Somo:AGANO LA DHABIHU

SOMO: AGANO LA DHABIHU

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Tar. 3-1-2026

Rejea Kitabu. 
ZABURI;50 soma yote


Kutambua Agano la Sadaka yaitaji ufahamu mkubwa Wa Ki Mungu Watu Wengi Wanaishi nje ya Agano la Sadaka ndiyo maana Huwa wanamuona Mungu Kama Ananjaa au Wanawapa wachungaji na Hata akiwa Anasali kanisa limepasuka Ukuta na kwake kukawa kumepasuka ataanza kuziba UFA Wa nyumbani kwake. 

AGANO LA DHABIHU ni Patano lako na Mungu wako Katika Kujitoa Sadaka Kama vile. 
Malimbuko, Fungu la Kumi, Thamani, Shukurani, Nadhiri,Kujenga Madhabahu, Kuteketezwa Nk. 

HAPA unatakiwa Utoe Sadaka Mwenyewe Kwa Moyo usiokuwa Wa kulazimishwa Sasa Mpaka ufikie hicho kiwango Ujue   Moyo Wako Umepatana Na Mungu Kuona Umhimu Wa uhusiano wako uliopo Wa Sadaka na Mungu Kama hicho Kiwango hujafikia HUWEZI kuwa Mwaminifu Hata iweje AKILI Yako inawaza changamoto haioni Madhara IPO Mbele ikatolee Sadaka miungu Kuliko kuigusa Madhabahu ya Mungu kwa Sadaka 

SABABU ZA KUKOSA AGANO LA SADAKA

1:Mioyo yetu ipo mbali na Neno Kujifunza Tunataka Shortcut Nije uniombee niendelee na Mambo Yangu utaijuaje nguvu ya Sadaka si utaitoa tu Kama Desturi Siyo umeilewa.  Mfano wapo Watu wamekuta wazazi wanaotoaga Fungu la Kumi naye analitoa lakini Hana Elimu na Fungu hilo la Kumi. 

2:Kujifanya Tunajua na Tuko bize Inakufanya maombo ambayo yanakupa Uzima Wa Milele Kupuuza na Kushikilia Mambo yasiyoelimisha. 

3:Kukosa Masomo na Mafundisho Yanayotupa ufahamu Wa kuelewa VITU Mbalimbali vya Kiroho na Mwili. 

4:Madhabahu Zinazotuhudumia Zinakuwa Hazitujengi Kuelewa nguvu na Uwezo Mkubwa Wa Sadaka.


UMHIMU WA AGANO LA SADAKA

1:Utakuwa Mtoto Wa Mungu uliye hai Kiroho umekomaa. 

2:Utamfanya Mungu Ashughulike Yaani ipo hivi Sadaka Yako inavyotolewa inaweza kwa wakati huo Isitende lakini usifikiri haitaleta matokeo Wewe nikusubiri kwa Mungu. 

3;Baraka Mbalimbali Huvutwa na Sadaka

Mungu Anasema VITU vyote ni vyake kwa Hiyo unapomtolea Unamrudishia aliyekupa Hiyo KAZI Pesa Usitoe Kitu Umuone Mchungaji Au uone dhehebu Utoe na Umuone Mungu. 

Tupitie hii mistari Tujifunze Kitu 2026 Anza na Agano la Uaminifu Wa Sadaka Mbalimbali. 

Zaburi 50:12-17 

12:Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo.

 13:Je! Nile nyama ya mafahali! Au ninywe damu ya mbuzi!


 14;Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.


 15:Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.


 16:Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, 
Na kuliweka agano langu kinywani mwako?

 17:Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

TUNAFANYA NINI SASA
==≠{{{{{{========={{{

UKIYASOMA HAYA MAANDIKO Mungu anakuonyesha Kukuambia Utoe Dhabihu Siyo kuwa Yeye Ananjaa hapana anakutambua Wewe Mtu wake na Amekupa kilicho chake Kukupima Na Kuutazama Uaminifu Wako Kwake. 

Kuna Wakati Mungu Matengemeo yake alijua utakuwa na Agano na Sadaka Hautakuwa Mtoto msumbufu kwa Hiyo anapokuona vile Unampa maswali haya ajiulize. 

Basi Tuweke Agano la Dhabihu Tuwe Waaminifu kulitunza Agano letu na Mungu VITU VINGI Vitafunguka vyenyewe Tu. 

WITO WANGU

Nikukaribishe 2026 Tukatae Kuwa Watoto Wa Sumbufu Tukubali Kubadilika Mungu Anataka Tujifunze Tumjue Yeye Siyo Tuvijue alivyoviumba Tumjue Sana Yeye Mwenyewe Mungu ndiyo Tutakuwa na Baraka Mbalimbali. 


WASILIANA NAMI MWENYEWE PASTOR RICHARD
WhatsApp +255710889892

Piga Simu kawaida 0759861768


Share kwa unaotaka wajifunze kitu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO