SOMO:TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA
SOMO: TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA WENU
Mwalimu: Pastor Richard (Mwalimu wa Wanandoa)
Mahali: Morogoro Veta Dakawa
Mawasiliano: WhatsApp +255 710889892
UTANGULIZI
Karibu katika nakala hii inayoenda kukupa mwanga katika kuendesha uchumba, hasa kwa vijana wetu ambao wapo kwenye mahusiano. Mahusiano mengi yanavunjika na kutokufikia malengo kwa sababu ya ukosefu wa elimu. Nakuandalia mwongozo huu ili kukuwezesha kufikia ndoa yenye baraka na heshima.
Maana ya Utaratibu:
Ni makusudi au mpangilio mzuri wa kulifanya jambo liwe katika ubora wa kuonekana vyema.
TARATIBU 10 ZA KIFUATWA KIBIBLIA
1. Mruhusuni Mungu Ajenge Uchumba Wenu
Mnapaswa kuendesha uchumba wenu kwa kutumia akili za Kimungu na siyo za kwenu tu.
- Andiko: Zaburi 127:1
- Mfumo: Uchumba wenu uwe kama
- Pembe Tatu (Triangle). Juu muwekeni Mungu, kulia mchumba mmoja, na kushoto mwingine. Msikaribiane sana kimwili kabla ya wakati; mkikaa mbali na dhambi huku mkimsogelea Mungu, mtakuwa na hofu ya dhambi na kuepuka uzinzi.
2. Rasismiheni Uchumba kwa Wazazi
Uchumba wenu usiwe wa uchochoroni au gizani. Hakikisheni mnaenda kwa wazazi kujitambulisha mapema.
- Andiko: Mwanzo 4:9
- Onyo kwa Mabinti: Usikubali kwenda kuishi (kujiolesha) kwa mwanaume ambaye hajakutolea mahari. Jitambue kuwa wewe ni wa thamani.
- Onyo kwa Vijana: Mwepuke binti anayekimbilia uzinzi au kutaka kuzaa kabla ya ndoa.
3. Jichanganyeni na Jamii
Msipende kujitenga kila mnapoonekana.
- Andiko: Mwanzo 24:19-21
- Ushauri: Shirikianeni na watu wengine katika shughuli za kijamii na kikundi. Kujitenga wawili-wawili kila saa huleta maswali na kuondoa ushuhuda mzuri mbele ya jamii.
4. Lindeni Ushuhuda Wenu
Mnakumbuka kuwa mnaheshimika katika jamii na ninyi ni watoto wa Mungu.
- Andiko: Mithali 22:1
-
Mazingira ya Kuepuka:
- Kukaa gizani wawili peke yenu.
- Kukaa chumba kimoja wawili peke yenu.
- Mazingira yoyote tatanishi.
- Kukeni sehemu za wazi ili Mungu asitukanwe kwa sababu ya mwenendo wenu.
5. Msiwashane Moto wa Mapenzi
Msianze kupeana vishawishi au mazungumzo yanayochochea tamaa za kimwili.
- Andiko: Wimbo ulio Bora 8:7, 2:7
- Wachumba wengi hushindwa kufikia ndoa kwa sababu ya kuchokana mapema baada ya kuingia kwenye mtego wa tamaa.
6. Wekaneni Wazi (Ukweli na Uwazi)
Uchumba ni wakati wa kutengeneza msingi wa ndoa. Msidanganyane.
- Andiko: Waefeso 4:25
- Mambo ya kuweka wazi: Mahusiano ya nyuma, tabia unazopenda/usizopenda, matatizo ya kiafya, kazi, umri, na uvaaji.
7. Malizeni Tofauti Zenu
Usitoe nafasi kwa adui kuvunja uchumba wenu kupitia migogoro.
- Andiko: Mathayo 6:14-15
- Jifunzeni kusameheana na kupatana kwa upendo. Mkivumiliana kwenye uchumba, mtaweza kuvumiliana kwenye ndoa.
8. Chagueni Walezi Wenye Hekima
Tafuteni wanandoa ambao ndoa zao ni mfano wa kuigwa ili wawe walezi wenu.
- Andiko: Mithali 11:14
- Walezi hawa watawasaidia kutatua migogoro na kuwapa busara ya kufika kwenye ndoa salama.
9. Tumieni Kinywa Kujenga
Kuna maneno matano (5) muhimu ya kutumia:
"Nakupenda Sana": Ina nguvu kubwa kwa mpendwa wako.
"Samahani Sana": Omba msamaha kwa upole unapokosea.
"Asante Sana": Onyesha shukrani kwa kila jambo, hata liwe dogo.
"Uvumilivu": Onesha uvumilivu wakati wa changamoto (kama kukosa kazi).
"Kujaliana": Onesha kujali anapoumwa au anapopitia magumu.
10. Anza Uchumba Ukiwa Tayari kwa Ndoa
Usianzishe uchumba ili mradi tu uonekane una mtu.
- Andiko: Mithali 3:1
- Lengo kuu liwe ni kuoa au kuolewa kwa heshima. Hii inamletea Mungu heshima na wazazi wenu pia.
HITIMISHO
Unapofuata taratibu hizi, unaleta heshima kwa Mungu na wazazi wako. Nakukaribisha Morogoro Veta Dakawa kwa mafundisho zaidi yatakayofungua ufahamu wako.
Wito
Penda kujifunza zaidi; mafundisho yanakufungua ufahamu kuliko maombi pekee.
Maoni
Chapisha Maoni