MAOMBI YA KUAMBATANA NA WATU SAHIHI

SOMO; MAOMBI YA KUABATANA NA RAFIKI SAHIHI.

Kuna marafiki wengine unaweza kuwa nao pasipokujua kumbe katika ulimwengu wa roho ni Antena za kichawi Adui Anawatumia marafiki ulionao Akunase kwenye Eneo lake. Siyo Kila rafiki ukajua ni rafiki mengine mapepo yanajivisha sura za marafiki zako kwa kuwa huombi na hujuagi kuomba unaweza ukashagaa toka umeshikana nae urafiki maisha yako yanazidi Kuharibiwa.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 
WhatsApp Group la Maombi na Mafundisho +255759861768

MAOMBI HAYA TUNASIMAMIA 
                "Mithali 18:24 "
 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍
ZINGATIA HILI;
============
Hakikisha Unapuguza marafiki wanaokupa hasara au ukiwa nao ndiyo majanga yanaongezeka Ambatana na marafiki unaona ukiwa nao unapiga hatua ya kiroho na unakuwa na ukaribu na Mungu.

NAMNA UTAKAVYOOMBA;

Piga Magoti ukiwa mahari Tulivu Omba Kwa Kusoma Sala hii.

Baba Yangu mfalme wangu wa Amani Rafiki mwaminifu kwangu tena mzazi mwaminifu unayejua kunilea umenipa hekima Nijue Kusimama mbele zako niyalete haya machache Bwana Nipo hapa Leo Unisaindie kufanya msako msako na uparation kwa marafiki zangu ulionipa na niliojipa mwenyewe kwa akili Zangu Najua wapo sahihi na Wasio Sahihi Ninaomba uwaondoe urafiki wangu na wao ambao Siyo Sahihi ukavunjike ukaribu ukaishe kabisa Kwa Jina la Yesu nibakizie marafiki Sahihi na Uliokusundia wewe Katika Jina la Yesu.Amen 
.Rudia ×4


KISHA SIMAMA HAPO ULIPOPIGA MAGOTI

NYOSHA MIKONO YAKO JUU PIGA MAKOFI USEME MUNGU NAKUSHUKURU RUDIA RUDIA KUSHUKURU 

Kisha utakuwa umemaliza hili. Maombi haya omba Siku Tatu mfululizo 


Shirikisha maombi haya na Watu wengine

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.