Somo;Tunza MUUJIZA WAKO UKISHATOKA KWA Pastor Richard Karibu
.⌚⌚SOMO;JUA NJISI YA KUUTUZA MUUJIZA WAKO UNAPOKUWA UMETOKA KUFUNGULIWA MOROGORO VETA DAKAWA⌚⌚
Imeandaliwa na Pastor Richard
👉🏽👉🏽Lengo: SoMo Hili linamsaidia mtu ajue njisi ya kukaa na kulinda Kile alichokipokea muovu asije Tena kumrudisha kwenye Tatizo au Akaanza Kupitia yaleyale aliyofunguliwa pia inamuongoza hata Yule mtu anayekuwa Ameenda kuupata ukombozi au kufunguliwa mbali mfano. umeenda dar umeenda south umeenda Morogoro Sasa ukisharudi hujui uendelee vipi kutunza ulichokipokea hasahasa MUUJIZA WAKO unajikuta Baada ya muda unaanza Kurudi kule kule matatizo yaleyale yanaanza tena.👉🏽👉🏽👉🏽Karibu katika SoMo Hili Biblia inasema👉🏽
👉🏽Zaburi : Mlango 39
1 Nalisema, Nitazitunza njia zanguNisije nikakosa kwa ulimi wangu;Nitajitia lijamu kinywani,Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu
👉🏽👉🏽👉🏽Kama umeamua kuwa Safi nakutoka kwenye matatizo huwa Tunamanisha Kwa Vitendo kubadilika kila kitu 👉🏽👉🏽Vitabu👉🏽👉🏽Luka;10;30-34👉🏽Luka:13;7👉🏽Ufunuo:3;8 1Tim:5:8
Karibuni Wanangu Tujifunze hiki
MUUJIZA Ni Nini?? ni Kupokea au Kutendewa Kitu ulichomuomba Mungu
KUFUNGULIWA Ni NINI? Ni Kutenguliwa au Kunasuliwa Kutoka Kwenye Mitengo walivyokufungafunga katika ufalme wa ngiza au Kunasuliwa Kutoka Kwenye Minyororo mbalimbali uliyofungwa nayo.
Kwanza mtu Ukishajua Nini kilichokuwa kinakufunga na kukutesa huwa hatua yakufunguliwa moja kubwa Sana kujua Walivyokufunga au Chazo Cha Tatizo Nini.
Unapoombewa Unafunguliwa unapokuwa umefunguliwa umefunguliwa huwa Ni kazi Sasa ukishatoka hapo kwenye kufunguliwa mwendelezo wako njisi unavyotakiwa Uishi au Ukaaje ili Tatizo lisirudi Tena au ufanyaje ili Kile Ulichokipokea kuendelea Kudumu maana changamoto wengi wanafunguliwa wanatoka Madhabahu mbalimbali na Hawajui wafanyaje wanapokuwa wamerudi kwenye maeneo Yao wanapoishi.
HATUA YA KWANZA NI WEWE MWENYEWE ULIYEFUNGULIWA KUSHIKA WOKOVU
Hapa namanisha Uokoke Utembee na Imani Ya Yesu Usimamie Imani yako usiaze Kurudi nyuma
Mtu mwenyewe anatakiwa asimamie wokovu alioupata nakuendelea nao hata anapokuwa amerudi nyumbani inatakiwa tafuta makanisa ya wokovu na nenda kwa mchungaji eneo ulipopata mweleze Mimi Nimeokoka Nampenda Yesu Kuanzia Leo nitakuwa nikishiriki ibada hapa hapo watakupa mafundisho ya Kiroho nakukuongoza kiroho Hali hii itakufanya kutunza MUUJIZA WAKO na Utaendeleaa Kutendewa Zaidi na Zaidi wakati huo Madhabahu yako Unakuwà unajua iliyokufungua Na unaendelea kushiriki Kila kitu kwa Baba yako mpaka pale tawi likifika hapo ulipo unarudi nyumbani kwako katika Madhabahu yako.
HATUA YA PILI UTAMBUE NA USIMAME KATIKA MADHABAHU YAKO
Mtu anatakiwa asipasahau nyumbani yaani katika Madhabahu Yake iliyomfungua na Kupokea muujiza wake siku Zote hata atakapokuwa amerudi huko aelewe Madhabahu ya Moto wa Yesu ilimtendea hiki Alifunguliwa Akamuona Mungu minyororo na mizingo Yake ilituliwa huko asisahau Aendelee kusimama tu katika kuona mwendelezo wa Mungu anavyomtendea asiaze kuchaganya Madhabahu zigine au kwenda kuzitolea Zaka katika sehemu isiyo Madhabahu Yake atapoteza muujiza wake inatakiwa Aifanye Madhabahu Yake na Kujenga Madhabahu Yake
Soma;Malaki:3;10
Fungu la kumi ushike kutoa katika Madhabahu yako usiende unatoatoa ovyo
HATUA YA TATU ENDELEA KUFUNDISHWA Neno la Mungu
Mtu anatakiwa afundishwe Neno la Mungu ili Azidi kujua njisi ya kujilinda mwenyewe kiroho na kimwili sababu mtu anashabuliwa Sana kiroho na kimwili kwa hiyo mtu anapokuwa amefundishwa Maombi Kumtumikia Mungu maisha Yake anajirida kimwili na kiroho pia Unajikuta vitu kwako vinafunguliwa kwa Ajili tu ya Wewe Kuwa Upo vizuri katika Habari za Mungu.
Unatakiwa Upende Neno la Mungu Maana maisha yako yatakuwa salama kuliko uzaniavyo.
Mambo Yanayokukuza na Uendelee kujifunza.
KUSHUKURU;
Neno kusema Ansate nikubwa Sana Kwa Mungu Unapoendelea na maisha haya utakapokuwa umeshafuguliwa Utaendeleaa kukutana na changamoto za kawaida zisikutie hofu endelea kumtukuza Mungu na Kusema Ansate Bwana Kwa Kuzidi kunifundisha Imani nakukutengemea wewe katika mapito yangu yote.
Tunaona wale vipofu kumi mmoja alirudi kusema Ansate muujiza ulidumu
KUJITOA;
Kujitoa muda wako na Kutenga muda unatakiwa uwe na muda wa Maombi au ibada wewe na Mungu pia kutoa maisha yako Yawe na Mungu Tu Usiache Maombi kisa Upo busy Tafuta muda wako hata ukiwa umerudi nyumbani omba.
Yule mjane alitoa seti Mia alihesabiwa Bora katika utoaji
KUTUMIKA:
Kutumika kwa Mungu Ni Swala mhimu Sana maisha yako Kumtumikia Mungu haimanishi mpaka uwe mchungaji hapana Tumika na Pesa zako Kama Kujenga kanisa kufangia kupamba kanisa Kununua vyombo ufanyapo haya unajiwekea hadhina kubwa Baadae mbinguni na duniani Usiache kutumika Mtumikie Bwana.
Yule mjane serepta alitumika kumlisha eliya alihesabiwa haki
MAOMBI:
Maombi ni mhimu kwa mtu aliyeokoka na kuendelea kuomba nakusali Ni mhimu tembelea katika vikundi vya Maombi au ibada au mnaweza kuanzisha kikudi Cha Maombi ulipo mnapoendelea na Maombi unazidi kujiwekea ulizi mwenyewe na kutunza adui asikuguse Tena.
JAMBO LA MHIMU UKITOKA HUKU;
Ni wewe Kutafuta kanisa la kiroho nakuendelea kutunza wokovu wako na muujiza ulioupata Morogoro veta Dakawa usirudi ukaendelea Kama ulivyokuwa Mara ya kwanza badilika na simamia Madhabahu ya MOTO wa Yesu hapo ulipo.
Baada ya muda Kanisa la Moto wa Yesu litakufikia kabla Madhabahu yako haijafika hapo unatakiwa unaendelea kulelewa kiroho nauzidi kukua Zaidi
Mambo haya ukiyazingatia utatunza Ushuhuda wako muujiza wako.
Naitwa Bishop Richard Nipo Morogoro veta Dakawa
Simu+255759861768
Kanisa la Moto wa Yesu
Makao makuu Morogoro veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni