SOMO; WAJIBU WA MAMA MCHUNGAJI NA MCHUNGAJI NDANI YA KANISA.

SOMO; WAJIBU WA MAMA MCHUNGAJI NA MCHUNGAJI NDANI YA KANISA. 

UTANGULIZI 
Ni vyema somo hili liwafikie walengwa wapate kujua nini kinawapasa wafanye ndani ya kanisa Kwanza waelewe wao wanasimama kwa niamba ya Mungu wamepewa watu waongoze nakuwachunga Kiroho katika Kondoo hao wanapaswa wawajue vizuri nakujua zinzi lao na Aina ya malisho wànayowapa.
Zaburi:23;1-4 Malaki.2:7, Mathayo.5:14-16

Basi Upo namimi Pastor Richard nakuletea Nakala hii Ujifunze kitu fatana nami mpaka mwisho.

MAANA YA MAMA MCHUNGAJI ?
Mama mchungaji ni msaindizi wa mchungaji katika majikumu ya kutimiza wito wake anasimama kwa niaba ya mchungaji hata kama hayupo.

MAANA YA MCHUNGAJI?
Mchungaji ni msaindizi wa Mungu anayesimama kwa niaba ya Mungu kuwaongoza watu kiroho nakuwakuza kiimani.

MAMBO YA KUJUA NA YA MUHIMU KWA MCHUNGAJI NA MAMA MCHUNGAJI 
________________________________________

1;Mungu Amekuweka Kwa Niaba Yake Kumuwakilisha Kwa Watu wake.

2.Mungu Amekupa Kibali  Kuliko wengine Amekuamini Kuliko wengine fanya kazi kwa uaminifu

3.Mungu Ameweka Nguvu na Neema ya Kuvusha watu kwa mbinu mbalimbali ndani yako.

4.Usijilinganishe na mtu yeyote ukiwa wewe mama mchungaji au Baba mchungaji unatakiwa utimize maono na mshikamano kati yako na Mwezako.

5.Usisahau watu na Jamii inaangalia Mienendo yako na ushiriki wako katika jamii.

*"WAJIBU  WA MAMA MCHUNGAJI NA BABA MCHUNGAJI NDANI YA KANISA WANALOLIONGOZA*@

Waebrania:13:20,  1Petro.5;1-4

Kuna kondoo ndani ya kanisa watatu na kila kondoo anatambia zake yaani namanisha kwamba kunawaumini wa aina tatu ndani ya Kanisa kila muumini anatabia zake 
Ni vyema uwajue waumini unaowaongoza wakoje Karibu uendelee kupata ufahamu.

1:AINA YA KWANZA ni KONDOO WALIOPOTEA.
Hawa ni wale waumini au ni mkusanyiko wa waumini waliorundi nyuma kwa Sababu zao Binafsi au Kupitia Majaribu wanayokutana nayo wanaamua waache hata kwenda Kanisani hata kuhudhuria vipindi vya katikati.

Ukiwajua wala hutumii nguvu kuwafanya warundi kundini.

UNACHOPASWA UFANYE KWA KONDOO WA AINA HII
Nenda wafatilie ujue changamoto yao nini kwa nini Hawaii Kanisani Sikiliza kero zao waombee na kuwaambia Jumapili hii nikuone kanisani uje. Usikate tamaa kuwatafuta na Kuwarundisha Kanisani.
Ni Jukumu lako mama mchungaji  hili kumsaindia mmeo kufatilia watoto wako wa kiroho.
Soma: zaburi;11;16, Mathayo.18;12-13

2..AINA YA PILI Ni KONDOO WALIOTAWANYIKA.
Hawa ni mkusanyiko wa waumini ndanj ya kanisa wanaoyumbishwa na Kupeperushwa na upepo.
Wakisikia huku kuna uponyaji wataondoka kwenda kuna mganga anatibu watamfata wakisikia kuna mafuta au maji wataondoka ndani ya kanisa nakufata huo miujiza Hawapendi wafundishwe neno au kubadilika wawe kondoo waliotulia.

Watu hawa Huyumbishwa Na Kuruka Rika mara kanisani aje mara asije ibadani. Watu hawa hawajatulia kanisani hawaeleweki ni wanao au siyo wanao.

UNAPASWA  UFANYE HILI.
Hakikisha unawakusanya nakuwaweka wawe pamoja kisha wafundishe waijue kweli wasijifunganishe na mafundisho ya uongo au Kuharibu imani yao. Ni jukumu la Baba mchungaji na mama mchungaji kukaa na watoto wao wenye tabia kama hii.
Soma Isaya.40:11, Ezekieli 34;12

3.AINA YA TATU NI KONDOO WALIOTULIA KWENYE ZINZI WASIKIAO SAUTI YA MCHUNGAJI WAO.
Hawa ni Waumini Waliotulia ndani Ya Kanisa ni watu waliosimama na Kanisa hawarukiruki hawaachi kanisani ni waaminifu kuonekana katika ibada  ni watu wanaopenda kujifunza Nakubadilika kabisa.

UNAPASWA UFANYE HAYA.
Hakikisha Kundi hili Unaendelea kulikuza kiroho na kulilea zaidi ili lifanyike kuwa mabadiliko kwa waumini waliopotea au kurundi nyuma.

Soma Yohana.13:3-17 Isaya.40:11

TUFANYE NINI KAMA WACHUNGAJI. 
Tunatakiwa Tuwajue Kondoo tunawaongoza ili kuwasaindia zaidi kiroho nakuwalea kiroho Kupitia somo hili ufahamu nimekufungua kindogo ukiongeza na maarifa ya nakala za masomo ya wengine itakufanya ujenge kanisa bora.

HITIMISHO 
Tunaweza Kulijua kundi endapo tunapoamua kulilea na kufanya wito tulioitiwa.

Wito
Tumia namba hii Kumfata Pastor Richard WhatsApp Yupo Morogoro Veta Dakawa +255759861768


    KIAPO CHA UCHUNGAJI
========================
Mimi Mathew Majaliwa Sinkamba Ninaapa na Kupokea majukumu  ya Kuwa Mchungaji Wa Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania Na Kufata Katiba ya Holy Spirit church Tanzania na Kuilinda Na Kuitetee Kuanzia Leo Katika Jina la Yesu.Amen ×3

Wote Tuseme Amen



KIAPO CHA MAMA MCHUNGAJI 

Mimi Stara Joseph Moleli Ninaapa na Kupokea Majukumu Yote ya Kuwa mama mchungaji nikiitunza na kuilinda Katiba ya Holy Spirit church Tanzania na Kuitetea Katika Jina la Yesu.Amen 



        MSIMIKAJI KWA MCHUNGAJI 

Kwa Mamlaka niliyopewa na Kristo Yesu Ninakusimika Wewe Mathew Majaliwa Sinkamba Uwe Mchungaji Rasimi wa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania  Ukatumike Shambani mwa Bwana Katika Jina la Yesu. AMEN 



          KWA MAMA MCHUNGAJI 

Kwa Mamlaka niliyopewa na Kristo Yesu Ninakusimika wewe Stara Joseph  Moleli Uwe MAMA Mchungaji Rasimi wa Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania  Uende Ukawe msaindizi na mama wa wengi Katika Jina la Yesu.Amen 


Nitawaombea sasa.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.