Hisia Za Kweli Kwake.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
Kumkumbatia mnapokuwa faragha.
Kumbusu na kumwambia maneno matamu,wengine husema maneno yanayovunja mifupa.
Mfano:Nakupenda wewe tu mpenzi wangu,hakika siwezi kukuacha mpenzi wangu, Unaniweza wewe tu mahabuba.

7✍️✍️Mtosheleze.
🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈🎈
Husika na mahitaji yake ya kimwili na kihisia.
Hakikisha anajisikia vizuri anapokuwa kwa kumtimizia mahitaji yake ambayo una uwezo nayo yale usiyoweza shaurianeni.
Jambo analolipenda lipe kipaumbele.
Tendo la ndoa au mapenzi yafanyike kwa usahihi na kwa kutoshelezana.
“Watu wengi  wakishazoeana tu wakazaa watoto basi wanaona  tendo la ndoa siyo jambo la muhimu ni swala la dharura,na np utapata mallalamiko mengi kwa wanandoa ama wapenzi wakisema zamani tulikuwa vizuri ila sasa amebadilika




HITIMISHO 

Hakikisha Unachukua nafasi ujifunze kitu Kuhusu Somo hili ili kuujenga Uhusiano Wako vizuri.


Share Somo hili.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.