Somo: Dalili za mme mwema

✍️✍️SOMO;✍️ DALILI ZA KUJUA UMEPATA MME MWEMA/MKE MWEMA ULIYE NAE UTAMJUA KWA HAYA,

Mithali;31:7-11
Mithali;12;3-6

✍️✍️DARASA LA WANANDOA
✍️✍️MWAL.PASTOR RICHARD
✍️✍️SIMU+255759861768
Nipo Morogoro veta Dakawa.

✍️✍️Tunakutana Katika Masomo ya Wanandoa Kwa Lengo la Kutunza Ndoa Zetu na Kujua mahusiano yetu yapo sahihi nakuyajenga yalipobomoko Kiukweli Katika Jambo la Kupata MKE mwema au Mme mwema Ni rahisi Sana ukiwa mvumilivu na mwanamaombi usiyechoka kumuomba Mungu na Msimamo utakipata kilicho Bora Kwako na chenye Faida katika maisha Yako.

✍️✍️Wapo watu huamini mme mwema hayupo au MKE mwema hayupo Wapo Sana shida watu wa Ni Adimu Sana wanapatikana makanisani tu

Lakini wanaume waliokamilika Wenye hofu ya Mungu Wanapatikana popote unaweza kutana nao hata mtandaoni hata Kwenye usafiri hata Lakini Mme mwema Hutamuona Popote isipokuwa ndani mwa nyumba ya BWana.

Karibu Nataka nifundishe Dalili Za Kujua UMEPATA MME MWEMA

✍️✍️MASILIANO
Mtapata kuwasiliana na mme mwema kwa Muda Aliouweka Kama saa Moja Basi mtaongea na kuchat Hatapoteza muda wote Kila wakati au mida yote Anawasiliana. Ataweka muda maalumu.

Na Atapata muda wa kukufundisha kukueleza maisha ya ndoa njema na Kumtengemea Mungu.

Kwa kuwa umempata Kanisani muda mwingi Atakuwa Yupo na Mungu yeye na ibada yeye na Kanisa Usiaze kushangaa

Lakini Mme mwenye hofu hutamkuta muda mwingi kanisani lakini Mme mwema utasikia naenda kwa mchungaji naenda kanisani.

Tabua hata chat Zenu zitaonyesha uhitaji wake wa kufika hatua nyigine Kama kuyatambulisha mahusiano Yenu hii Ni hatua kubwa Sana ukipelekwa na mme mwema kwa wazazi wake Ujue Amejiridhisha Juu Yako.

✍️✍️MAZUNGUMZO
Maongezi Yenu au MAZUNGUMZO Yenu ataongelea maisha ya mbeleni Ataongelea historia Yake umjue vizuri Ataongelea kusundi lake kukupenda Atazionesha hisia hizo kwa Maneno macho Sura Yake

Unachotakiwa Ni Kupata muda kumsoma katika maongezi Yake na muda mwingi atatamani mahusiano Yenu yanaenda hatua igine.

✍️✍️UAMINIFU
Atakuwa Mwaminifu Sana Wala Huwa Hana Hofu ya Kufikiria mke wake Sababu Anajua Kama Amepata MKE Basi Ni mwema Kama Yeye Ikiwa Mungu Amempa MKE hawezi kukosea.

Husimama Kuwa na Imani na Uaminifu kwa mke wake hawezi kupenda Mara mbili au Kurusu Mwingine Aingilie uhusiano wake.

Utaona tu katika Dalili zitafatana na matendo Yake mema yaliyojawa Ushirika na Mungu muda mwingi.

Hupenda uwe Mwaminifu nawe

✍️✍️SIRI
Atatuza Siri zako na madhaifu na Kila utakachomweleza hatakisema nje Huwa wamejawa na Uaminifu wenye kuhifidhi madhaifu upendo was ajabu Nguvu ya uamsho wa mahusiano hutamchoka maana ajua kutubu na kujishusha akikuuzi ukamwambia pia msikivu.

Huwa Hana haraka ya penzi lako au kufanya tendo la ndoa kabla hajakupeleka kwa wazazi

Anajali thamani Yako ukimwambia kitu Anakuelewa na atakifanyia kazi.

Hupenda mwanamke nae Ajue kuwa na Siri mtuza Siri za ndani

✍️✍️MSAMAHA
Anapenda kutumia Neno MSAMAHA pale Anapokosana nawe au kupishana Kauli
Ataomba msamaha na Atabadilika pia  nawe huhitaji hivyo uwe

✍️✍️MAKUBALIANO
Husimamia Sana Kile mnachokubaliana kwa hiyo akikueleza kitu ujue Atakuja kukifanya Kama amekueleza atakutambulisha mwaka huu ujue itakuwa huwa hapendi ukubaliane nae wewe UFANYE Tofauti na mapatano Yenu

Kwa hiyo ukimpata Basi uwe makini unapoongelea Jambo la mapatano.

✍️✍️KUJITAMBUA
Anapenda uondoe marafiki wasio na Faida au Mawasiliano na watu ambao walikuwa wanakutania au unachat nao huwa anawivu pia mfatliaji Sana Na Anataka nawe ujitambue Kama MKE

Yeye hujitambua Kama mme mwema na utembea hivyo.

✍️✍️HUFATA AGANO LA  UCHUMBA
Hurasimisha mahusiano kwa wazazi Tena atakupeleka nyumbani kabisa kwenye chimbuko lake alikokulia Ataweka wazi utajulikana rasmi Sasa na hatazini nawe mpaka akarasmishe mahusiano Yake.

Swala ndoa kwake hufata usione ukafikiri ataishia TU hapo akikupeka nyumbani kwao ujue Amepata uhakika wa kukuoa wewe
Ujue Kuanzia hapo wewe MKE wa Mtu unayetambulika Kama Adamu na Hawa Mungu alivyowabariki Baada ya mahusiano Yao kuyatambua wakaanza maisha ya ndoa nakuanza kuzaa.

Hiyo hatua ya Kufika kukutambulisha MWANAUME huwa mpaka afanye Basi Amejiridhisha Juu Yako.

✍️✍️✍️Na wabariki mliofatilia Hizi ndizo Dalili za Kumjua mme uliyempata Ni mme mwema au SI mwema lakini Anahofu tu na Mungu.

Comment na share katika mafundisho haya

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.