SOMO:SIRI YA FUNGU LA KUMI

SOMO:SIRI ZA USHINDI WA FUNGU LA KUMI
UNAPOLITOA KWA UAMINIFU. 

Ni Utaratibu Wa Madhabahu hii Kukufundisha uelewe kitu katika Uaminifu Wa Zaka.

Hapa nimeandika Point Muhimu tu Uzijue

​1. MAANA NA KIWANGO CHA ZAKA

​UFAFANUZI 
Zaka ni 10% ya mapato yako yote kabla ya makato yoyote ya kazi yako unayoifanya (kama kodi, bima, au madeni).


​KUSUNDI:Ni agizo la Mungu lililowekwa kwa ajili ya ulinzi wa kazi na mapato yako Unayoyafanya
Malaki:3:8-12


​ 2. KANUNI YA MADHABAHU

 1:MOJA NI ​UAMINIFU WAKO KWA MUNGU: 

Fungu la kumi linapaswa kutolewa kwenye madhabahu inayokulea kiroho na unayoshirikisha maombi yako.
​Utambuzi: Ili madhabahu ikutambue na kukujibu, lazima uwe mwaminifu katika utoaji wako mahali hapo.


​### 3. MASHUJAA WA IMANI KATIKA UTOAJI

Shujaa

✍🏾Tendo la Uaminifu

✍🏾Matokeo ya Kiroho

Konelio✍🏾


Alitoa zaka kwa ✍🏾  uaminifu na kufundisha familia yake.

Mungu alisikia na kujibu maombi yake (Matendo 10:1-6).

Tabita✍🏾

Alitoa zaka kwa✍🏾 uaminifu licha ya kuwa na uchumi wa chini.

  Mungu alimkumbuka na kumfufua kutoka kwa wafu (Matendo 9:34-38).


 Ibrahim ✍🏾Alimtolea Mungu✍🏾 zaka kabla hata ya kupokea majibu.



4:MWONGONZO WA KUTOA  FUNGU LA KUMI KATIKA MADHABAHU HII YA HOLY SPIRIT CHURCH



Mwongozo wa Mahesabu ya Fungu la Kumi (Zaka)

​1. Kwa Wafanyakazi (Mshahara)

​Zaka inapigiwa hesabu kwenye mshahara  ( Salary) kabla ya makato yoyote ya kibenki, bima, au mifuko ya jamii au mikopo nk


  • Mfano 1: Ikiwa mshahara wako ni 1,000,000 lakini unashika mkononi 700,000 baada ya makato, zaka yako ni 100,000.

  • Mfano 2: Ikiwa mshahara wako ni 800,000 lakini unadaiwa benki na unashika mkononi 400,000, zaka yako bado ni 80,000.

​2. Kwa Wafanyabiashara


​Unatakiwa kuandika mauzo yako kila siku kuanzia tarehe 1 mpaka tarehe 30 ya mwezi ili kupata jumla kuu.

  • Hatua: Chukua jumla ya mauzo yote ya mwezi mzima.

  • Mfano: Ikiwa jumla ya mauzo ni 500,000, utatoa 50,000 kama fungu la kumi kwa ajili ya kuombea biashara yako iongezeke.

  • Kidokezo: Hata kama ulizungusha mtaji na huna pesa mkononi inapofika mwisho wa mwezi, unapaswa kutafuta fungu la kumi kulingana na mauzo uliyofanya.

​3. Kwa Wakulima


​Mkulima anatoa fungu la kumi pale anapovuna mazao yake shambani.

  • Mfano wa Magunia: Ukivuna magunia 10, gunia 1 ni la Mungu.

  • Mfano wa Vipimo: Hata kama ni debe na nusu, mpe Mungu sehemu yake ili uone mazao yakifunguka zaidi.

​4. Kwa Wasio na Kazi (Utoaji wa Mwili)


​Ikiwa huna kipato cha fedha kwa sasa, Bishop Richard anafundisha kujitoa kwa njia nyingine:


  • Huduma: Kujitoa mwili wako kuhubiri injili au kuvuna watu.

  • Usafi: Kwenda kufanya usafi kanisani kila wiki kama ishara ya kujitoa kwako.

FAIDA YA TUNAPOTOA FUNGU LA KUMI


​1. Afya ya Kiroho na Kimwili

Yeremia:30;17
  • ​Mtoa zaka mwaminifu anatetewa na Mungu dhidi ya magonjwa yanayoweza kuteketeza fedha zake.

  • ​Inajenga ukomavu wa kiroho, kwani huwezi kuwa mwaminifu katika utoaji kama huna imani au ufahamu wa kumjua Mungu wako.

  • ​Baraka za Mungu humjilia na kumfikia yule anayeisikia sauti ya Bwana kupitia utoaji.

​2. Ustawi wa Familia na Uzao

Kutoka:23:26
  • ​Mungu anaahidi kuibariki familia ya mtoaji, ikijumuisha kupata mke au mume.

  • ​Inaleta wingi wa uheri katika uzao wa tumbo lako, mifugo, na mazao ya nchi yako.

  • ​Mungu anakuweka kuwa taifa takatifu unaposhika maagizo yake ya utoaji.

​3. Mafanikio ya Kiuchumi

Mithali:16;3
  • ​Uchumi wa mtoaji unasimamiwa na Bwana, na milango ya baraka inafunguka kwa kiasi kikubwa.

  • ​Mungu anafungua hazina zake nzuri za mbinguni ili kutoa mvua ya baraka kwa kazi za mikono yako.

  • ​Mtoaji anafanywa kuwa "kichwa wala si mkia," akipata uwezo wa kukopesha mataifa mengine badala ya kukopa.

  • ​Kazi na mawazo ya mtoaji yanathibitika mbele za Bwana


OMBA HIVI UNAPOTUMA FUNGU LA KUMI


Kuupitia Fungu la Kumi la mwezi huu, ninalitoa katika madhabahu hii ya Moto wa Yesu, ninaomba likaongee na likanene kwa habari ya mimi: Nijenge nyumba yangu, madai yangu niliyokatwa kimakosa nikalipwe tena haraka, na mchumba wangu akatoe mahari nyumbani na tufunge ndoa haraka. Naomba uipokee kwenye madhabahu yako ya mbinguni na ipate kibali na majibu nikayaone katika Jina la Yesu. Amen."

​📲 Namba za Kutuma (Richard Julius Kushoka)

​Ili kukamilisha utoaji wako, tumia namba hizi zilizotolewa hapa chini Jina Litatokea  Richard Julius Kushoka

  • M-PESA: 0759861768.

  • TIGO PESA: 0710889892

  • HALO PESA: 0628355985

  • CRDB BANK: 0152361572400

 








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO