SOMO : KUELEWA SIKU AU DALILI ZA KUKUJULISHA Upo Tayari Kupata mimba

*SOMO:NJISI YA KUELEWA SIKU ZA KUPATA MIMBA*

Na Sababu zinazofanya Wanandoa wasizaye haraka kutokujua Elimu hii

Ufunuo:12:2

Isaya 26:17

Ayubu:3:3

YAI KUPEVUKA HUA HATUA YA KWANZA KUIJU

Yai la Mwanamke hupevuka siku 14 kabla ya ya siku ya bleed.
Hii ni siku muhimu sana kwa wana ndoa kuijua. Siku hii yai huwa linakuwa limeshakomaa na tayari limeshatoka katika nyumba yake ya mayai (ovaries) na kuelekea katika mirija ya uzazi (fallopian tube) tayari kukutana na mbegu ya kiume. Na kumbuka mbegu za kiume huishi muda wa masaa angalau 72 kwa hiyo muda wowote ndani ya masaa 72 kabla ya yai kutoka katika ovaries mtwanamke anaweza kudungwa mimba. Mfano kama yai linatoka tarehe 13, basi ukifanya tenbdo la ndoa siku ya tarehe 13,12,11,10 zote unaweza pata mimba - kwa hiyo hizi huitwa siku za mimba (fertile days), tofautisha na siku za hatari ambazo ni kuanzia siku yai limetoka na siku kadhaa baada ya yai kutoka.

*KWA NINI BAADHI YA WANANDOA HUCHELEWA KUTUNGA MIMBA* ?

Kupata mtoto ni majaliwa ya mwenyezi Mungu lakini inaweza pia sababishwa na baadhi ya mambo kama vile yalivyoorodheshwa hapa chini. Hizi ni baadhi ya sababu, ili upate uhakika unatakiwa uende hospitalini na upime.

1- *MAISHA MAFUPI YA YAI LA KIKE* .

Yai likitoka katika nyumba ya mayai na kuelekea mirija ya uzazi hadi kizazi linaweza ishi masaa kuanzia12 hadi 24+. Mfano yai limotoka saa1 asubuhi na wewe ukakutana na mwenza wako saa5 usiku. Ikiwa yai lako linauhai wa masaa12 hilo yai mbegu za kiume zitalikuta limesha pooza. Lakini kama lina uhai wa masaa 20 basi kuna uwezekano mkubwa wa kutunga mimba. Nini cha kufanya kama unahangaika kupata mimba hakikisha unazitumia vizuri siku za uzazi, ikiwezekana fanya tendo la ndoa usiku na asubuhi - amka na BBC. Baadhi ya dawa za tiba mbadala zimeonyesha kuwa na uwezo wa kutibu matatizo ya mayai kutokomaa vizuri

2- *MBEGU ZA KIUME HAFIFU/DHAIFU/CHACHE* .

Mbegu zinaweza kuwa hazina mikia na hazina nguvu na haziwezi kuogelea hadi kuliwahi yai. Mshindo mmoja unaweza kutoa mbegu karibia au zaidi ya milioni40. Mbegu hizo hushindana ili kuliwahi yai, ni ile mbegu bora tu ndio itafika mapema.Kama mbegu ni chache (chini ya milioni 10 kwa mshindo mmoja) basi uwezekano wa kuwa na mbegu bora nyingi unakuwa mdogo.

3- V *IZUIZI KAMA UVIMBEE KWENYE MIRIJA YA UZAZI*

Uvimbe unazuia yai na mbegu za kiume kukutana kirahisi. Uvimbe unaweza jitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa na hali ya hewa au uvimbe tu usiojulikana kama endometriosis

4- *UCHACHU MKALI KWENYE UKE (ASIDI NYINGI* )

uchachu mkubwa unaua mbegu nyingi za kiume, hivyo kupunguza idadi ya mbegu zenye uwezo wa kuliwahi yai.

5- *UCHAFU NDANI YA KIZAZI*

uchafu na ute mzito ndani ya kizazi huzifanya mbegu kushindwa kuogelea na kuwahi kurutubisha yai

6 *- MALANGO WA UZAZI KUTOKUFUNGUKA (CERVIX* ) –

Mlango kati ya uke na mji wa mimba usipofunguka na kuruhusu mbegu kupita inachangia pia kuchelewa kupata ujauzito.

7- *MVURUGIKO WA HOMONI* .

Baadhi ya homoni kutofanya kazi vizuri. Homoni ndio zinaamrisha mwili kufanya kazi zote za uzazi tangu kuamrisha yai litoke, lipasuke na pia lijishikize kwenye mji wa uzazi. Pia homoni ndio zinachochea viamshi vya tendo la ndoa. Kama homoni zimevurugwa basi mambo yako yatavurugika.


*DALILI ZA SIKU ZA UZAZI ZA KUPATA MIMBA*

1- *UTE UTE UKENI* -

Ukikaribia siku zako za uzazi yaani yai ndio linajiandaa kutoka katika mji wa mayai basi kunakuwa na mabadiliko ya ute ukeni, siku za mwanzo kunakuwa na ute mzito, siku ya uzazi (yai limetoka) kunakuwa na ute unaonasa kama utauvuta unavutika na siku zinazofuata baada ya yai kutoka ute unakuwepo lakini unakuwa mgumu kama mtindi.

2- J *OTO KUONGEZEKA* Mwilini -

Joto la mwili linaweza ongezeka kuanzia siku kabla yai halijatoka na linakuwa juu zaidi siku yai limetoka. Kama unapima joto pima asubuhi kabla hujaamka kitandani.

3- *MLANGO WA UZAZI KUWA LAINI* –

Mlango wa uzazi upo kati ya nyumba ya uzazi na uke. Mlango huu kawaida huwa mgumu kama pua, lakini siku yai likitoka unakuwa mlaini kama shavu au lips na pia hupanuka kidogo na kusogea zaidi kwenye uke. Wakati huu pia mlango huu huwa ni rahisi kufunguka.

4- *HAMU YA TENDO LA NDOA KUONGEZEKA* –

Wanawake wengi katika siku hizi huwa wachangamfu sana kwa tendo la ndoa. Mwanaume inatakiwa uwe mwelewa pindi mwenzio anapokusogelea uchangamke mana ukizubaa unapoteza ramani ya uzazi.

5- *MAZIWA KUWA*
*MAZIWA KUWA LAINI* .
*
Hii huwa dalili Moja wapo za kukujulisha upo kwenye wakati wa kushika mimba

6- *UWEZO WA KUNUSA VITU VINGI HUONGEZEKA* –

Wanawake wengi huwa na uwezo mkubwa wa kunusa na kuelewa harufu za vitu vingi sana wakati wakiwa period.

7- *MAUMIVU UPANDE MMOJA WA KIUNO* –

wengine pia hupata maumivu upande mmoja wa tumbo la uzazi. Kama dalili hii itaambatana na dalili zingine hapo juu na pia inaangukia siku ambayo umeikadiria ndiyo ya uzazi basi una uhakika hiyo ni ndio siku yenyewe

. 8- Kuna dalili nyingine nyingi lakini si za jumla kwa watu wengi zinakuwa kwa watu wachache wachache kama kuumwa kichwa na kujisikia vibaya katika mwili wake



Naitwa PASTOR RICHARD

Nipo Morogoro VETA DAKAWA

Tovoti

Www.mchungajirichardi.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.