MAOMBI YA KUOMBA KABLA HUJALALA
MAOMBI YA KUOMBA WAKATI UKIWA UNALALA
Neno la Usiku (Zaburi 121:3-4)
"Asiuache mguu wako usogezwe; Akulindaye asisinzie. Tazama, Yeye alindaye Israeli hasisinzii wala halali usingizi."
Maombi ya Usiku
1. Shukrani
"Mungu Baba, asante kwa neema yako iliyoniongoza siku ya leo. Asante kwa pumzi ya uhai na kwa ulinzi wako katika kila hatua niliyopiga. Nakushukuru kwa riziki, afya, na kwa kuniepusha na mabaya yaliyokuwa wazi na yale ya siri."Katika Jina la Yesu.Ameen ×3
2. Toba
"Naomba unisamehe kwa yote niliyokukosea leo, iwe kwa mawazo, maneno, au matendo. Takasa moyo wangu na unipe roho ya unyenyekevu na upendo kwa wengine. Katika Jina la Yesu. Ameen×3
3. Ulinzi na Amani
"Baba, nikienda kulala sasa, naomba malaika wako wa ulinzi wakazunguke nyumba yangu na familia yangu. Ondoa kila hofu, wasiwasi, au mashaka ya kesho. Funika usingizi wangu kwa damu yako takatifu; niamushe nikiwa na nguvu mpya na tumaini jipya la kuendelea na majukumu yangu Katika Jina la Yesu. Ameen×4
4. Kukabidhi Kesho
"Ninakabidhi mipango yangu ya kesho mbele zako. Ikawe siku ya mafanikio, amani, na utukufu kwa jina lako la Yesu. Amen×2
Lala kwa amani, ukijua kuwa ulinzi wa Mungu haushindwi kamwe. Mungu Ameangiza Malaika
Maoni
Chapisha Maoni