SOMO: CHANZO CHA MATATIZO
👆🏽👆🏽✔ *SOMO: CHANZO CHA MATATIZO KWA MWANADAMU*
Yakobo:1:2-4
2Koritho:1:3-7
8-10
KUNA MAMBO YANAYO MFANYA MTU ATESEKE AU APITIE MATATIZO Ambayo humfanya mtu aishi kwa Shida na Matatizo Mbalimbali karibu ufuguliwe katika somo hili
Lengo la SOMO : Uelewe NJISI yakutoka kwenye Tatizo lako au Umsaidie mwenye Matatizo
*KABLA SIJAENDELEA KUNA Jambo ambalo lazima uelewe mtu alianza kuteseka pale tu Adamu na Hawa waliambiwa wawe waagalifu wanaweza kutumia miti yote Lakini wasitumie mti wa miujiza na mabaya na Mema. LAKINI HAWAKUWEZA KUTII AU KUZINGATIA*
KWANINI mtu huwa mgumu sana kwenye kushika anachoelekezwa chenye kuokoa maisha yake hii huwa sababu ya kuteseka
*Mwanzo:1:31 mwanzo 3*
*1:MATOKEO YA DHAMBI*
Hii huwa sababu inayomfanya mtu atende dhambi na akishatenda ile dhambi humfanya ajute na kupitia katika chagamoto mbalimbali na kumpelekea mtu Awe chazo cha mateso
Mambo hayo huwa ni
Pamoja ya dhambi Adamu na Hawa
Dhambi za watu
Mfano Madawa ya kulevya Ulevi Uzinzi usherati wizi ujambazi nk
Hizi ni baadhi ya dhambi zinazofanya uteseke kama uzinzi uashereti Ulevi wizi nk
*2:MATATIZO YALIYO NJE YETU*
Hali hii huwa ni Matatizo tusiyoweza kuyazuia wala kuyadhibiti
*MAMBO HAYO NI* :-
1:Matatizo Yaletwayo na Watu
Kuna Matatizo yanayosababishwa tu Na Wanadamu wezetu kama vile
a. Vita hii huleta madhara Mengi kama vifo njaa uharibifu nk
Nchi kwa nchi zinapopingana huwa chazo cha tatizo ni la wachache wasio na Mapenzi na nchi yake.
b. UJAMBAZI: jambazi huwa mtu asiye na Huruma huleta madhara makubwa ulemavu Husababishwa na majabazi
Haya Ni baadhi ya Matatizo ya watu
2: *MISIBA YA KIMAUMBILE*
Kuna Matatizo mengine huletwa na Mazingira maumbile ya dunia Mambo hayo ni :-
1:Matetemeko ya ardhi:
Haya huwa hatari sana Maana huua wengi Husababisha ulemavu kuharibu makazi uyatima ujane
2:KIFO
Kifo ni janga liliingia duniani kwenye aguko la njia Adamu na Hawa: Huwa halizuuliki
3:Hali ya Hewa
Hii huwa ukosefu wa Mvua Hali hii huleta njaa na vifo
*3:MATOKEO YA UCHANGUZI WETU*
HII HUWA MATATIZO YALETWAYO NA SISI WENYEWE KUKOSEA KUCHANGUA hali hii ukikosea kuchangua mtu hutoseka.
Mfano katika mahusiano ndoa nk
Watu wengi waliokosea kwenye uchumba kuchangua huteseka
waliokosea pia kwenye ndoa kuchangua huwa wakishaolewa ndoa zao huwa Kila siku za majuto huzuni kulia kutokuelewana ndani.
Hali hii Huwakilisha *UCHANGUZI* wao haukuwa wa kuzingatia Vigenzo vya mke Mwema au mme Mwema atakayewafaa.
Lakini Leo wapo wanaofurahia mahusiano yao kwa kuwa wamechangua sahihi uchanguzi wao
Kuna wengine ndoa zao zimetawaliwa na Upendo na Amani wanafurahia wake zao waume zao kwa kuwa wamechangua uchanguzi sahihi.
*Huu HUITWA UCHANGUZI MZURI*
*4:MATENDO YA MUNGU KWA AJILI YETU*
Kuna Matatizo ambayo hurusiwa na Mungu tuyapitie Mambo hayo ni dhiki mbalimbali
*KUTUPITISHA HAYA LENGO LA MUNGU HUWA NI HAYA:-*
1: Kutusafisha na Kutuhakikisha Imani
Yakobo:1:2-4
Matatizo au Mapito Mengine huwa ni Mpango wa Mungu ili atuimarishe kiimani na Tukue kiroho. Mtu huyu akivumilia Shida hizo mapito hayo MUNGU hujikuza.
*2:KUUMBA UPYA UTU WETU WA NDANI*
Majaribu au Mapito yetu tukiyashinda hutufanya tuwe wa wakristo kweli kweli pale tunaposimama bila kumuacha kristo huwa tunainuliwa na Kupokea Majibu yetu.
2Wakoritho.4:8-17
3:KUTUPITISHA KATIKA DHIKI NA KUTUSHINDIA. KUWASAINDIA WENGINE
Tunapopitia katika Shida mbalimbali MUNGU hulenga kutusaidia tuwe walimu kwa wengine wenye Shida kama hizo
2wakoritho.1:3-7
*4:KUTUFUNDISHA KUMTENGEMEA MUNGU*
Matatizo hutufundisha kumtengemea MUNGU :
Tunapokutana na matatizo tukashindwa kuyatatua au mpito fulani humfanya mtu amtengemee MUNGU Na anapomtengemea MUNGU humjibu na hali hii humfanya mtu amtengemee MUNGU kwa kuwa Tayari anakuwa ameshajuwa Uweza wa MUNGU.
Tunapopitia Mapito tuliomwamini kristo na kumtengemea MUNGU hutushindia katika majaribu yetu.
2Koritho:1:8-10
*HAYA Ni MAMBO YANAYO SABABISHA MATATIZO UPITIE*
Naitwa PASTOR RICHARD
Mch.kiogozi WA makanisa YA Holy Spirit
Makao makuu Morogoro VETA DAKAWA
Simu +255759861768
Tovoti
www.mchungajirichardi.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni