SOMO; MAMBO AMBAYO HUPASWI KUYAONGEA NDANI YA NDOA.
👊DARASA LA WANANDOA 🤛
Karibuni Wanando ndani Ya Darasa Tusemezane Tujifunze Kitu mimi Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Nakuandalia nakala hii..
Wanandoa Tunapoingia ndani ya ndoa wengi wetu tulishawahi kuwa na mahusiano kabla ya kupata ndoa au Tulishapitia hali fulani familia zetu na wengine Tumetoka familia ambazo hazikutunza vizuri ndoa Wazazi wetu hawakuwa vizuri kukaa nasi kutufundisha juu ya namna Tunavyopaswa kukaa na wake zetu au waume zetu Kwa hiyo Tunapokuja kuingia maisha ya ndoa Tunaona kama magumu sana na tunaweza kukopi maisha ya wazazi wetu karibu ujifunze kitu hapa naamini utapata kitu.
1:UKIOLEWA/KUOWA NDANI YA NDOA USITOE SIRI ZA HALI YA UZAIFU KWA WAZAZI WENU BAADALA YAKE MWAMBIENI BABA WA KIROHO AWAOMBEE.
Mfano mkeo umemuowa lakini kwenye tendo la ndoa kuna shida hakuhudumii ndani au umekuta anamatatizo sehemu zake za siri au Zipo mara mbili za kiume na za kike umeingia naye kwa ndoa Usiaze kuwaeleza rafiki zako nje.
Nawe Bint mfano mumeo Hana Uwezo wa nguvu za Kiume unapoingia kwenye tendo la ndoa Hawezi Usimwimbie mama yako au Baba yako mweleze Baba Wa Kiroho Aliombee hilo.
Mithali;14;1
2;USIAZISHE STORY UKIWA NA MKEO/MUMEO KUONGELEA WAPENZI WA ZAMANI AU WATU WA NJE AMBAO ALISHASIKIA UMEZAA NAO.
Rejea
MITHALI; 19;11
Kuna Wanaume Wanatabia hii Unakuta mke hajabahatika mtoto Anatoka nje ya ndoa Anazaa nje ya ndoa anaanza kumkusanyia watoto awalee Mwanamke Amepewa Neema ya Uvumilivu lakini Akichoka hii huleta Athari akilini mwake na kuifanya ndoa Yenu msiwe na maelewano ndani.
Tunza heshima ya mkeo ujue Anacheti Serikali na madhabahu inamtambua hao wengine usiwaongelee ukiwa na mweza wako unamuumiza machozi yake nikifungo kwako.
3:USITAMKE CHANGU NI VYANGU SEMA VYETU.
Mwanzo;2;23
Hii ni Siri nyingine inayokuwa inatengani mwili mmoja na kuweka tofauti Ni Kauli inayowakera Wanandoa Wengi Mfano umenunua kiwanja kwa hela yako unasema hiki changu Sababu hukutoa chochote Wewe.
Biblia inasemaje kuhusu hii tabia
Mwanzo 2:23
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
4:USIMSEME VIBAYA MZAZI WAKE AU MLEZI WAKE
Hata Kama Wewe Wazazi WAKE Huwapendi Unazijua Tabia Zao Mbaya Hufurahii mienendo yao eidha Baba yake au Mama usiongee mbele yake maneno mabaya Linda kinywa chako hata kama mama yake mchawi na unajua Anakutesa Wewe Usiseme mama yako mchawi baadala yake Mwambie Baba wa Kiroho Akusaindie kuomba.
5:USIAZISHE STORY ZA KULAUMU AU ZINAZOKUMBUSHIA ASIYOPENDA.
Mithali;12;1
Kuna Watu Ambao Huwa Hawapendi Uwakumbushie Makosa yao au Kule walitoka Mwangalie Mweza wako kama anaona Kuna vitu vinamuuma nakuondoa Amani kwake Usimwambie.
NIMALIZE KWA KUSEMA TUFANYE NINI SASA.
Tujenge ndoa Zetu Tuangalie Vitu Vinavyofaa na Vile Visivyofaa Mazungumzo Yetu Yatawaliwe na Amani ndani Ya ndoa.
Sisi ndiyo Wanandoa na Wajezi WA ndoa Zetu ni Sisi Wawili Hakuna watatu basi Tulinde ndoa zetu.
WITO
Kama Hujaungwa Kwenye Group la Maombi na Mafundisho mazuri kama haya muombe Baba Yetu Wa Kiroho Pastor Richard Akuunge WhatsApp +255759861768
Maoni
Chapisha Maoni