SOMO: NGUVU YA MTAZAMO INAVYOBADILISHa

SOMO; NGUVU YA MTAZAMO UNAVYOBADILISHA MAISHA YAKO. 

Rejea
Vitabu: Mithali:15:29-33.  1Wakoritho:9:7-10  2Wakoritho.5:16

UTANGULIZI:-
Ni mhimu Kujifunza Hili Somo kwa Sababu Watu Wengi Wanaishi kwa mitazamo yao na huo mtazamo huwapa nguvu ya kuyapa majina majira mbalimbali na kuishi kulingana na hayo majira walivyoyapa Majina.

Mfano; Bint Anapitia kipindi cha kupata wachumba na kuachwa Mtazamo akilini utakuja Amefungwa na nguvu za ngiza Ataanza kuishi ndani ya huo Mtazamo mpaka apate mtu amtoe katika huo mtazamo atapokea mtazamo wa kuolewa.

Mtu Amekuwa Akiitwa kazini anaishia Itaview Haitwi Mtazamo utakuja Wanaoitwa kazini wana watu wakubwa hilo ni Jina la mtazamo wake mwenyewe. 

Mtoto Wa Mungu Ninayekuletea Hili Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro Lengo Ujifungue Kamba ya Mtazamo iliyokufunga.


MTAZAMO NI NINI..? 
Mtazamo ni Picha na Muonekano wa Majira unayo yapitia namna unavyoweza kuyaita majina..?

Mfano; Mambo yanaenda vibaya kila kitu hakiendi Utakiita hicho kipindi kigumu.
Huo ndio mtazamo utakaouishi.

Umepima ukaambiwa unauvimbe kwenye kizazi Mtazomo utakuja hutazaa tena na utaita huwezi kuzaa kwa sababu Daktari alikuambia Unauvimbe.

TAFAKARI UELEWE NINACHOKIMANISHA HATA MAISHA UNAYOYAISHI YANATOKANA NA MTAZAMO. 

MTAZAMO: Unaweza Kubadili Maisha yako au Kuyafanya yabaki yalivyo hivyo hivyo.


MTAZAMO UPO AINA MBILI. 

1:MTAZAMO WENYE MABADILIKO NDANI YA MTU.

2:MTAZAMO WENYE KUMFANYA MTU ASIBADILIKE NDANI YA MTU.


   1; MTAZAMO WENYE MABADILIKO 

Huu ni Mtazamo Wa Mtu kuyapa majira anayoyapitia majina yenye ushindi majina yenye kumpa matumaini mwenyewe. 

Mfano; Wapo watu hata wakiwa wanapitia kipindi kigumu kiaje hawakipi Jina Wanapitia Kipindi kigumu.

Wapo watu hata wakiwa wanapitia majira ya kutokuolewa au kuowa hakiiti Jina Amefungwa asiolewe au asiowe hukiita wakati Wa Bwana  bado.

MTAZAMO  huyapa majina majira ili kuyafikia yule mtu au kuyaishi lazima nguvu ya mtazamo  iyape majina.

Swali la Kujiuliza: Wewe Maisha Yako Umeyapa MTAZAMO ngani umeyaita majina ngani Badili huo Mtazamo kuanzia Sasa.


2:MTAZAMO WA KUTOKUBADILIKA.

Nikitendo cha mtu kuyapa majira majina ya yanayomfanya Ashindwe  kuyatafsiri vyema na kuyatatua hali inayomfanya aishi maisha ya kushindwa kila kitu.

Kushindwa Kwa Mtu hutengemea Mtazamo wako na Fikira zako unavyotafsiri majira.

Mfano; Mgonjwa mtazamo wake Unawaza Tiba Tayari Anawaza Ataponaje 

Yaitaji utulivu na Umakini Mkubwa Sana Kuirusu hali Mtazamo ndani yako iwe faida kwako ibadilishe Maisha yako.


FAIDA UTAKAZOPATA UKIWA NA MTAZAMO MZURI;

1:Utakuwa mtu wa maisha yaliyojaa ushindi kila ufanyacho.

2:Utakuwa Mtu  Mwenye Kuyabadilisha majira na kuyatatua katika nyakati mbalimbali kwa kuyatazama kiushindi.

3:Mtazamo Unanguvu Ya Kuyafanya Maisha yako yakafika mbali Sana.

4;Mtazamo utasimamisha dhulumba na mawimbi yote utakayokuwa unapitia.

5:Imani huzalishwa na Mtazamo wako utakavyoitafsiri.


HASARA ITAKUWA KINYUME CHA FAIDA.


TUFANYE NINI SASA.

Hakikisha Maisha Yako unayaongoza na kuyatazama katika MABADILIKO makubwa ndani yako ruhusu kuyatafsiri vyema nyakati mbalimbali unazozipitia ili uwe mshindi na uvuke katika vipindi vigumu.


HITIMISHO 
Tunapaswa Kuwafundisha na kuwaelekeza watu wajue Mtazamo ulivyo na nguvu kuyafanya mambo yetu yaende tutakavyo.

Wito.
Share chukua muda niulize swali kama hujaelewa inbox WhatsApp +255710889892

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
KANISA LA HOLY SPIRIT CHURCH TANZANIA 
MAKAO MAKUU MOROGORO VETA DAKAWA 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.