SOMO; MAOMBI
SEMINAR :TOPIC: ✍️π MAOMBI
Mwalimu; Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768
Tufunue Vitabu hivi;2Mambo ya nyakati:7:14-16 1Wafalme;8;38-49 Zaburi;61;1,86;6 1Petro;3;12
SOMO HILI AU WALAKA HUU UNASURA "5"
A:MAANA YA MAOMBI
B; MAKUNDI YA MAOMBI
C;SEHEMU ZA MAOMBI
D:TABIA YA MAOMBI
E: HITIMISHO
UTANGULIZI.
π✍️SIKU YA KWANZA; Tarehe 3/8/2020 Jumatatu muda saa;4;00-6;00
AππMAANA YA MAOMBI NA UFAFANUZIq WAMAOMBI ππ
1:MAOMBI NI NINI??Ni Hali ya uwasilishaji wa Taarifa na maendeleo ya Mtu Kiroho na Kimwili mbele Za Mungu Yenye Kutaka Apewe Majibu na Anachokiomba Nakukiamini.
Bππ✍️KUNA MAKUNDI MAWILI YA MAOMBI;(WANAPOOMBA)
✍️Kundi la Kwanza Ni la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua
✍️Kundi la Pili Ni la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua
C:KUNA SEHEHEMU TANO ZA MAOMBI MTU ANAPASWA AZIJUE.
1:AINA ZA MAOMBI ANAZOPASWA MKRISTO AOMBE
2;MIKAO YA MAOMBI ANAZOPASWA MKRISTO AKAE WAKATI ANAOMBA
3;STAYLE ZA MAOMBI MKRISTO ANAZOPASWA APITIE
4:MBINU ZA MAOMBI NAKUKABILI TATIZO MKRISTO ANAVYOPASWA
5;MUDA WA MAOMBI MKRISTO ANAOPASWA AOMBE
D:TABIA YA MAOMBI
✍️Tabia ya Maombi ya Mazoea
✍️Tabia ya Maombi ya Kujitoa
✍️Tabia ya Maombi ya Nguvu
✍️Tabia ya Maombi Madhaifu yasiyo na nguvu.
E; HITIMISHO
Hapa Somo Letu Na Semina Ya Wiki moja Kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili Itakuwa imeisha
KARIBU Semina YETU
π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯
SEHEMU: A : MAANA YA MAOMBI
Maana Sahihi ya Maombi Ni Pumzi Yenye uhai wa mkristo yoyote yule ili ukristo wake uimarike Unaitajika Maombi "AFANYE MAOMBI"
MAANA HALISI MAOMBI π✍️Ni uhai wa mtu aliyeokoka au mwokovu a
Maana ya Pili; Maombi Ni Uwasilishaji wa maendeleo ya Mtu mbele za Mungu Yenye kutaka Apewe jibu juu ya alichokiwakilisha.
NANI ANAPASWA AOMBE ?
Ni Mtu Yeyote Yule ANAPASWA aombe Juu ya anachokitaka kwa Mungu
KATIKA UWASILISHAJI MTU MAOMBI HUWA YANAWEZA
1;Kuchukua Muda Mrefu
2;Kuchukua Muda Mfupi
MAOMBI YA KUCHUKUA MUDA MREFU NI MAOMBI Yanayochukua muda mrefu mtu mpaka Apokee inaweza kuchukua mwaka Kuchukua Miaka mtu ndio anajibiwa
MAOMBI YA KUCHUKUA MUDA MFUPI hii huwa ni Maombi Yenye kuchukua muda mfupi mtu anapokea hitaji lake.
2mambo ya nyakati : Mlango 7
15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa
TUNΓENDELEA SURA YA PILI; ✍️SEMINAR SIKU YA PILI✍️Jumanne;4/8/2020
Muda Kuanzia Saa;4;00-6;00
Tumeshaona Maana ya MAOMBI Katika Sura "A" Jana Tumejifunza Maana HALISI ya MKRISTO MAOMBI YANAMAANA GANI??
Maswali Ya Jana Yalikuwa??:
Kwanini Tunaomba hatujibiwi Wakati Baba Yetu Anatuombea Mbinguni "Yesu Kristo""?
Jibu;
Baba Yetu Alituagiza nasisi tuombe tusikae na kusema Yupo Yesu Ananiombea Wakati wewe umekaa Akasema amfatae lazima ajitaambishe kuutafuta Ufalme wa Mungu
Luka : Mlango 11:9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa
KUNA MAKUNDI MAWILI YA MAOMBI
1:Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua
2;Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua
Tuanze Kujifunza Kuangalia Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua
Hili Kundi likoje Tutaliona nakujifunza mengi.
1;KUNDI LA WATU WANAOMUOMBA MUNGU WANAEMJUA.Yohana:14;25-26
Hili Huwa Ni mkusanyiko wa wakristo waliopata Neema ya Kumjua Mungu wao Vyema Kupitia Neno la Mungu kuona Kujifunza.
Maana ya Pili ni Watu wanaojua vyema UWEZO wa Wanachokiamini Nakukitumaini.
MUNGU NI NANI?
Mungu Ni roho aliyeziumba roho zingine hii ukijua Ni rahisi Kuelewa kipi unapaswa Ukiombe.
CHOCHOTE KILICHOUMBWA NA HII ROHO; Hupaswi kukiomba au kuaminishwa Ukiombe katika maisha yako ya ukristo Ujue Mungu wako Ni ROHO.
Mfano Wapo watu huomba Mizimu na Wegine Wapo ndani ya kanisa Wegine Ni Manabii Wachungaji au Wanamaombi Wazuri Kumbe roho za mizimu zinawapa mafunuo na kuwaelekeza wakatoe Sadaka wengine wakaabudu Makaburini Usiku wa manane
Wapo watu huamini majini mazuri na huwa Wanaanza kuyaomba mtu Yeyote Yule atakayeabudu au Kukiomba Kitu KILICHOUMBWA na Mungu huwa Tunasema Anaabudu au Kumuomba Mungu asiyemjua Tukisimama na Kumwabudu na Kumuomba Mungu wa Kweli Mungu hujibu tusimchanganye tu
MUNGU WA KWELI NI MSAFI HAPENDI UOVU.
Ukiingia Kwenye Maombi uingie ukiwa hauna uchafu hujamuweka mtu maana Mungu wako Ni Msafi ukiingia Kuomba TU ukaomba huku umemuweka mtu au huachi pombe huachi Uchawi huachi Uzinifu huachi kutokuwasamehe watu ujue Utakuwa umejiondoa katika Kundi la Watu wanaomjua Mungu.
IMANI YENYE KUMJUA UWEZO WA UNAEMUOMBA
Kabla ujaomba lazima akili yako ijipime Mungu uliye nae Anaweza Yote Au Mengine Ni Wewe unaweza Kuyatatua
UJue Kwamba Mungu hujishughulisha Sana NA YALIYOKUSHINDA KWA AKILI YAKO NA UFAHAMU WAKO
Mambo yanayotatulika kwa Akili na Ufahamu wako huwa Anaachia Akili Yako na mastiff yako ifanye kazi.
Wapo watu Wanamchanganya Mungu Sehemu wanapopaswa watumie akili wao wanatumia nguvu sehemu wanapopaswa watumie Ufahamu wait wanatumia Pesa au Maombi
MUNGU WA KWELI ANATHAMINI SANA AKILI NA UFAHAMU
Kwa hiyo sio kila Kitu uombe vitu vingine vinaitaji utumie akili tu na Ufahamu
MAMBO YANAYOMDHIHIRISHA MTU ANAE OMBA MUNGU WANAEMUJUA
1:Huwa wanakuwa Waaminifu Kati yao na Mungu
2;Huwa Wanatumia Akili na Ufahamu pale pakutumia Ufahamu
3:Huwa Na nguvu ya Kumtengemea Mungu
4: Huwa Wanaamini Ubatizo Ufufuo na Ukombozi wa nafsi
5:Huwa Wanaamini Sio Kila anenae kwa Roho Ni Roho Mtakatifu
6;Huwa wanamaandalizi ya Maombi
7;Huwa wanajitenga Mbali palipo na uwepo wanapoomba
8:Huwa wanajua vyumba Vya Maombi
9;Huwa wanajua Tabia za Maombi
10;Wanajua umhimu na Maana Ya Maombi
Hizi Ndio Dalili Zinazomjulisha Mtu aombaye Maombi kwa Mungu Anayemjua
2:KUNDI LA MAOMBI YA WATU WANAOMUOMBA MUNGU WASIYEMJUA
Hili huwa Ni Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua nakutambua uwezo wake
Hawa Ni wapinga Kristo na Wapaganii au Muumini Anayeabudu KILICHOUMBWA na Mungu huyo naye Huhesabiwa Anaenda tu kanisani kukiabudu asichokijua
MUNGU ASIYEJULIKANA NI
1:Mizimu
2:Mapepo ya uaguzi kusoma nyota nk
3:Majini Kuyaabudu nakusujudia
4;Wachawi na Waganga huabudu Mungu Asiyemjua.
Tabia za Mungu Asiyemjua
1;Kukuongoza katika Uharibifu wa maisha yako au Wegine
2;Ulevi,Uzinzi,na Uchafu wote anakuogoza nakanisani unaenda unasimama Madhabahuni
3;Hukutazamisha Imani ione Pito linanguvu kuliko Mungu.
MAMBO YANAYOMDHIHIRISHA MTU ANAE OMBA MUNGU WASIYE MJUA
1;Huwa Mioyo Yao inaingia Maombi wakiwa nakinyongo
,2;Huwa Wapo gizani Wegine Hawajui Kama Wapo na Mungu wasiomjua
3:Huezi Mira na Matambiko ya kwao
4;Hurishana vitu na kutumikia miungu migeni
5:Huwa hawajui Uwezo na UKuu wa Mungu wa Kweli
6:Wanatumika na Ushirikina Uganga hirizi na mafundo.
7:Huwa Wanaamini waganga Ndio Tiba kwao
8;Huwa Hawapendi Maombi
9;Huwa Hawataki Habari za Wokovu wa Mungu
10;Huwa Hawajui Maana na uhalisia wa Maombi kwa mkristo
Hizi Ndio Dalili Zinazomjulisha Mtu aombaye Maombi kwa Mungu Asiyemjua.
Kesho Tutaendeleaa Sura ya 3; SEHEHEMU KUU 5 ZA MAOMBI
SWALI;
Kwanini watu Wasiomjua Mungu Wanamuomba Mungu na Anawajibu Kwanini Sisi tunamuomba Mungu na hatujibu..?
JIBU;Watu wasiokuwa wa Mungu wasiomjua Mungu humuomba mungu sio Mungu
Kwa hiyo huwakilisha utawala wa Shetani Ambao Upo unamiliki
1Wafalme;18:35-40
2mambo ya nyakati : Mlango 33
18 Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli
LEO NI SIKU YA TATU YA SEMINA YETU JUMATANO LEO TUPO SURA YA 3
TUNΓENDELEA a....
Tumeshaona Maana ya MAOMBI na Makundi ya Watu Wanaomba Leo Tunaangazia Sehemu Tano au Vyumba vitano vyakuingia unapoomba TUTAINGIA CHUMBA KIMOJA KIMOJA ILI UELEWE
πππππππππππππππππ
"Sura ya 3; SEHEMU KUU TANO ZA MAOMBI"
TUTAINGIA CHUMBA KIMOJA KIMOJA KATIKA CHUMBA
CHUMBA CHA KWANZA; Karibu Tuingie Tukione
Seminar Jumatano Tar;5/8/2020
Mwal Pastor Richard
Mwadaaji:Roho Mtakatifu
πͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺπͺ
CHUMBA CHA KWANZA "✍️AINA ZA MAOMBI ya MAOMBI MKRISTO ANAZOPASWA AOMBE.
Mkristo Unapaswa Ujue Aina Za Maombi Unazopaswa Uombe Na Hii itakusaindia Kupambana Vyema Kiroho Sio Kwenda kwenda TU au Kuomba Omba tu.
Kuna Aina Tano za Maombi Mkristo Unapaswa Uzijue
1:Maombi ya Sifa na Toba
2:Maombi ya shukrani
3:Maombi ya Vita na Ukombozi
4:Maombi ya wote
5;Maombi ya Binafsi peke yako
1:MAOMBI YA SIFA NA TOBA
Haya huwa Ni Maombi unayopaswa umsifu Mungu nakumtukuza kwa Yale machahe anayokutendea Na Utubu pale ulipowaza au Kufikiri kinyume kwa Ajili yake
✍️✍️MAOMBI YA SIFA✍️✍️
Zaburi : Mlango 143
7 Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea;Usinifiche uso wako,Nisifanane nao washukao shimoni
MAOMBI YA SIFA YANAKUWA HIVI
:1 Tamka umwinue Mungu na Umsifie ✍️mfano;Hakika wewe Bwana unaweza hata Hili nililofikilia Kuwa ngumu Kwako KUMBE ndogo Sana Haleluyaaa Bwana Unanifurahisha Nasema Shetani na ugonjwa huu kwangu hauniwezi maana ninae Baba mwenye nguvu Katika jina la Yesu Amen π
2; Sifu Matendo Yake hata Kama unamuona Kachelewa✍️Mfano:;Nikakupigia Makofi Bwana wa Mabwana Ansate kwa Kujibu nilichokuomba Unajua Baba Nakupenda Sana sababu kila nikiomba unajibu Na sema pokea Sifa halafu piga Makofi kwa Bwana.
3;Cheza Sifa Kabisa✍️Mfano: Imba Mimi Ni Wa Juu..Juu Juu Sana Shetani Ni was chini...chini Sana
Wimbo 2;I Love you Dady...I Love you Dady Forever I Love you Dady..
Sifu huku Ukicheza.
4;Abudu Kwa Moyo Wote✍️Mfano;Amen,,Amen,,Amen,, Haleluyaaa Haleluyaaa Ha..le..luyaaaa
TOBA
Unatakiwa Umuombe MSAMAHA Mungu kila unapomkosea
Mfano;Piga Magoti uombe Eeh Bwana Naomba unisamehe nimekuwa nikinug.unika nikiwaza mabaya nisamehe Baba yangu ππ
2;MAOMBI YA SHUKURANI
Haya huwa Ni Maombi unayopaswa uombe Umshukuru Mungu Kila wakati kwa wema wake.
2Wakoritho : Mlango 9
11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu
MAOMBI YA SHUKURANI YANAKUAJE
1;Tamka Maneno ya Ansate nyigi ✍️Mfano;Ansate Bwana,,,Ansate Yesu Umefanya kwangu,,,Nakushukuru Wewe Bwana
2:Thamini Madogo Madogo Unayotendewa✍️Mfano; Hili Mimi Namshukuru Mungu Tu
3;Kumbuka Aliko Kutoa Mungu✍️Mfano;Yaani Mimi Nilikuwa nife lakini Mungu aliniokoaa
44
3;MAOMBI YA VITA
Haya huwa Ni Maombi ya kupigana nakunyaganyana Umiliki wa Kitu kwa nguvu ya Kiroho hii huwa Unatakiwa Upambane Kiroho Vita Kweli Kweli.
2Wakoritho : Mlango 10
3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili
MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA MAOMBI YA VITA.
1:Usiweke mtu moyoni au Mawazo✍️ Mfano:Unaomba huku Unamtu umekosana nae utapingwa tu.
2;Tamka Maneno kwa Kukaza Ulimi au Amri✍️Mfano;Achia Toka Pingwa
3:Kuwa Makini Unapotaja YESU usitaje yesu Neno la Mungu tumia vizuri.
Neno linasema hatupingani Kimwili Nakupinga Pingaa Kwa Jina La Yesu 2wakoriho:10:5 Kila Elimu iliyojiinua mbele yangu naivunja nabomoa kwa Jina La Yesu...endeeleeeeaaa
4:Tumia Siraha hizi
MOTO WA YESU
Mapanga
Roho Mtakatifu
Malaika wa Vita/Moto
Jina la Yesu
Neno
Na Siraha za Kimwili zilete katika Roho..
5:Omba huku Unatembea na Kufanya Kitendo
6;Kabla hujaanza Omba Malaika wa Maombi ya Vita
7:Ukimaliza Yafunike Kwa Damu ya Yesu Maombi Yako
4;MAOMBI YA WOTE
Haya huwa Maombi yanayoombwa na wote watu zaidi ya mmoja
MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA HAYA MAOMBI
1:Tamka kuwaombea wengine✍️Ombea wagonjwa Wenye HITAJI
2;Ombea watu Wengine eidha kwa Makundi Makundi au Kwa Majina✍️ Mfano Naombea Wagonjwa Katika jina la Yesu π Naombea wadongo Zangu wafaulu mitihani Yao....
3;Wafunike Kwa Ulizi wa Mungu.
5: MAOMBI YA BINAFSI
Haya huwa Ni Maombi yakujiombea mwenyewe TU usiombee Wegine.
MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA
1;Tamka maneno yakujiombea mwenyewe TU✍️Mfano;Mungu Unisaidie nipate kazi
2;Kumbuka kuyafunika kwa ulizi Maombi yako.
CHUMBA KIMOJA TUMEKIMALIZA KESHO Tutaendeleaa Chumba Cha Pili Cha Maombi
✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️πͺππππππππ
KARIBUNI KATIKA SEMINAR SIKU YA 4 ALHAMIS
Tar:6/8/2020
Mwal; Pastor Richard
CHUMBA CHA 2:MIKAO YA MAOMBI
MIKAO MAANA YAKE✍️Ubunifu wa Kuomba Kama mkristo UNAJUA UBUNIFU WA KUOMBA
KUNA MIKAO 6 YAKUOMBA
1;MKAO WA KUSIMAMA
2:MKAO WA KUPIGA MAGOTI
3;MKAO WA KUSUJUDU
4;MKAO WA UMEKAA
5;MKAO WA UMELALA
6;MIKAO WA KUTEMBEA
Maoni
Chapisha Maoni