SOMO:AINA ZA MABUSU NA MAANA ZAKE

           "DARASA LA UCHUMBA"
======={{{{{====={{{{{{{==========
SOMO: AINA ZA MABUSU (KISS) NA MAANA ZAKE. 

Mabusu Yalianza Toka Kipindi cha Adam
Na Eva Vitabu vinaelezea Busu ni Hisia ya Upendo

Rejea Vitabu.Mwanzo;27;26-27  2Samweli:20:9
Mithali;7;13 Wimbo:1:2


Mabusu huwa ishara ya upendo na heshima kubwa mno siyo kila busu utakalopewa linamaana moja kuna busu mtu akikubusu linaongea kwa habari ya kuhitaji Penzi lako jingine la kuonesha anakujali mno lakini anaongopa Jigine LA upendo tu Ni Vizuri kujua na ukaweza kutofautisha means kila Busu linaongea juu ya hisia Kali za Upendo Kati yenu wawili. 

Naitwa Pastor Richard wa Morogoro
Kutoka Kanisa LA Moto wa Yesu
Karibu Ujifunze nami


1.BUSU LA KWENYE PAJI LA USO. 

Busu hili maana yake nakujali nakupenda, na nakuthamini, ila hutumika kirafiki kindungu au hata kwa wapenzi pia.

JINSI YA KULITUMIA

Utambusu mtu kwenye paji lake la USO kuonesha Unampenda na Kumjali

Litumie kubusu mtu wa karibu ndugu mototo mzazi rafiki unaowajali. 


2.BUSU LA KWENYE SHAVU. 

Hutumika kwa watu wote, ndugu, marafiki hata wapenzi pia, ni ishara ya upendo kwa mtu wako wa karibu.

JINSI YA KULITUMIA BUSU HILI. 

Mbusu mtu kwenye shavu lake kuonesha Upendo wa Kawainda wa Kindugu 

Litumie kwa  watu wote hii inaongea Upendo wa Kindugu. 

3.BUSU LA MDOMONI

Linaweza kutumika kwa wapenzi, marafiki hata wazazi ni busu kavu lisilo husisha ulimi, ni ishara ya mapenzi mazito na heshima kwa yule mtu.

JINSI YA KULITUMIA BUSU HILI. 
Unatakiwa umbusu kwa mdomo wote wawili mkutanishe mdomo ukiwa mkavu mbusu mtu kwa ajili ya kuonesha Umempenda Sana. 

Litumie Kwa Mtu umpendaye kimahusiano na unamheshimu mno.

4.BUSU LA MDOMO NA ULIMI.

Busu hili huusisha ulimi na ulimi baina ya watu wawili hutumika zaidi kwa wanandoa, huitwa deep kiss 

JINSI YA KULITUMIA BUSU HILI

Busu hili mbusu mmeo au mkeo anayekubusu anakuwa anakuambia anaomba Tendo la ndoa mfanye hii huusisha mdomo na ulimi Kati ya hawa watu wawili Hali Ambayo huimbua Hisia za Kimahamba. 

Litumie kwa mweza wako mkiwa faragha wawili

5.BUSU LA SHINGONI. 

Ni busu la kuomba kitu zaidi, yaani anaekupa busu la shingo ni mtu anaekupenda. 
JINSI YA KULITUMIA BUSU HILI

Simama nyuma ya mweza wako mbusu shingoni linakuwa linamanisha mtu anaitaiji Tendo La ndoa anahisia nawewe za  Penzi lako

Litumie kwa mweza wako

6.BUSU LA SIKIO.

Linaweza kuanzia kwenye mdomo, likahamia shingoni hadi sikioni hii pia ni aina ya busu baina ya wanandoa

JINSI Ya KULITUMIA BUSU HILI

Anza kumsongelea mweza wako Anza kumbusu mdomoni taratibu shuka kwenye sikio hamia shingoni hili busu ni kwa Wanandoa tu. 

Litumie Kwa Mweza wako mkiwa wawili Tu 

7.BUSU LA BENGA

Busu hili halina tofauti sana na busu la shingo, ni ishara ya kuhitaji zaidi kutoka kwa meanandoa

JINSI YA KULITUMIA BUSU HILI

Nikama nilivyoelekeza ya sita hili huwa BUSU LA wanandoa kuhitaji Tendo LA ndoa. 


MABUSU Huongea Kwa hiyo mtu anaweza akaongea nawewe kupitia Busu halafu usimwelewe kumbe mwezako anakuambia kitu hasa kwa wanandoa ndani ya ndoa. 

Watu wengi mabusu huchukulia kama Kawainda lakini yanaongea kwa habari ya Upendo wa Juu Sana Hisia Kali Sana. 

Jifunze Kila Mara kuongea na mweza wako kwa mabusu mfundishe ajue. 

Share SOMO hili. 

Limeandaliwa Na Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richard Wa Morogoro

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO