SOMO : MAHUSIANO KUJUA MCHUMBA MWENYE MALENGO NAWE
*SOMO: HATUA NZURI ZA KUMJUA MCHUMBA WAKO ALIYE NA LENGO NAWE*
Vitabu vya Biblia tunaongozwa na
Zaburi 119:9
Torati 22:23-28
Mithali 7:7
Muda au Wakati mzuri wa kumjua huyu kweli ni mchumba wangu Hakikisha Uwe Umefata Hatua hizi za Kutunza Uchumba wenu usivunjike Asiwe mtu wa kutaka mzini Kabla ya hatua hizi mabint na wavulana hufikiri kuzini Kabla ya kutabulishana ni nzuri huwa ni dhambi kumbwa ambayo hupelekea mtu asiolewe au kuoa anakuwa anaanzisha mahusiano yake hayadumu
1: *Hatua Ya Kwanza Mtambulishe kwa Marafiki Zako*
Hii huwa mmekaa miezi 4-6 Katika uhusiano bila kuzini na mkiwa mnachunguzana na kujuana mapungufu yenu
2: *Hatua ya Pili Mtafute mtu atakayekuwa anakuongoza na kukushauri mwenye uzoefu wa mahusiano au mchungaji*
Hii huwa mkishafikisha Miezi 6 YA uhusiano wenu au unaweza ukawa na Mlezi wako WA mahusiano utakayemweleza Kila kitu utakayemwamini wewe Bint au Mvulana waweza kumwambia mchungaji au rafiki yako
3: *Hatua Ya Tatu huwa Unatakiwa umweleze mchungaji anayekulea kiroho uliyenaye ambaye ni Baba yako mlezi*
Hii huwa mahusiano yenu yakifikia mienzi nane mpeleke ukamtambulishe kwa mchungaji hii hukusaidia mahusiano yenu kujengwa katika misingi ya kiimani ya kidini na kuongozwa na hofu ya MUNGU
*4:Hatua ya Nne Huwa kwenda KWA Wazazi kutabulishana*
Hii huwa mahusiano yenu Yamefika mwaka na kuendelea BILA kuzini mkishafika huko wazazi ndio huwa wenye maamuzi ya wewe kukupokea au wakakushauri kulingana kuwa Tabia zako wanakujua na walishapitia huko Mengi walishaona huwa ni watu mhimu sana kwenda
*Tatizo lilopo KWA VIJANA*
Wanakimbilia Kuaza kuzini au kutabulishana haraka hasa kwa mabint wengi huwa na pupa za kuwa kama wasiojitambua pasipo kuchunguza kijana mwenyewe Dini yake wewe mkristo Hutakiwi uolewe na mwislam au Mtu asiyemjua MUNGU lazima ndoa yako itakuwa ya mateso na taabu kwa haraka haraka za kuchangua na kumtambulisha utakuwa unajikuta unatambulisha tu vijana Alafu unaachwa Unakuwa umeokoka Lakini Bado Unakuwa unaendeshwa na shetani pasipo kujielewa Binti usikimbilie Kumtambulisha au kuzini Utakuja kujikuta unatelekezwa na watoto kazi huna na hapo ndio utajuta na kukumbuka somo hili
Ansate wewe Uliye kwenye mahusiano na mtu asiyemjua MUNGU mfanye amjue MUNGU
Unayeishi Maisha ya kukurupuka kutambulisha wachumba badilika
Wewe Unayeishi na mtu bila wazazi kujua wafanya dhambi kumbwa sana nendeni mkatambulishane
Naitwa PASTOR RICHARD
Mch.kiogozi WA makanisa YA Holy Spirit
Nipo Morogoro VETA DAKAWA
Tovoti www.mchungajirichardi.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni