✍️✍️SOMO; PETE YA NDOA

✍️✍️SOMO✍️PETE YA NDOA.

Nawasalimu Watumishi Wa Bwana Katika jina la Yesu Inawezekana ndio Mara ya Kwanza kujiunga Ukurasa huu wa Moto wa Yesu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Nakukaribisha kujua historia ya Pete ya ndoa

Wengi Tunavaa Pete huwa bado hatuelewi Pete ya ndoa ilianzia wapi na kwanini unapofungishwa ndoa unavishwa Pete hususa kwa wakristo wote.

Tufunue Biblia Zetu Tusome;Kutoka;26;29 Luka;15;22-32 Yakobo;2:2-7 Mwanzo;38;18 isaya;3;20-22

✍️✍️Lengo la SoMo;Tujue Pete za ndoa umhimu wake na historia Yake.

✍️✍️DHIMA YETU MOTO WA YESU: Tujue kweli na kweli ituweke huru.

✍️✍️HISTORIA YA PETE YA NDOA✍️✍️

Pete ya ndoa iliazishwa kuvaliwa na Watu wa Agano la kale katika Falme mbalimbali wakati huo Pete ilikuwa ikivaliwa mkononi kumtambulisha mtu Kama Ni mtawala na mwenye Amri juu ya kitu fulani. Pete hii katika Agano jipya Tunaona Anavishwa mwana mpotevu ikiwa ishara ya kumtambulisha Mwanae kuwa Tena kuwa SI Mtoto aliyekosana na Baba Yake kwa upendo baba Anaamua aangize Aletewe Pete ambayo itambulishe upendo alionao baba mfano wa Pete Luka:15;22-32

Pete ilianza kuvaliwa miaka 3000 iliyopita Kutoka Kwenye kuvaliwa Pete na watawala Pete hii ilianza kuvaliwa na wanandoa na hii siyo angizo la Mungu wa Roho MTAKATIFU.

Isipokuwa Ni Mapokeo tuliopokea Kutoka Romani ilianzisha watu wavae Pete ikiwa na Lengo la Kuweka muunganiko kwa ishara ya Pete Kati ya mwanamke na MWANAUME

Tulipokea hivyo nasi Tunatembea katika utaratibu huo Katika Mapokeo hayo Kutoka Romani mpaka makanisa yote ya kikristo ishara Kubwa ya Mtu aliye Kwenye ndoa Ni Pete.

✍️✍️✍️ANGALIZO KWAKO✍️✍️

Sio kwamba upendo wa kweli upo Kwenye Pete hapana upo moyoni.

Sio kwamba mtu akivishwa Pete hatazini Kama mtu anasifa ya kuzini ataendelea tu

Sio Kwamba Pete ndio ndoa hapana ndoa Ni patano lenu Wawili mlilopatana

✍️✍️UMHIMU WA KUVAA PETE ya Ndoa✍️✍️
1;Pete hukujulisha kwa watu Kama wewe unakutana na watu wengi kuwa upo double sio single

2;Huwa inamtambulisha mtu na kumuweka aheshimike kote.

3:Inavuta Usikivu mwa watu ambao utakao ongea nao wakijua umeolewa/Umeoa.

4;Huwa Ni ishara ya upendo usiovunjika au kuvuliwa au kuchokana.

5;Ina nguvu Sana kwa aliyepokea Mapokeo ya kujua Pete haivuliwi.

Unachotakiwa ujue Pete haivuliwi.

✍️✍️PETE YA NDOA INAKOSA NGUVU KWA HAYA.

1;Haina udhibitisho wa maandiko kuwa ukioa au Kuolewa utavishwa Pete.

2;Haina Ukweli kuwa Ni lazima uvae Pete ya ndoa ukioa au Kuolewa.

3:Inampa nafasi Kubwa Mwanadamu na Akili zake na Sio Mungu kwa Sababu Angano la ndoa Ni la Mungu Pete ya ndoa Ni la Mwanadamu

4:Upendo wa moyoni unanguvu kuliko upendo wa kuagalia Pete kidoleni.

5;Pete ya ndoa inamaana endapo Utafundishwa na hutaivua kwakuwa kila Jambo tulilipokea

✍️✍️HITIMISHO✍️✍️
Watu wafundishwe kweli na Wachungaji kabla hawajawafungisha ndoa kutokana imefikia hatua watu wameacha upendo wa moyoni wameanza kutazama Pete na wakizivua Pete zao wanaendelea na uzinzi lakini wakirudi Kwenye majumba Yao wanavaa Pete za ndoa

Wawaeleze Pete ya ndoa haivuliwi ikishavikwa imevikwa Ni Bora usivae Pete TU kuliko mtumishi anaombea Pete unavaa unakuja kulivua Angano lenu Shetani anaanza kutuma watu mwishowe unaanguka nakusaliti ndoa yako.

✍️✍️WITO✍️
Tumia Simu hii kuongea na Pastor Richard Yupo Morogoro veta Dakawa
Mpigie Jioni +255759861768

Comment na share

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.