SOMO: NGUVU YA KUFANIKIWA

✍️✍️SOMO; NGUVU YA MAFANIKIO

Tufunue Biblia Zetu Tusome Matendo;11;29,3Yohana;2;2,Yoshua:1;7

         ✍️✍️UTANGULIZI✍️✍️

NGUVU YA MAFANIKIO ni Hali inayomsukuma mtu kwa bidii na ujasiri nis Yote kufikia Malengo Yake.
Bila mtu kuwa na nguvu ya mafanikio huwa hawezi kuitwa mtu mwenye mafanikio Tunapaswa Sasa Tujue Kwanini Wengine wanafanikiwa halafu kwanini Wengine hawafikii Kusundi lao.

KUNA AINA 2 ZA WATU KATIKA MAFANIKIO.

a.Kundi la Kwanza Ni Watu WENYE UWEZO MDOGO WA KUFIKIRI.
Kundi Hili huwa watu waliojikatia Tamaa na wanamtazsmo wa kuona watu flani flani wenye hadhi flani ndio wanaofanikiwa.

Kufikiri kwao na Nia ya kufanya kazi Hakuna huishi kwa kuaglia mwingine na sio yeye Ukikaa nae anamaneno ya kukatisha Tamaa Anawaza kushindwa tu.

Huwa Wana Dalili Hizi watu Hawa.

1;Wanaongopa maisha
Ukiongopa maisha kila kitu Utashindwa maana ulishaona maisha yamekupinga au huyawezi.

2;Wasiothubutu kufanya.
Wapo watu wamelalia Maono Yao hawathubutu kufanyia kazi wazo Leo.

3;Wasiojasiri Katika Maamuzi
Mtu ambaye sio jasiri huanguka na Kupingwa haraka asisimame

4;Wasio na Nia
Huwa Hawana msukomo wa kujituma.maisha huwataka watu wanaojituma

5;Wasio Hondari.
Hondari huwa mtu asiyechoka inamaana endapo wewe unachoka wakati bado hujafanikiwa. Maisha huwataka watu Hondari

6;Hawaviheshimu.
Usipokiheshimu unachokipata ukipata unauza tu ujue huwezi kukaa na mafanikio Yenye nguvu mafanikio huja kwa kuheshimu Pesa. Nakupunguza marafiki Wasio na Malengo nawe.

Hawa huwa dalili hizi zinawalenga Watu wale fikira zao ndogo katika kufikia Malengo Yao huwa Wanaruhusu haya yawatawale ndio maana hawaendi mbele Ufahamu wao Huwaza hivi nakuamua ivyo.

✍️✍️✍️B.KUNDI LA PILI; WATU WENYE FIKIRA KUBWA(Nguvu ya mafanikio)

Hawa huwa Ni watu wanaosimamia Nia Yao Malengo Yao huwa wapambanaji hawachoki au Kukata tamaa

Hawa watu unajua huwa wanafanikiwa kwa Sababu ndani mwao wanasiri Hizi.

Dalili Zao huwa zipo hivi.

1;Wenye Wazo.
Huwa wanawazo au wanafikiria Nini wafanye hatua Zipi waende wafanye nini. na husimamia Mawazo Yao.

2;Wenye Nia
Huwa ndani mwao wana Nia kweli  wanakusundia kweli wafanye ivyo.

3:Wenye Utayari.
Wapo Tayari kuishi popote na kupambana na kazi yoyote iliyohalali huwa Wapo Tayari.

4;Wenye Ujasiri.
Huwa sio watu wakuongopa maisha wao hukabiliana na mazingira yoyote Yale hawachangui.

5;Wanamcha Mungu.
Huwa watu wanaomcha Mungu katika Roho huwa wana imani na wanaombea Mambo yao.

Hizi ndizo Siri ya Mtu mwenye nguvu ya kufanikiwa

Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.