SOMO: ANGALIA UMRI WAKO NA USICHEZEE MUDA
SOMO: UMRI WAKO USICHEZEE KATIKA MAISHA.
Mithali 14;1 Isaya;58;12
Darasa la Wanandoa
Meal; Pastor Richard
Simu+255759861768
✍️✍️✍️Karibuni Darasa la Wanandoa Tunataka Tuongelee Vijana Ambao umri unazidi kuwatupa mkono hawajui Bado hatima Yao bado Wapo kwa wazazi au Ndugu.
Karibu uone umri wako unaenda nao sawa au Hapana Kisha Comment Ni mhimu kujali muda wako ili usije kuzeeka Unateseka huna kitu chochote.
Karibu ujifunze
Umri🙏20 - 25 = Kama ni kielimu hujafikia malengo yako, sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya, pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.
Umri✍️25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau KAZI RASMI kama umeajiriwa au umejiajiri au una shughuli yeyote ya kukuingizia kipato.
Umri✍️30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja, tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa. Ni vema ukiwa na familia, kwa maana ya kuwa na watoto kama Mungu kakuwezesha.
35 - 40 = Ni wakati kiwanja kiwe kimejengwa na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia. Hapa inabidi upambane sana kuweka misingi.
40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja, kama hukujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki, ni umri wa masahihisho. Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa watoto wapo kwenye level tofauti za elimu, kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.
45 - 50 = Kwa yule ambae hakukosea huko nyuma basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako, kama ni shughuli zako ni kuanza kuwahusisha, huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fursa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 - 40.
50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na kazi zinazotumia nguvu au akili nyingi
60 - 70 = Kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.
70 - 80 = Kula matunda
80 - 100= Umri wa kusubiria mauti
Yote kwa yote, maisha yetu yapo mikononi mwa MUNGU, kumbuka kufanya Ibada wakati wote
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni