Somo; UMEFICHWA Ufahamu wako

✍🏾✍🏾👏🏽SOMO: UMEFICHWA UFAHAMU WAKO USIELEWE KITU 👏🏽🙏🏽🙏🏽

Chukua Biblia Yako kabla sijaendelea Tusome; Hosea;13;14 Habakuki:3;4 Isaya:48;6 Yeremia;16;17 Wakolosai:1;26 Mathayo;10;26

Tafakari kabla ujaendelea mistari Soma Kisha tulia TU kimya Dakika Tano Ufahamu wako unaenda kufunguliwa Biblia uielewe na kuitafakari.

              ✍🏾✍🏾👏🏽 UTANGULIZI 👏🏽🙏🏽🙏🏽
Ushuhuda wa Mtu aliyehesabiwa haki na Mungu Akiwa katika Kufa

Nikiwa Katika Huduma ya kutembea mikoani Mimi Pastor Richard nilifika Tabora wiliya ya NZEGA Taarafa Ya ITOBO nikaifikia familia moja mtu  Mmoja alikuwa mgonjwa Sana  Mungu akawa Amenituma nifike hicho Kijiji Cha Ikindwa Nilipofika pale Sauti ya Mungu ikasema ingia nyumba ile uombe Maji ya kunywa Kisha uendelee na safari nilipoingia ilikuwa Ni nyumba ya wanaomcha Mungu nikapewa Maji nikajitambulisha Naitwa Pastor Richard Hapo MKE wa Yule Mgonjwa akasema Pastor Richard mme wangu anaumwa Sana Sasa Ni Mwezi yupo kitandani TU niliingia chumba alichokuwa Amelazwa Mgonjwa Sauti ya Mungu nikaisikia nimwambie mgonjwa Mungu anamchukua lakini Amesamehewa dhambi zake kwa kuwa Alitoa kiwanja chake kuwa panjegwe Kanisa Ambacho ndugu walinionyesha Kanisa lilikuwa limejengwa Tayari.

Nilipomwambia hivyo nilimuombea nikamwambia Bwana Mtumishi wako nimeuleta Ujumbe huu Kama ulivyosema kweli Baada ya wiki Mungu alimchukua.

Nataka ujifunze kunawakati Mungu Anaweza kukujaribu utoe Kitu lakini kwa kuwa unatamaa na Mali zako na viwanja vyako ukashindwa kutoa Mpaka unakuja Kufa Ufahamu wako ulishafichwa Usielewe msamaha wako upo kwenye kutoa Kile unachosukumwa utoe.

Wapo watu Uponyaji wao upo kwenye Neno TU kwa Kuwa Ufahamu wako UMEFICHWA unakimbilia Kuombewa Tatizo lipo pale pale.

Wapo watu hawaolewi kwa kuwa ili waolewe wanatakiwa wasizini na wayasimamie mahusiano Yao kwakuwa Ufahamu wako UMEFICHWA unaendelea kuzini na mahusiano yako huwezi kuyasimamia yafikie Lengo:

Karibuni wanangu Naitwa Pastor Richard Ndiye ninayekuwasilishia Ujumbe huu Ufungue Ufahamu wako ulipofungwa unaenda TU bila Akili Kuelewa.

Lengo kuu la SOMO; Kuponya watu Ufahamu wao waliofichwa wanaendeshwa na Shetani na maisha yasiyo Yao nao kwa kuwa hawajielewi wamesarenda wawe watumwa katika urithi wao.

WALENGWA WA SOMO: Umri 18-45
SoMo Hili Lika La Vijana Waliokoka na Wapangani wenye Akili timamu wenye Nia ya kubadilika katika maisha Yao.

Mtu aliyefichwa Ufahamu wake asielewe Kitu Ni Mtu AMBAYE anaishi imradi anaiona Siku yake akiamka akipata asipate yeye haendi na muda au majira mazingira watu hajui kujua kwanini yeye peke Yupo Tofauti na wezake wengine wanapinga hatua yeye ndio kwanza anaendelea kukaa

Wanawake wezake wanajishughulisha hiki yeye ndio kwanza Anasema mme wangu kanikataza au Anataka kuajiriwa ofisini Wakati hana ujuzi wa Kitu chochote.

Mabinti wezake wanaolewa Vijana wezake wanaoa Yeye ndio kwanza Anasema Mimi nakula ujana maisha menyewe mafupi.

Wapo watu shinda Ni ufahamu UMEFICHWA ubaki kuwa ngizani ubaki upo TU unajipa matumaini yasiyo na faida.

Hasara Za Ufahamu kufichwa Usielewe Kitu.

1:Utaingia mpaka makanisa yaliyounganishwa kuzimu au yakichawi ukifikiria unatafuta miujiza kumbe unajiongozea matatizo kwa sababu mtu aliyefichwa Ufahamu anachukia Neno la Mungu anafurahia TU umuombee aende.

2;Utaolewa na ndoa yako itayumbishwa yumbishwa mpaka mtakuwa Kila Siku mnagombana na mmeo kwakuwa shemeji atakupa maneno mawifi watakueleza hili marafiki wazazi nao Utajikuta unasikiliza watu nje.

3;Utaendelea Kupata wanaume Waongo wanawake Waongo kwa kuwa Ufahamu wako hujui Kuelewa MKE mwenye wito wa Kuolewa au mme mwenye wito wakutuza familia unajua KUONA mme wa kutelekeza familia asiye na wito wa ndoa nae ndio unaenda kujichanganya hapo

4;Utaingia na KUONA wezako wanavitanda tivi nyumba lakini ukijiangalis wewe huoni Unafanya Nini zaidi ya Kupata mshahara kuuza vitu unaishia kukopa ujue Ufahamu UMEFICHWA usijue

5;Kijana Utaendelea Kubisha Na Kutokufanya kazi nakuishi kwa wazazi siku Zote au Dada yako alipoolewa nawe umeenda kukaa hapohapo
Ujue UMEFICHWA Ufahamu.
Nk

Faida ya Umhimu Ufahamu kufunguliwa.

1:Utaingia MADHABAHU sahihi makanisa sahihi hutapotea

2;Utaolewa na Kuoa MKE au Mme mwenye wito wa kuitwa Baba Bora mama Bora MKE mwema mme mwema.

3;Hutakosea katika Maamuzi yako ufanyapo

4;Utapinga hatua kila ufanyacho

5;Vijana na watu wengine watajifunza Kitu kizuri Kwako katika ndoa yako ilivyo na Amani na upendo.

Naitwa Bishop Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Piga Simu+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.