SOMO; ONDOA FIKIRA Chafu ufunguliwe

✍🏾✍🏾SOMO;ONDOA FIKIRA CHAFU UFUGULIWE
2Wakoritho:2;11,3:14,4;10 na 10:5 Matendo;8;22

Karibuni wanangu Naitwa Pastor Richard SoMo ondoa fikira chafu ufunguliwe
Linalenga SOMO Hili Kukufungua uliyefungwa na fikira chafu au fikira zakujiona wewe mateso sehemu yako.

Fikira Ni Nini??
Fikira Ni Hali ya Mtu kujijengea tabia fulani katika maisha tabia hiyo inaweza kuwa chafu au nzuri. Sasa Chazo chake huitwa fikira yaani mtazamo usiobadilika.

Fikira imegawanyika katika Makundi Mawili.
1;Fikira Yenye Nguvu
2:Fikira isiyo na Nguvu

Fikira Yenye Nguvu
Ni Hali ya Mtu kwenda sabamba na mabadiliko ya nchi na kuwa mwepesi kubadilika Kutoka pale anapoona hapampi Faida kwenda kwenye Faida mfano;
Nataka niwe na biashara kumbwa Huyu mtu anafikiri hivi Sasa anatakiwa Aifanye biashara Yake iwe Kubwa kwa kutofautisha Huduma na Wegine hata kuitangaza
Mfano unauza online uona biashara haiendi hakikisha Unafanya kazi kumbwa kuitangaza tu na kuielezea biashara yako mtandaoni

Hizo moja ya Wewe kuwa na fikira Kubwa Yenye Nguvu mfano unataka Kuolewa Lakini unaona wanaume unapata au WACHUMBA unapata wataka uzini ukizini nao wanakuacha lazima fikira zibadilike uwe ninataka niwe na msimamo huu mpaka ndoa

Mfano wewe unakataliwa tu Ndugu hawakupendi Lazima fikira ikupe kujiuliza kwanini hupendwi na ubadilike au ufanyie kazi palipo na uzaifu

Fikira Yenye Nguvu humpelekea mtu kuwa na nguvu ya kubadilika haraka anapongundua kuwa Mimi matatizo haya yanatokea hapa

Fikira Isiyo na nguvu Ni Hali ya Mtu kutokubadilika kabisa atafanya kosa na ataendelea kukosea tu miaka yote.

Mfano; Mimi sitaki niazishe Biashara ndogondogo wakati huo huna hata mtaji Mkubwa na ujui utapataje.

Au Mtu Anataka aendelee kukaa kwa wazazi harafu anatafuta MKE aoe.

Au mtu Anataka Apate kazi hatafuti yeye anaambia watu TU nitafutieni

Yaani fikira zinatakiwa zibadilike Acha kulemaza fikira zako kufikiri madhaifu madhaifu tu

Mtu kufunguliwa halafu bado fikira uziendeleze kusema Mimi Sitafunguliwa Mimi ninatazo nitakufa na Tatizo.

Ondoa fikira chafu kufikiri kushindwa shindwa Kila kitu acha kufikiri huwezi Kila kitu badilika kwenye fikira ili ufunguliwe Badilisha fikira zako.

Utapata Faida Hizi Ukiondoa fikira chafu

1;Utabadilishwa kitabia na mienendo
2;Utawavutia hata watu wa mataifa wakuinge
3:Utavuka hapo ulipokwama
4;Utamuona Mungu akikujibu haraka
5:Utakuwa mfano kwa Wengine.
6;Utawavuna watu waokoke
7;Imani yako itakuwa Kubwa
8;Utapanga mikakati mikubwa na itafika

HASARA Utakazo zipata Usipoondoa fikira chafu.

1;Tabia yako haitabadilika wala mienendo
2;Hakuna atakayeinga kwako au kukufata
3;Hutamuona Mungu akijibu
4;Imani yako haitakuwa
5;Hutazaa hata mtoto we kiroho
6;Utapanga mikakati itaishia njiani
7;Hutavuka hapo ulipokwama

Fikira zikipingwa na adui hukumaliza Kila kitu Lakini fikira ukazinjega imara Utavuka mengi.

Naitwa Bishop Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.