SOMO:MAOMBI YA KUOMBA UNAPOTOA ZAKA,

SOMO; MAOMBI YA KUOMBA UNAPOTOA ZAKA(FUNGU LA KUMI).
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Soma Maandiko haya Tunayosimamia.
Malaki:3:8-14, Luka,;18:10-12, Nehemia:13:12 Mwanzo;14;20 Kumb.Torati:14:22


MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUTOA ZAKA(FUNGU LA KUMI)

1.Usitoe Zaka Kama Siyo Kwa Baba Yako Wa Kiroho AU Madhabahu yako.

1wafalme;18;30-35 Mwanzo;22;1-19


2.Ukianza Kutoa Zaka Usimwimbie Tena Mungu au Kuacha maana utatembea na laana ya wizi wa fungu la kumi.

Soma; Malaki:3:8-9

3;Fungu la Kumi ukilitoa Kwa Baba Yako wa Kiroho Katika Madhabahu yako litakubariki na Utainuliwa Juu mengi yatafunguliwa.

Soma Malaki;3;10-14

4 Baraka mbalimbali  huja kwako unapokuwa na msimamo wa fungu la kumi 
Kumb. Torati:28:1-20

5;Toa Fungu la Kumi ujue unayempa ni Mungu na Siyo Mwanadamu Ukitoa zaka mwambie Mungu nimekuwa mwaminifu wa Kutoa fungu la kumi fanya nami yangu haya.
1.Naitaji ndoa, 2.Naitaji nipande cheo kazi 3.Naitaji mapacha sita Naomba unibariki mpaka nishagae.

Matendo;10;1-5, 1samweli.1;1-14

6; Weka Angano moyoni mwako na Mungu hutamwimbia Fungu la Kumi Tena. Hutakuwa Anania na Safira.
Matendo;5;1-10


HUTAKIWI ZAKA AU FUNGU LA KUMI  UPELEKE KWA.
.1.Yatima, Wajane,Wagonjwa, n.k

Kwa Andiko hili; Malaki;3;10 Inakuangiza ni sheria Utoe zaka kwa uaminifu kwa Baba yako wa kiroho ili hata maombi yako yawe na nguvu ubarikiwe nakufungua madirisha ya mbiguni uyafukuze magonjwa laana na mikosi. Hii ndiyo huwa imani iliyosafi ukiwa mwaminifu wa zaka kwa Mungu.
Soma. Waebrania;11;5


Sadaka Za Waitaji Unatakiwa upeleke kwa yatima wajane wagonjwa hii huwa ndiyo Dini iliyo safi πŸ‘‡πŸ‘‰Yakobo;2;27


JINSI YA KUTOA  ZAKA/FUNGU LA KUMI. 

1:KWA MFANYA KAZI SERIKALINI/BINAFSI

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Kama Unafanya Kazi Mshahara wako 1000000 Lakini hii hela inakatwa mifuko mbalimbali kama Nssf,Bima,Bank unakuja kupokea 700,000 Hutapingia hesabu ya 700000 Bali utachukua hesabu ya 1000000 
Ambayo Fungu la Kumi ni 100000 Laki moja.
Utatoa Kila mwezi

Kama Unapokea 800000 Mshahara wako lakini unadaiwa bank ,unakatwa kwenye mifuko yako Unakuja kushika mkononi 400000 utapigia hesabu ya 800000 Laki nane ambayo ni Sh.80000 Utaitoa


2;KWA MFANYABIASHARA YOYOTE YULE;

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Kama wewe unaduka au unatembeza kibiashara chochote kile Γ¬li kiendelee kukua kitolee Fungu la Kumi Tena kwa Uaminifu.

Utauza mauzo yako kila unachouza unaandika 
mpaka Tar 30 mwisho wa mwezi Chukua Jumla ya  mauzo yote Jumlisha 

mfano kuanzia Tar.1-30 Jumla Ya Mauzo 500000 Laki Tano.
Utatoa 50000 kwa ajili ya Fungu la kumi unaiombea hilo fungu kuhusu biashara yako.
Fanya hivyo kila mwezi tu.

Kama ulizungusha ukauza na ukanunua tena bidhaa na mwezi umefika fungu la kumi huna utauza mauzo utakayouza utatafuta fungu la kumi. Kwa hiyo unatakiwa zungusha biashara yako mwezi mzima lakini kumbuka kuandika mauzo. 
Unapotuma Fungu la Kumi ombea Biashara yako ili mauzo ya ongezeke.

3:KWA MKULIMA YEYOTE YULE.

✍✍✍✍✍✍✍✍
Mkulima yeye fungu lake la kumi analitoa pale anapovuna mazao Yake Shambani.

Mfano  Umepata Junia Kumi Mpe Mungu gunia moja peleka kanisani.

Umevuna Gunia Debe na Nusu peleka kwa Mungu 

Ukifanya hivyo utaona mazao yanavyofunguka utakuwa mtu wa kuvuna Sana

Kumbu torati;28;1-5





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.