SOMO:MAOMBI YA KUSHUGHULIKIA NA ROHO ZA KUPOTEZA VITU.

MAOMBI YA KUSHUGHULIKIA NA ROHO YA KUPOTEZA VITU KUTUMIA PESA VIBAYA ROHO YA UFUKARA.

Habari Kamanda Wa Bwana Yesu Mwanamaombi Mwezangu Nataka Nikufundishe Kitu Katika Ulimwengu wa Roho Huwa ipo roho inayomtumikisha Mtu mambo haya
1.Umasikini uliopitiliza
2.Kupotelewa na Vitu mara kwa mara
3.Kupata Pesa lakini inakuwa na matumizi yasiyo ya maendeleo inaisha tu bila kujua imetumikaje.

Hii Roho huitwa Ratifa ni Jini Linalohakikisha inapomwingia mtu linamshika kumutumikisha bila kujielewa.

Waefeso:6;12 

MSTARI HUU TUNASIMAMIA SOMA.
👇👇👇👇👇👇👇
2 Wakorintho 10:3-4
[3]Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 


WANAOPASWA KUOMBA MAOMBI HAYA NI WATU HAWA.

1.Wanapotelewa Na Vitu ovyo ovyo au Kudhurumiwa,Wanaotumia Pesa ovyo wanafanya kazi lakini hakuna wanachofanya cha maana walio masikini kupitiliza au wanaona wanafatiliwa na roho hiyo.

2.Wataomba bila kuacha mpaka Waone mabadiliko

3.Hutakiwi Ufunge haya maombi huyatolei Sadaka hayana maelekezo ya Sadaka. 

4.Utafata ninavyokuongoza kuomba na ni vizuri ukayafoward yakakaa kwenye inbox au ukayaandika ili usipoteze.



JINSI YA KUOMBA  MAOMBI HAYA.

1.Ninavunja Kila mawasiliano kati ya mikono yangu na roho ya kupoteza vitu kama pesa nguo za ndani nk ninaharibu kila dalili na viashilia vyote vinavyoonekana kunitumikisha kuanzia Leo  Katika Jina La Yesu.Amen 


2.Naharibu mwasiliano kati ya Akili zangu ufahamu wangu na roho ya kunitumikisha nikipata Pesa nazitumia kwa matumizi mabaya natumia kula starehe natumia kulipa madeni natumia kununua nguo kusuka kununua gari wakati hata kiwanja Sina nyumba sina lakini natumia pesa kwenye uzinzi kwenye Kufanya mambo yasiyo ya msingi Pesa yangu ikawe na mahusiano nawewe Mungu Ikawe na nguvu ya kufanya mambo yanayoonekana katika Jina la Yesu.Amen 


3.Nimeamua nibadilike katika mikakati ya matumizi ya kila Pesa ninayoishika mkononi mwangu kila mwezi nitafanya jambo litakalonipa faida nakuacha Alama Kwangu Katika Jina la Yesu.Amen 

4.Nakiri mimi kuchukia kuchukia roho ya wizi wa Fungu la kumi ninaomba unipe madhabahu na Baba atakayeniongoza na Kunilea Kiroho shuhudia ndani yangu Sitaki nitoe fungu langu la Kumi Katika Madhabahu Ambayo si Yangu shuhudia na useme nami kwa Uwazi naahidi na huyo Baba Wa Kiroho utakayenipa  nitakuwa mwaminifu na nitafata anavyoniongoza ili nifunguliwe Katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia×4
.

5.Kila Umasikini na Kila Roho ya Kuniendesha Katika mawazo ya kimasikini masikini ninaamuru iniachie na iondoke Kabisa kwenye damu yangu kwenye kufikiri kwangu Naharibu Naharibu ndani yangu kwenye mawazo yangu iniachie Katika Jina la Yesu.Amen 

6.Endelea Sasa Kuomba maneno yanayokuja kinywani mwako omba tu.


HITIMISHO 

Tambua Maombi Pekee ndiyo njia Ya wewe kupata suhulisho ya Hali ya ufukara na umasikini kuondoka

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.