SOMO:SIFA ZA MWANAMKE MUOLEWAJI

DARASA LA UCHUMBA 

SIFA ZA MKE MUOLEWAJI

🌴👉👉🌴🌴🌴🌴🌴
SOMO: HIZI NDIYO SIFA ZINAZOKUJULISHA HUYU NI MWANAMKE WA KUOWA. 

Kila Palipo na Mwanaume muoaji ujue yupo mwanamke mwenye Sifa za kuolewa Ambazo huwa hazipishani Sana na Sifa za Mwanamme muoaji. Ukiona hizi sifa huyo mchumba wako hana ujue siyo mwanamke wa kuowa.

Naitwa Pastor Richard Ninayekuletea Somo hili fatana nami.
Karibu ujifunze kitu



1:Mwanamke Muolewaji Atakupa Nafasi Ya Kwanza Kwenye Maisha Yake.

Mkiwa kwenye uchumba utaona haachi kukujulia hali  atakuwa tayari kufanya chochote Kwa Ajili yako kilicho ndani ya uwezo wake Kwenye Uchumba tu vitu vingi mtaanza kubadilisha nakutengenezana.

Ukiona wewe mwanaume unatumia nguvu sana kumfanya awe mke wako ujue sawasawa unataka kubemba Junia la misumari kichwani mwako.

Soma Mithali:18:16




2:Mwanamke Muolewaji Anaheshima na Adabu Kwa Watu Wote.
.
Mwanamke muolewaji utamjua katika uvaaji wake Utamjua Katika Tabia zake Na Mienendo Yake Unapoongea anakuwa makini kukusikiliza na Anapokujibu Anakujibu kwa heshima siyo kwako tu atafanya hivyo kwa watu wote. Huwa kio na barua inayosomeka vizuri kwa Jamii na Kanisa.

Soma Warumi;12:10



3:Mwanamke Muolewaji  Hana Haraka ya Kufanya Tendo la ndoa nawewe .

Mwanamke Muolewaji ukimtaka kimapenzi kabla hujamuowa au Kufata taratibu hukataa akiitaji ufate taratibu ukiona mwanamke Anajirahisisha kwenye uchumba anataka mzini au mzae naye ujue huyo hakufai Kumuweka ndani akawa mkeo.

Soma Mathayo;5;27




4.Mwanamke Muolewaji Humpenda Mungu Sana Anapenda Ibada Sana.

Mwanamke muolewaji hupenda mambo ya ibada hupenda kanisani ukiona mwanamke kanisani hapendi hata mambo ya Mungu hataki yupo bize na Waganga au Dunia hii Huyo Mwanamke hakufai kuowa.

SOMA Kumbukumbu la Torati;6:5




5:Mwanamke Muolewaji Anahekima Na Nimuelewa Sana.

Mwanamke Muolewaji  Anahekima na Busara Anauwezo wa Kuvumilia na Kukushauri vyema nakuona hatari mbele yako kabla haijakutokea Atatumia Hekima Yake Kujenga Uhusiano wenu.

Soma Mithali;14:1



6;Mwanamke Muolewaji Hutambulisha Uchumba wenu.

Mwanamke Muolewaji atakutambulisha kwa mchungaji wake atakutambulisha kwa ndugu wa karibu na Kwa Wazazi atakuwa tayari kukupeleka hataishi nawewe kabla ya wazazi wake kukujua.

Soma  Kutoka;20;12



7.Mwanamke Muolewaji Husamehe.

Mwanamke muolewaji husamehe na hapendi kuhifadhi vitu vinavyomuuzi  lazima atakuambia unapomkosea au Kumkwanza.

Ukiona mwanamke hapokei Simu zako au Amekublock ujue huyo mwanamke usimuowe hafai kuitwa mke.

Soma Mathayo;6;14-15




8;Mwanamke Muolewaji Huwa mpambanaji Anajitambua Nafasi yake Kama mwanamke. 

Mwanamke muolewaji huijua Nafasi yake huwa mpambanaji hamtengemei mwanaume Anapenda Ajishughulishe na Mia Mia hujali familia yake Hutunza famillia yake hujilinda mwenyewe na kila hatari yenye kutishia ndoa yake au mahusiano yake.

Zaburi;128;3-4



9.Mwanamke Muolewaji Anahofu Ya Mungu.

Mwanamke Muolewaji  Huwa Anakuwa Na Hofu ya Mungu utaweza kumtambua Jinsi alivyo na hofu na Mungu.

SOMA 2 NYAKATI; 19;7


10; Mwanamke Muolewaji Huongozwa Na Upendo Wa Dhati.

Mwanamke Muolewaji  Huongozwa na Upendo wa Hali ya Juu Sana Atakupenda hivyo ulivyo bila Kuangalia uwezo wako au hali yako ya Kimaisha.

SOMA 1WAKORITHO 13:4


HIZI NDIYO SIFA ZINAZOKUJULISHA MWANAMKE MUOLEWAJI ALIYETAYARI KUTENGENEZA MAISHA NAWEWE YA NDOA.


KWA USHAURI NIFATE INBOX WHATSAPP +255710889892



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.